19 May, 2011

VIJISENTI VINAPOSHINDWA KUKUSAIDIA..

Mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF) bwana Dominique Strauss-Kahn ambaye pia ni mwanasheria,mwanasiasa na mwanauchumi wa kifaransa amewekwa jela Marekani kufuatia madai ya kutaka kumbaka mhudumu wa Hotel (Hotel Maid).Baada ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kufuatia kitendo hicho bwana Strauss-Kahn kupitia mwanasheria wake aliomba aachiwe kwa dhamana ya (vijisenti)  Dollar Million moja ($1m) mahakama ilikataa dhamana hio na kumrudisha rumande.


                                       Aliyekua mkurugenzi wa IMF-Dominique Strauss-kahn 

Kufuatia skendo hio mkuu huyo wa IMF amelazimika kujiuzulu wadhifa wake ambapo Umoja wa nchi za Ulaya (EU) wamesha tangaza kinyang'anyiro na wagombea wa awali ni kama ifuatavyo:-

  • Mohamed El-Erian, Egypt

  • Stanley Fischer, Israel

  • Gordon Brown, UK

  • Kemal Dervis, Turkey

  • Peer Steinbrueck, Germany

  • Montek Singh Ahluwalia, India

  • Christine Lagarde, France

  • Agustin Carstens, Mexico

  • Trevor Manuel, South Africa

  • Axel Weber, Germany
  • ETI JUMAMOSI TAREHE 21/05/2011 MWISHO WA DUNIA???!!

    Imeripotiwa kutokea wahubiri wa kidini jijini New York-Marekani kufuatia wanacho dai mwisho wa dunia ni tarehe 21/05/2011 ambayo ni siku ya Jumamosi.Wahubiri hao ambao wamekua wakifanya kazi hio bila kuchoka wametoa vielelezo mbali mbali kuthibitisha tukio hilo.Zaidi wamedai tukio hilo si lazima litokee wakati mmoja duniani kote kufuatia kutofautiana masaa lakini lazima iwe tarehe iliyo tajwa!!

    Ni matumaini yangu hayata tokea yale ya Kibwetere wa Uganda kuchoma moto waumini wake wanao sadikika  kufika 1000 ndani ya kanisa la '' Amri kumi za Mungu'' eti mwisho wa dunia umefika na kubaki yeye na bosi msaidizi wake  Bi Credonia Mwerinde nje mnamo Machi 17 mwaka 2000.Hata hivyo mpaka sasa haijulikani kama Kibwetere  na mwenzie wapo hai na polisi wa Uganda kwa kushirikiana na wale wa kimataifa (Interpol) bado wana mtafuta Kibwetere popote alipo Duniani. Pamoja na kua na maswali mia nane kidogo mie yangu macho!!

    Kwa habari zaidi soma hapa:http://uk.news.yahoo.com/preachers-prophesying-end-world-york-000338169.html

    Zaidi kuhusu Kibwetere soma hapa:http://www.culteducation.com/kibwetere.html

    18 May, 2011

    17 May, 2011

    MAMBO YA KIPANYA...

    Sasa kama hali ndio hii uhuru wa vyombo vya habari uko wapi?






    IPI NI SAHIHI?

    HII?

                                                              AU HII HAPA CHINI


                                                                               AU HII

    15 May, 2011

    BAFANA BAFANA 1 TAIFA STARS 0

    Timu ya Taifa ya Africa kusini maarufu kama Bafana Bafana au Boys Boys or Go Boys Go Boys jana Jumamosi ya tarehe 14/05/2011 imeibanjua Taifa Stars ya Tanzania 1-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.Bafana Bafana ilijipatia goli lake hilo kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake Siyabonga Sangweni (29) jezi namba 44.Hilo ndo lilikua gori pekee lililo ipa Bafana Bafana ushindi mpaka mwisho wa mchezo

    Man of the match Siyabonga Sangweni

    Habari zaidi za mechi hio bonyeza link:
    http://supersport.com/football/bafana/news/110514/Bafana_defeat_Taifa_Stars

    09 May, 2011

    DUNIA IMEKWISHA......

    YAANI NIMETAMANI KUJIFICHA BAADA YA KUONA HII KITU KUCHEKA IMESHINDIKANA NA SINA CHA KUONGEA ZAIDI HAPA SEE FOR YOURSELF....

    SOURCE:NTV

    07 May, 2011

    SHAME ON YOU SCAMMERS!!!!!!!!!

           ''Can I Give You This Trust?....NO THANK YOU!!...   Reply Immediately.(ILI UIBIWE HARAKA LOL)

    Dear Friend,
    I am ( Mr.David Chalimo )The Head of files/Recording Department in a bank Burkina Faso in African.I Hoped that you will not expose or betray this trust and confident that i am about to repose on you for the mutual benefit of our both families.I need your urgent assistance in transferring the sum of $ 15 million U.S dollars ( fifteen million U.S dollars) into your account.

