20 May, 2011

DOLLAR MILLION 6 ZAMUOKOA

Hatimaye aliyekua Mkurugenzi wa IMF  Dominique Strauss-khan akubaliwa kutoka rumande kwa dhamana ya Dollar Million 6 ( $6m) na masharti makali ikiwemo kua chini ya ulinzi kutoka kampuni binafsi kwa gharama ya Dollar laki mbili kwa mwezi ambazo ni juu yake,kuwekwa chombo cha kisasa mguuni kitakacho onyesha alipo kwa saa 24 kila siku,kufungwa kwa video camera katika nyumba atakayo kaa na alarms kumzuia asitoke.

Mheshimiwa huyo ambaye mpaka sasa amejihudhuru wadhifa wake kama Mkurugenzi wa IMF kwa takribani miaka minne kutokana na kashfa ya kutaka kubaka mhudumu wa hotel huko Marekani,ataachiwa na kwenda kuishi kwa muda katika nyumba ya muda ambako mkewe Heiress, Anne Sinclair, mwanahabari na  Millionea wa kifaransa amempangishia wakati akisubiri kesi yake kusikilizwa hivi karibuni.
Zaidi soma hapa kwa kiingereza: http://www.dailymail.co.uk/news/article-1388834/Wife-daughter-disgraced-IMF-boss-arrive-court-appeal-bail-hearing.html#ixzz1MrCCmdJV

IKO WAPI HII??!