20 October, 2011

CHANGAMOTO YA LEO

KUTOKANA NA MATATIZO YA FOLENI ZA HAPA NA PALE JIJINI DAR ES SALAAM PIKIPIKI (MAARUFU KAMA BODA BODA) IMEKUA KAMA MKOMBOZI JAPO KUNA TATIZO.HIVI HAWA WAENDESHAJI PIKIPIKI LESENI WANAPATA ZA HALALI? KAMA NI HALALI KWANINI AJALI NI NYINGI? NADHANI KUNA HAJA YA WATU WANAOFANYA BIASHARA HII KUA NA MAFUNZO MAALUMU YA LAZIMA KULINDA MAISHA YAO PAMOJA NA ABIRIA AMBAO WANAWABEBA.ALIYETENGENEZA HII PICHA HAJAKOSEA NI KWELI SASAHIVI KUA/KUPANDA PIKI PIKI NI SAWA NA KUTAFUTA  ULEMAVU TENA WA KIZEMBE KABISA.WAJIBU WA SERIKALI HAPA NI KUTOA LESENI HALALI NA KUZIKAGUA MARA KWA MARA, PIA MTUMIAJI WA CHOMBO KAMA HIKI THAMINI MAISHA YAKO KWANINI UENDESHWE NA  MTU ALIYELEWA,HANA UZOEFU AU ANAPITA SEHEMU YA HATARI NAWEWE UNAMUANGALIA TU? SERIKALI HAIWEZI FANYA KILA KITU KUA MWANGALIFU!!

(KAMA PICHA YAKO TUWASILIANE SIKUMBUKI NIMEITOA WAPI NINGEKUSHUKURU)

TATIZO LA AJIRA LIPO KILA SEHEMU

                            Watu 500 wapanga mstari kuomba kazi (nafasi 20 tu) UK

Kufuatia kuanguka kwa uchumi kuanzia mwaka 2008/2009 ambako kumeathiri mzunguko wa fedha nchi mbalimbali duniani ambapo kila serikali iliweza jitahidi kunusuru uchumi wake kwa namna yake.Hapa Uingereza Gordon Brown alilazimika kuuza nusu ya dhahabu ya nchi kunusuru uchumi ulio yumba.(soma hapa).USA nao wali inusuru nchi kwa $700 Billion (soma hapa).Anguko hilo la uchumi lilipelekea makampuni mengi kufungwa na kupoteza ajira za watu wengi sehemu mbalimbali duniani.Hapa UK watu zaidi ya 2 million hawana ajira hivi sasa na serikali ndio inawagaramia kwa job seekrs allowance (kwa wazawa na wenye sheria ya kuishi nchi hii)


Sijashangaa kuona msururu ulijitokeza Chuo kikuu Dodoma kwa nafasi 12 za ajira.Ila nimeshangazwa na utaratibu wa kuita watu zaidi  ya 2000 kwa nafasi 12 za ajira.
    Ati msururu wote huu waitwa kwa usaili wa nafasi 12 za kazi!!! hivi inaingia akilini??
   (picha kwa hisani ya Bongo Pix Blog)

Hii ni kuchezea akili za watu huwezi ita (shortlist) watu 2000 kwa nafasi 12.Hawa watu wanasafiri toka sehemu mbalimbali sio ustarabu kuita watu wote hao kwa nafasi hizo chache (soma hapa na hapa).Hii ni sawa na shule/chuo kinachochukua wanafunzi 100 kutoa fomu laki moja za kuomba nafasi tena kwa kulipisha watu pesa huu ni wizi wa hali ya juu sana.Ufisadi sio lazima mtu ale rushwa hata huu ni ufisadi.