    The money has been dormant for yearas in our Bank here without any body coming for it.I want to release the money to you as the nearest person to our deceased customer(the owner of the account)who died a long witah his supposed next of kin in an air crash few years ago.I don't want the money to go into our Bank treasury account as unclaimed fund. So this is the reason why i contacted you, so that we will release the money to you as the nearest person to the deceased customer.

    Please I would like you to keep this proposal as a top secret or delete it from your mail box ,if you are not interested.Upon receipt of your reply,I will send you full details on how the business will be executed and a text of application which you will fill and send to the bank for the release of the money to your account.Also note that you will have 40% of the above mentioned sum, if you agree to transact the business with me while 60% will be for me.

    I will not fail to bring to your notice that risk is free in this transaction and that you should not entertain any atom of fear as all required arrangements have been made for the transfer.Please for full trust,don't forget to reply with your contact information like-:Your Name,Age,Marital Status.,Cell Phone
    Number,Your Country,Your House Address,Your Occupation,Sex,Religion,Your ID Card Or International Passport and Your Private E-mail Address for full trust.

    Looking forward to haear from you immediately
    Mr.David Chalimo




    06 May, 2011

    JOSE MOURINHO APEWA BAN YA MECHI TANO

    Jose Mourinho (Meneja Real Mdrid)
    Meneja wa timu ya Real Madrid Jose Mourinho apewa ban ya mechi tano ikiwa ni adhabu kutoka UEFA kufuatia kushangilia kinafiki baada ya kutolewa uwanjani mchezaji wa Real Madrid 'Pepe'  na baadae Wolfgang Stark  mwamuzi katika mechi hio  kali baina ya Barcelona na Real Madrid kumpa kadi nyekundu Jose ambaye alionekana kushangilia adhabu ya mchezaji wake.

    Adhabu hio ni sambamba na faini ya Euro 50,000  kwa Jose Mourinho na 20,000 Euros kwa kilabu hicho kufuatia utovu wa nidhamu wa washangiliaji wa Real Madrid uwanjani siku hio ya mchezo ambapo Barcelona waliibuka kidedea kwa 2-0 usiku huo dhidi ya Real Madrid.Pepe mwenyewepia alipewa ban ya mechi moja na kwa upande wa boss wake (Mourinho) amesha tumikia adhabu hio kwa kuto hudhuria mechi moja na kilabu hicho kimedai kukata rufaa kwa adhabu  zilizo tolewa mapema iwezekanavyo.

    zaidi soma hapa: http://www.skysports.com/story/0,,11833_6916716,00.html

    AL-QAEDA WATHIBITISHA KUUWAWA KWA OSAMA

    Habari zilizo jiri hivi karibuni toka kundi la kigaidi la Al-Qaeda ni kwamba kiongozi wao Osama Bin Laden ni kweli ameuawa na Marekani nchini Pakistan eneo la Abbottabad.Habari hizo zimenaswa kwenye mtandao unaosadikika kutumiwa  na kundi hilo wakidai shangwe za Marekani kwa kifo cha kiongozi wao kitageuka kua huzuni hivi karibuni.Hata hivyo kundi hilo limeahidi kuwepo kwa mashambulizi mapya kwa Marekani na washirika wake kusherekea miaka kumi ya mauaji ya 9/11 Marekani.Hio ni sambamba na kuishinikiza Pakistan kuandamana kwa kitendo cha Marekani kumuua Osama.


    Katika upande mwingine Marekani imedai shambulizi la kumuua Osama limewawezesha kupata habari ambayo Osama ali rekodi siku chache baada ya kifo chake.Habari hio ilikua ni ya mashambulizi ya kulipua Reli na treni huko Marekani.


    Kwa habari zaidi soma hapa: http://uk.news.yahoo.com/bin-laden-plotted-attack-us-trains-022222947.html


           na hapa                                  : http://news.sky.com/skynews/Home/World-News/Video---Osama-Bin-Laden-Barack-Obama-At-Ground-Zero-Amid-Pakistan-Compound-Raid-Story-Doubts/Article/201105115986145?lpos=World_News_Third_Home_Page_Article_Teaser_Region__4&lid=ARTICLE_15986145_Video_-_Osama_Bin_Laden%3A_Barack_Obama_At_Ground_Zero_Amid_Pakistan_Compound_Raid_Story_Doubts

    03 May, 2011

    NANI ALAUMIWE??

    Hivi mwanafunzi kama huyu akifeli ata mlaumu nani?. kweli walimu wetu wana kazi kubwa sana kama mambo yenyewe ndio haya.Hivi kwani mtu huwezi zima simu ukiwa darasani ok, kuzima ngumu weka silent basi kwani simu kuita darasani mbali na kukupotezea muelekeo katika kipindi inaharibu utulivu na mwendelezo wa kipindi darasani.Mie naona wanafunzi wa aina  hii aidha wanyang'anywe simu kama hawaweza fata masharti au watolewe nje ya darasa waka ongee vizuri huko nje kama simu ina umuhimu kuliko kipindi.

    Maadili Mashuleni (Kazi safi ya Haki Elimu)


    Ni wazi kwamba serikali haiwezi kufanya kila kitu kudhibiti maadili ya wanafunzi ila inawezekana kwa ushirikiano wa wazazi, walimu ama walezi.Kwa wazazi kama unamnunulia mtoto wako simu ni vema umwambie matumizi ya hio simu akiwa shule, kwa walimu ni vema kuwaambia au kuweka tangazo linalo zuia matumizi ya simu muda wa masomo au darasani.Pia wazazi tuwe karibu na watoto wetu kujua hata wanaishi vipi na shule wanaendeleaje,utakuta mtoto ana simu ambayo hata baba au mama hawana (nina maana ya Gharama sana) mnunuzi hajulikani na simu hio hutumika wakati wa shule na usiku nyumbani wakati hata wazazi hio namba hawaijui.

    Kama wazazi tunajiweka mbali na watoto wetu wa shule basi hata wasipo faulu tusilalamike.Ijulikane kwamba kusoma inahitaji moyo na faraja ya wazazi ni muhimu katika masomo.Ni lazima mzazi ujue maendeleo ya mwanao angalau kwa kila muhula.Kwakuto fatilia maendeleo ya mwanafunzi ndio siku ya siku unakuta mtoto wako ni mvuta bangi tu shule inamboa haitaki tena, kafukuzwa ana mimba (kwa wasichana) au tu amekua mtoto aliyekosa maadili kwa namna zote.Zamani mtu anaweza sema hajui sasa haki elimu ndio hao wanafichua maovu mashuleni.Wazazi,Waalimu pamoja na Serikali ni lazima tuwajibike sehemu zinazo tuhusu.

    SICK TUNES ONCE AGAIN

    WARNING:Be advised that some songs in this list (hereunder) contain strong language!! i'm warning you!.

                                                          Auburn-la la la

    Iyaz- island girls
                                                                      
                                                                      Jeremiah ft 50 Cent-down on me

                                                             Chris Brown-Beautiful people
                                      
                                           YC ft Racks-future

    Wiz Khalifa-this plane

     Waka Flocka- No Hands

    NELLY-Just a dream

    N Dubz-Girls (clean version)

    Enrique Iglesias - One Day At A Time (feat. Akon) 

    02 May, 2011

    BREAKING NEWS:OSAMA BIN LADEN IS NO MORE!!


                                                    Osama  Bin Laden enzi za uhai wake.

    Kiongozi namba moja wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda (pichani juu) Osama Bin Laden ameripotiwa kuuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan baada ya mapigano makali ya kurushiana risasi kabla ya kifo chake.Habari zilizo tapakaa mitandaoni zinathibitisha kifo cha Osama ikiwa ni baada ya taarifa ya ikulu ya Marekani kuthibitisha kifo hicho kupitia hotuba ya Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye amekaririwa akisema''to those families who have lost loved ones to Al-Qaeda's terror justice has been done''

    Osama wakati akitafutwa kwa dili la dola million moja kwa atakaye mpata

    Hata hivyo Rais Obama ame tahadharisha balozi zake zote duniani kuwa makini kwa sasa kwani kuna uwezekano wa washirika wa Osama kulipiza kisasi kufuatia kifo cha kiongozi wao. Osama amekua akitafutwa na Marekani kwa muda sasa kufuatia shambulizi la Sept 11,2001 huko New York na Washington ambapo watu karibia 3000 walipoteza maisha.Huko Marekani watu leo wanasherekea kifo cha Bin Laden kwa shangwe zote.Watu mbali mbali pia wamesema Al-Qaeda sio Osama pekee (lile ni kundi kubwa sana) kwahio kazi haijaisha.

    Zaidi soma hapa:http://www.bbc.co.uk/news/world-us-canada-13256676
                               :http://latimesblogs.latimes.com/washington/2011/05/osama-bin-laden-dead-al-qaeda-islamabad-navy-seals.html
                               : http://www.guardian.co.uk/world/2011/may/02/osama-bin-laden-arab-reaction
                               :http://www.msnbc.msn.com/id/42852700/ns/world_news-south_and_central_asia/

    01 May, 2011

    GADDAFI SURVIVES NARROW ESCAPE

    Colonel Gaddafi is reported to have survived a narrow escape from NATO airstrike leaving his youngest son (Saif al-Arab Gaddafi, 29 ) and three grand sons dead.The Libyan government spokesman ( Mussa ) said Gaddafi and his wife were present during the attack and  survived unharmed.Moussa added that the attack is assumed 'a deliberate plan to assassinate Gaddafi.

    On the other hand The Libyan government spokesman Mussa Ibrahim told a news conference. "We think now it is clear to everyone that what is happening in Libya has nothing to do with the protection of civilians''.Apparently NATO has denied targeting Gaddafi, or his family and apologies for any casualities.

    The NATO's commander of Libya operations, Canadian Lieutenant-General Charles Bouchard, said the target was part of a strategy to hit command centres that threaten civilians."All NATO's targets are military in nature ... We do not target individuals," he said in a statement.

    For more click here: http://thestar.com.my/news/story.asp?file=/2011/5/1/worldupdates/2011-05-01T085440Z_01_NOOTR_RTRMDNC_0_-566815-3&sec=Worldupdates and http://www.bbc.co.uk/news/world-middle-east-13251601

    UGANDA NAKO KUMEKUCHA,VICHAPO NJE NJE

    Uganda nako shughuli ni watu na watu ndio hao wanapewa kichapo cha mbwa mwizi japo wanadai haki.Sasa sijajua huyu jamaa akija kuwa Rais siku moja atamfanya nini Museveni?! angalia video hapo chini polisi na wanajeshi walivyo mdhibiti kiongozi wa upinzani Dr Besigye. Shangingi wala halikusaidia kwani walivunja vioo vya gari lake na kumwagia maji yanayo sadikika kuwa na pili pili.Yaani combat ilikua unyama unyama!!
                                              Dr Kizza Besigye akidhibitiwa na wanajeshi


    NTV

     Siasa za Africa zinataka moyo jamani duh! Angalia Video hii hapa chini jamaa (Dr Besigye) ana moyo sana na mvumilivu, hapa anaenda zake kazini na kakamatwa kama kibaka vile tena bara barani.Nadhani hapa ndipo vurugu zilipo pamba moto baada ya huyu kiongozi wa upinzani kukamatwa.

                                                                       NTV

    WIZI HUU SIJUI UTAISHA LINI!!!!

    Hawa jamaa kweli wabunifu wa wizi yaani baada ya kututumia email nyingi kua tumeshinda mamilion ya pound  au tuwasaidie kuhamisha mamilioni yaliyo kaa hayana mwenyewe kwahio tuwape majina yetu kamili,namba za simu,anuani zetu na kadhalika ili kujipatia vijisenti bure kabisa sasa wamekuja na hii:-

    To apply for the Nigeria Social Insurance Trust Fund (NSITF) Recruitment 2011, Nigeria Navy, Standard Chartered Bank, International Breweries open for experienced and graduates trainees
    visit: www.nigeriaonlinejobsapplication.co.cc TO APPLY


    MTAKAO IBIWA HUKU MNAJUA HUU WIZI MITANDAONI SI VIBAYA MKATOA USHUHUDA ILI WATU WENGINE WAJUE KUNA WIZI WA NAMNA HII.MTAKAO TUMIWA UJUMBE KAMA HUO JUU PIA SI VIBAYA TUKAWASIKI, MIE NDIO NISHATUMIWA HIVO NA TITLE 'LATEST NIGERIA VACANCIES' SIO HUU TU KUNA WIZI MWINGINE KAMA WA KUJIFANYA WANANUNUA PAKA WA RANGI FULANI , HELA (COIN/NOTI ZA ZAMANI) HUO NI BAADHI YA UBUNIFU WA HAWA JAMAA AMBAO SASA WAPO DUNIA NZIMA WAKISAKA NOTI KWA NAMNA HALALI NA ISIYO KWAO NI MPAKA KIELEWEKE!!

    TOKA ZE COMEDY ORIGINO MPAKA KUHUBIRI NENO LA MUNGU!!!

    Video  ya kwanza hapa chini inaonyesha 'Masanja Mkandamizaji' anakandamiza nini mimi sijui!! au jina halisi Emmanuel Mgaya akihubiri neno na kudai yeye kaokoka na wajanja wote wameokoka (ni kweli wajanja wote wameokoka mie sijui, wajanja ni akina nani pia sijui!,yule aliyekua pembeni yake wakati akihubiri pia simjui).Ila niseme tu ni mwanzo mzuri kwa wasanii kuokoka kwani wana nafasi ya juu kabisa ya kurubuniwa na shetani kutokana na kujulikana kwao kwa jamii hii itawasaidia kama kweli wana maanisha KUOKOKA ISIWE MWAVULI WA KUFICHIA MAOVU na NI LAZIMA WAO KAMA KIOO CHA JAMII WAWE MIFANO YA KWELI NA SI VINGINEVYO !!. (ni mtazamo tu)

    Baada ya kusema hayo ningependa jamii yetu ya Kitanzania kujua maana halisi ya 'KUOKOKA'.kwa kusoma na kuelewa maandiko sio tu kuamini kila tunacho ambiwa ndio ipo siku tuje kuchomana moto eti mwisho wa dunia eti Mungu kasema!! Mfano Kibwetere wa Uganda alichoma moto kanisa ndani kukiwa na waumini!! kwakua watu waliamini kila alichosema hata waka kubali kuchomwa moto.Tusiwe wavivu wakusoma vitabu vya maandiko matakatifu.

    .Mimi inapofika hatua ya kuongelea imani zetu huwa sina ubishi kwakua naamini kila mtu ana imani yake na Imani ya mtu ndio inatakayo muokoa.Kama mtu hana imani ni kazi bure kusema ameokoka,vivyo hivyo kama mtu una sali kanisa fulani ambalo unadhani ukiwa huko ndio umeokoka  bila ya Imani hapo mtu unakua unapoteza muda wake bure.Au mtu kutumia kanisa fulani kama mwavuli wa kuficha maovu wakati ukweli ni kwamba umeoza!! Utakuja kuwa kuni za kuchomea wenzio huko eternal hell (kuzimu)



    Nijuavyo mimi kama nilielewa vizuri mafundisho ya dini...Imani ya mtu huanza na kuamini  uwepo wa Mungu na kukili imani yako kwa kinywa chako.Ni lazima uamini Mungu katika NENO LAKE (maandiko matakatifu) pia umtumikie ndipo udai wokovu wake kwa imani uliyokua nayo. ...na hapo ndipo nguvu ya Mungu itakuokoa, itakulinda, na kukuwezesha kuishi maisha mema katika yeye muweza wa yote.Ni lazima tutambue imani ya mtu haichezewi na ni vema na haki kuiheshimu.KUOKOKA KUNA MAANA KUBWA ZAIDI YA KUONGEA.....HATA HIVYO SINA MAANA WANAO SEMA WAMEOKOKA WANA TUDANGANYA ILA KAMA WANAONGEA WAKATI MOYONI WANAJUA SIO BASI WANAJIDANGANYA WENYEWE.WALIO OKOKA KWELI MUNGU AWAJALIE.

    The Bible says: 'Our hearts are deceitful, we should not trust in our hearts (Jeremiah 17:9)
                              'There are false christs,false gospels,and false spirits ( I Corinthians 11:4)
                              
    So how can you be sure that you've heard of the true Gospel,received true christ and the true Holy Spirit??! Comrades we must be certain that our faith is THE TRUE FAITH IF AND ONLY IF BASED ON SCRIPTURE AND NOT THEM FALSE ONES BASED ON FEELINGS!!!

    Angalia hizi Video hapa chini zinafundisha zaidi maana ya kuokoka



    29 April, 2011

    LEO MAMBO YOTE ROYAL,KAZI TUTAFANYA AKISHAOA!!

                                                                          Kate & William

    Ni ile siku iliyokua ikisubiriwa kwa hamu ambayo mjukuu wa Malikia Elizabeth wa pili Prince William anamuoa mchumba wake wa siku nyingi Kate Middleton.Ni siku ya kihistoria zaidi ambapo maandalizi ya harusi hii ya  familia ya malikia yamechukua muda mrefu kutokana na uzito wa tukio lenyewe.Katika kuwahi kujionea tukio live (sikwamba hawana Tv nyumbani) waingereza wengi wamekesha katika Tents nje ya jengo ambapo wawili hao wataoana mapema leo.

    Katika tukio hilo ambalo litakua katika ulinzi mkali watu zaidi ya million moja wanatarajia kuhudhuria katika eneo hilo na watu Billion mbili wataona/sikia tukio hilo kupitia vyombo mbalimbali ikiwemo Live Tv,Internet,Radio etc.Habari zaidi zinasema wengine wata jiachia kwa party za mitaani katika kusherekea siku hii ya mapumziko wakati prince William anaoa  jijini London mapema leo. SI VIBAYA KWA WENYE MA HOTELI TANZANIA NA MAHALI PENGINE KUZINGATIA UMUHIMU WA SIKU  HII  KWA KUWABURUDISHA WATEJA WAO (WAINGEREZA) AMBAO KWA TANZANIA WAKO WENGI TU ILI WASIJIONE WAKO MBALI WAKATI WENZAO HUKU (UK)  WALA BATA SIKU NZIMA!

                                   Mke na Mme watarajiwa Kate & William                                               

    Wageni rasmi katika harusi hii ni 2000 na katika hali isiyo ya kawaida, pamoja na ukaribu uliopo kati ya UK na USA Rais Obama haja alikwa!! Kwa maana hio naye ataona kwenye Tv kama mimi (kama atakua na muda) hii kali  lol.

    Kupata Ratiba ya Royal Wedding ingia hapa: http://www.theroyalweddingwilliamkate.com/the-wedding-day-schedule

    Kuangalia ROYAL WEDDING LIVE ingia hapa: http://www.royalweddinglive.tv/kate-and-william-wedding-day/

    ZAIDI YA WATU 280 WAFARIKI DUNIA KWA KIMBUNGA ALABAMA-MAREKANI

    Watu takribani 280 wafariki dunia kwa kimbunga kikali kwa kimatumbi (Tornadoes) nchini Marekani.Kimbunga hicho kilichotokea kusini mwa Marekani (ALABAMA STATE) kimefanya uharibifu mkubwa wa maisha ya watu pamoja na mali zao.Mbali na kuua watu kimbunga hicho kimeharibu miundombinu kama umeme,nyumba,barabara na mingine mingi na kufanya watu wapoteane katika tafrani hio.

      RAMANI YA MAREKANI NA STATES ZAKE (ALABAMA NDIO SEHEMU YA MAAFA KATIKA RAMANI HII KUSINI KARIBU NA GULF OF MEXICO)

    Tornado ni janga la asili kama ilivyo tetemeko la Dunia na hutokea pale upepo nyevu wa vugu vugu unapogongana na upepo mkavu wa baridi ambapo wimbi kali la upepo mkali na wenye nguvu hutengenezwa na kusafiri kwa mwendo wa takribani maili 100 kwa saa.Tornado ni janga ambalo hutokea mara kwa mara karibu na GHUBA YA MEXICO  kila Spring (wakati kama huu) na Summer kutokana na mgongano huo wa upepo nyevu na wa moto unaovuma toka  kusini (Ghuba ya Mexico) na kugongana na upepo baridi toka kaskazini mwa nchi ujulikanao kama 'Colder Dry Canadian Winds'.Huku kuna Watanzania wengi tu tuwaombee salama katika maafa hayo na wenye jamaa/ndugu  huko ni vema wakawasiliana kujua hali zao.

    SIJUI SASA WATASEMA AMECHAKACHUA CHETI???!!

    Born August 4, 1961 Honolulu, Hawaii,USA 

    Barack Obama (Rais wa Marekani)


    Baada ya utata kuhusu uraia wa Rais wa Marekani Barack Hussein Obama II,Whitehouse yaachia cheti cha kuzaliwa cha Rais huyo kuvunja utata uliovuma kwa muda mrefu sasa, Cheti kinaonyesha uraia wake kama Mmarekani na sio 'MKENYA' ukitaka kuona cheti bofya link hapa chini
    http://www.whitehouse.gov/sites/default/files/rss_viewer/birth-certificate-long-form.pdf

    28 April, 2011

    MALAWI WAMWAGA UGALI,UINGEREZA WAMWAGA MBOGA!!!

    Ni katika sakata la uongozi unaodaiwa kuwa ni mbovu nchini Malawi ambapo aliye kua boss wa Malawi enzi za ukoloni ikiitwa Nyasaland (Uingereza/UK) ambaye pia ndio mtoa misaada mkuu nchini humo amesiitisha misaada hio tangu mwaka jana kwa kiasi cha Pauni Million 3 kutokana na matumizi mabovu ya serikali ya Malawi.Kwa mujibu wa gazeti la 'The Telegraph' matumizi mabovu ni pamoja na ununuzi wa ndege ya Rais Bingu Wa Mutharika kwa kiasi cha pauni million 8 kwa nchi masikini kama Malawi.

    Katika sakata hilo Balozi wa Uingereza nchini Malawi  Mr Fergus Cochrane-Dyet ameamriwa kuondoka nchini humo kwa kosa la kuikosoa Serikali ya Malawi kwa matumizi mabovu na kunyima uhuru wa wananchi kuongea ama kuikosoa serikali kama ilivyo ripotiwa na wana harakati wa haki za binadamu.Kufuatia uamuzi huo wa Malawi, Uingereza nao wamemtaka kaimu balozi wa Malawi nchini Uingereza kuondoka mara moja. Amri hiyo imetolewa jana na  katibu wa Uingereza mambo ya nje William Hague

    20 April, 2011

    THE DIASPORA 3 CONFERENCE IN LONDON TO BE HELD ON, 6th - 7th MAY 2011.

    The Tanzania High Commission in London in collaboration with the Tanzania Association in the UK (TA-UK) are organizing a Tanzania Diaspora Conference (Diaspora 3 London) to take place from Friday, the 6th to Saturday, the 7th May 2011 at Sattavis Patidar Center, Forty Avenue J/W The Avenue, Wembley Park, Middlesex HA9 9PE(London, United Kingdom).

    Conference Agenda:
    The two-day event is a continuation of the Mission’s efforts to engage the Tanzanian Diaspora in its area of accreditation, including the United Kingdom and the Republic of Ireland. The conference agenda will include matters arising from the past two conferences held in London in 2008 and 2010.

    As it was the case with the previous conferences the Tanzanian private sector has been invited to participate. These include banks, NHC and estate agents, employment agencies and strategic companies that will be targeting to employ people from the Diaspora. Tanzanian companies as well as Tanzanian NGOs and groups operating in the UK are encouraged to participate.

    Objectives:
     Diaspora 3- London is necessary for the following reasons:

    •To carry forward the Government’s commitment to actively engage the diaspora to the development of their country.
    •To acknowledge the growing need of the qualified diaspora to relocate back to Tanzania following available opportunities.
    •To encourage professional Tanzanians in the Diaspora such as Medical Doctors, Computer engineers, Accountants, to participate in the social economic development activities back in Tanzania.
    •To acknowledge the value and importance of the Diaspora and consider the best way for the Government to engage them.
    •To review progress made since the establishment of the Diaspora Department at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation.
    •And finally to deepen the link between the Diaspora, their Government and their home country.

    Theme
    The theme for this year’s conference is ‘A Participatory Diaspora, a Stronger Tanzania.’ Apart from advocating for the continued efforts of the Government to engage the Diaspora, the theme acknowledges the value and importance of Tanzanian Diaspora in development of our country.

    Note:
    Sattavis Patidar Centre is located just off the North Circular Road and the car park on ‘The Avenue’ Corner of Forty Avenue will be available for the conference attendants. Those wishing to come by bus can take buses number: 245, 223, 83, 182, 297 and PR2. By tube they can use Metropolitan Line or Jubilee Line to Wembley Park.

    To register for the event click the following link: https://events.r20.constantcontact.com/register/eventReg?oeidk=a07e3o7xqgo021edbc3&oseq=

    14 April, 2011

    GBAGBO KWISHNEY, OUATTARA APETA..

    Wanasema mjumbe hauwawi  KUMBE CHA MTEMA KUNI ANAPATA?  hivi ndivyo ilivyokua kwa mshauri wa Gbagbo ( aliyekua Rais wa Ivory Coast).Hii ilitokea sambamba na kukamatwa kwa Gbagbo ambaye alishindwa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka jana (2010) na kung'ang'ania kubaki madarakani kinyume na sheria.Gbagbo ambaye alishindwa kwenye uchaguzi  baina ya Alassane Ouattara  na hatimaye kuamua kuendelea kua Rais na nchi yake kua katika machafuko mpaka alipo tolewa kinguvu mnamo Tar 11/04/2011 kwa msaada wa jeshi la umoja wa mataifa.


                                         Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara kuanzia tar 11/04/2011

    Gbagbo ambaye kwasasa amekamatwa na kupelekwa kusiko julikana kwa usalama wake, mpinzani wake Alassane ameahidi kumlindia heshima japo wakati wa kukamatwa ni kama vile alikua kibaka.Ouattara ndio rais wa Ivory Coast ambae ameanza kuitumikia ofisi kihalali tar 11/04/2011


    Mwananchi mwenye hasira akimshambulia mshauri wa  serikali ya Gbagbo huko Ivory Coast mara baada ya kukamatwa hoteli ambayo walikaa wakati wa machafuko nchini humo.( kama mambo yenyewe ndio haya sasa ndio nime elewa  maana ya yale mashangingi kutembea kama yameibiwa!!)


    Aliyekua Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo

     Zaidi soma hapa http://www.metro.co.uk/news/860721-new-era-for-ivory-coast-as-leader-laurent-gbagbo-spirited-away

    11 April, 2011

    FULL FACE VEIL BANNED IN FRANCE.

                                     A woman with full-face veil (photo from upi.com)

    France has banned Muslim women from wearing full  face veil.Today the law is put in effect and several emerges have been released depicting the type of veils that are not allowed.Generally the ban seems to be applicable (if the veil is worn)  mainly in public because according to the police guidelines in the implementetion of the law,victims will not be forced to remove veils and that the ban does not apply (if worn) inside private cars.

    So far, those  violating the law will be fined up to  £132 (150 euros). Early reports shows police have already arrested 59 women in the exercise of enforcing the law.On the other hand Muslim leaders have said they support neither the veil nor the law banning it. (????!!!)

    For more info read:  http://uk.news.yahoo.com/5/20110411/twl-french-ban-muslim-women-from-wearing-3fd0ae9.html

    MWAKA WA VIKOMBE KATIKA PICHA

          Hii ndio foleni siku za mwanzoni kuelekea kwa Babu-Loliondo

           Foleni kwa mbali ilikua kama hivi kuelekea Loliondo kwa Babu


    4x4 ndio ulikua mpango mzima kuelekea kwa babu ukizingatia barabara zetu ni mbaya zaidi hasa mvua ikinyesha.

    Huyu ndiye Babu Mwaisapile akiwa kazini na hatimaye kuiteka Bongo sasa hivi uki google Loliondo wonders utapata habari nyingi za huyu Babu kwenye vyombo vya habari ndani na nje ya Tanzania.

    Babu anazidi kugawa 'dose'


    Mheshimiwa na mpiganaji tegemeo naye alikuwepo...


    Waheshimiwa pia walikuwepo...

    Serikali haikua na namna bali kuunga mkono jitahada za babu pamoja na kuahidi kuwepo kwa 'research kuhusu dawa ya babu ambayo mpaka sasa HATUNA MAJIBU KAMILI ni matumaini baada ya utafiti huo kukamilika tutapata kueleweshwa..


    Babu alipata mpinzani toka Mbeya na Kikombe cha Mbeya ndio hiki maandalizi yanaendelea


    Huyu ndio Dogo wa Mbeya (17yrs) Kikombe chake kilikua bure
    Kwa dogo Mbeya hali ilikua kama hivi..


    Huyu mtoto sijui hata anajua hio ni dawa usikute anadhani CHAI!! kazi kweli kweli!


    Kikombe cha kwa dada Tabora ni maombi kwanza kabla hujakipata Kikombe!! 'Yaani sala na kazi'

    Kwa dada Tabora watu kibao kama kawa
    Kikombe cha Moro kikiwa kina andaliwa..


    Baadae Kikombe cha Moro mambo yakawa hivi.. na bei ni 200/=


    Safari hii Kikombe ni Njombe kwa Dr Mwandulami (58) ni bure 'until further notice'
    Wananchi wakipata Kikombe cha Dr Mwandulami Njombe Mkoani Iringa.


    Sasa hapa tumwamini nani katika hivi vikombe?? Na je ni lini serikali itatuambia ukweli kuhusu hivi vikombe? Je ikigundulika vikombe ni 'fake' nani wa kulaumiwa/kuwajibishwa?.Kusema kweli huu mwaka ni waajabu na mwamko kama mlivyoona ni mkubwa watu wana amini vikombe sana.Tujiulize ni kwanini??  je ni kutokana na matatizo yetu kiafya au wewe unaonaje?.Wizara ya afya ituambie baada ya utafiti kukamilika ili wananchi wajue kama kweli tiba ipo au ndio propaganda tu.

    06 April, 2011

    SIKILIZA HII WAKATI TUNA TAFAKARI MWAKA WA VIKOMBE!!!

    Sasa  dozi ni VIKOMBE VITATU  huko Njombe,Tafakari ya mwaka na haijawahia tokea Tanzania.Basi wakati tunatafakari VIKOMBE ambavyo mimi nafikiri ni Imani zaidi ndio huponya basi tusisahau na Burudani (wanasema raha jipe mwenyewe) lakini mara nyingine raha unapewa.Hii nyimbo ya Banana nimeipenda sana kama vipi isikilize ukiwa katika tafakari ya VIKOMBE LOLIONDO kwa Babu (500) ,MBEYA  kwa dogo (Bure) ,TABORA kwa mama (500) ,MOROGORO  kwa dada (200 /= hii nadhani ni sale itaisha.......!!!) NA SASA NI NJOMBE  Dr Mwandulami vikombe 3 bure ikthibitika inaponya utalipa.............???!!!.Big money!!!



    03 April, 2011

    HOW TO LOSE POLITICAL LEGITIMACY

    Picha sijui yanani kama yako niambie nikuandike
    You would wonder why today i'm talking about politics and certainly some of you might think I'm into politics! To be clear I don't do politics in real life though my career started with the same field (Science of Politics) which is technically not the politics we live (My view). So much so, my interest in this post is mainly to highlight some issues that (in my view and other people's views if any) any Government  MUST (if necessary) avoid Or face the consequences like CANADA,TUNISIA,EGYPT,LIBYA,YEMEN,SYRIA to mention a few. where political illegitimacy has (in one way or the other) appeared to the World.

    Hereunder (in a point form) are the few things that undermine political legitimacy of any Goverment:
    1.Giving unfulfilled promises to citizens every now and then.
    2.Assuming Citizens don't know of any embezzlement (If any) by Government leaders/officials.
    3.Being corrupt
    4.Unequal distribution of National wealth in a particular State or Nation.
    5.Cutting benefits that affect Citizens i.e Health Service,Housing,Education etc
    6.Using public office as a family business enterprise where the  whole favour goes to the Family & Family friends.
    7.Do not listen to citizens of any concern assuming the complaints are not basic
    8.Making the constitution that favour the rulling system for example lifetime president (including those serving for a long time as if they are the only best leaders to cling on power  as per their wish)
    9.Rampant unemployment
    10.Poor social services i.e Health,Education etc.

    02 April, 2011

    MUST READ THIS...

    RECALL NOTICE:


    The Maker of all human beings (GOD) is recalling all units manufactured, regardless of make or year, due to a serious defect in the primary and central component of the heart.


    This is due to a malfunction in the original prototype units code named Adam and Eve, resulting in the reproduction of the same defect in all subsequent units. This defect has been technically termed "Sub-sequential Internal Non-Morality," or more commonly known as S.I.N., as it is primarily expressed.

    Some of the symptoms include:
    1. Loss of direction
    2. Foul vocal emissions
    3. Amnesia of origin
    4. Lack of peace and joy
    5. Selfish or violent behavior
    6. Depression or confusion in the mental component
    7. Fearfulness
    8. Idolatry? (   )
    9. Rebellion


    The Manufacturer, who is neither liable nor at fault for this defect, is providing factory-authorized repair and service free of charge to correct this defect.


    The Repair Technician, JESUS, has most generously offered to bear the entire burden of the staggering cost of these repairs. There is no additional fee required.


    The number to call for repair in all areas is: P-R-A-Y-E-R.
    Once connected, please upload your burden of SIN through the REPENTANCE procedure. Next, download ATONEMENT from the Repair Technician, Jesus, into the heart component.


    No matter how big or small the SIN defect is, Jesus will replace it with:
    1. Love
    2. Joy
    3. Peace
    4. Patience
    5. Kindness
    6. Goodness
    7. Faithfulness
    8. Gentleness
    9. Self control

    Please see the operating manual, the B.I.B.L.E. (Basic Instructions Before Leaving Earth) for further details on the use of these fixes.


    WARNING: Continuing to operate the human being unit without correction voids any manufacturer warranties, exposing the unit to dangers and problems too numerous to list and will result in the human unit being permanently impounded. For free emergency service, call on Jesus.


    DANGER: The human being units not responding to this recall action will have to be scrapped in the furnace. The SIN defect will not be permitted to enter Heaven so as to prevent contamination of that facility. Thank you for your attention!

    Thanks to http://lukwangule.blogspot.com/