14 October, 2011

LEO NI SIKU NA MWEZI AMBAO BABA WATAIFA ALIIAGA DUNIA


Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 – 14 October 1999)

LEO TAREHE 14 MWEZI WA 10 NI SIKU NA TAREHE AMBAYO TUNA ADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.SIKU HII NI SIKU MUHIMU KITAIFA NA PENGINE KIMATAIFA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA.KATIKA KUMBUKUMBU HII NI VEMA SERIKALI NA WATANZANIA KWA UJUMLA KUKUMBUKA MAMBO MUHIMU AMBAYO MWALIMU ALIKEMEA KW ANGUVU ZAKE ZOTE.MFANO WA MAMBO HAYO NI RUSHWA (CORRUPTION) MAARUFU KAMA KITU KIDOGO.

RUSHWA IMEKUA KAMA  MCHEZO AMBAO UMEZAGAA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA.SASA HIVI HATA UKITAKA HUDUMA YA AFYA YA HARAKA NI LAZIMA UTOE KITU KIDOGO.HUDUMA YA BURE BILA KITU KIDOGO HUWEZI PATA KWA MUDA UNAOTAKIWA.MCHEZO HUU MCHAFU UMEKUA KWA KIASI KIKUBWA KIASI KWAMBA KUNA WATANZANIA WANA AMINI BILA RUSHWA HUWEZI FANYA LOLOTE.

MADHARA YA RUSHWA NI PAMOJA NA KUTO KUWAJIBIKA KWA VIONGOZI WETU,UONGOZI USIO WA SHERIA,MAADILI WALA HAKI,AJALI,VIFO,MAENDELEO DUNI,HUDUMA MBOVU KWA JAMII MFANO HUDUMA ZA AFYA,ELIMU,BARABARA  N.K.ITAMBULIKE WAZI KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU KUA RUSHWA BADO NI ADUI MKUBWA ALIYEKOMAA NA KUIDIDIMIZA TANZANIA KATIKA NYANJA ZA KIUCHUMI,KIJAMII,KISIASA NA KIUTAMADUNI.TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) IWE CHOMBO HURU NA CHENYE NGUVU KUWAJIBISHA WATUHUMIWA WA RUSHWA WANAPO BAINIKA BILA KUJALI NANI,CHEO,DINI WALA KABILA.ITAKUA HAINA MAANA KILA SIKU TUWE TUNASIKIA TAKUKURU WAMKAMATA  KAMANDA FEKI HUKO SIJUI WAPI!


MANENO HAYA YA MWALIMU YAPO AU HAYAPO? KAMA YAPO MBONA HATUONI WALIO KULA FIMBO 12 NA KUWAONYESHA WAKE ZAO WAKIWA WANATOKA JELA?.RUSHWA NI ADUI MKUBWA WA HAKI!


SOMA ZAIDI HAPA KUHUSU HISTORIA YA MWAL.NYERERE

Umar Farouk Abdulmutallab to face life sentence!!

                                                              Umar
 Umar Farouk Abdulmutallab pleaded guilty to trying to blow up a transatlantic flight on Christmas Day 2009.Having pleaded guilty at his trial in Detroit, he is set to face life in prison when he is sentenced on 12 January 2012.Umar is a Nigerian born man aged 24 year old,privileged,very religious and teacher's dream.According to Michael Rimmer, a Briton who taught him history, told the BBC Umar Farouk Abdulmutallab had been "every teacher's dream - very keen, enthusiastic, very bright, very polite".[BBC]


Abdulmutallab's father, Alhaji Umaru Mutallab, said he had approached the US and Nigerian authorities to warn them about his son's views in November - weeks before the attempt to destroy the flight to Detroit with at least 300 passengers on board.


FIKIRIA HUYU NI MTOTO WAKO!!..HIVI KAMA MZAZI UNAPOONA MTOTO ANAENDA KUSIKO UNAKAA KUMUANGALIA AU UNACHUKUA HATUA? JE MZAZI WA UMAR ANAJISIKIAJE KUMKOSA MTOTO WAKE KWA MAISHA YAKE YOTE? JE ANGEMUONYA AMA KUMLAZIMISHA KUBADILI MISIMAMO YAKE SI ANGELISAIDIA KUOKOA MTOTO WAKE? KIJANA MDOGO KAMA HUYU SASA ATATUMIKIA KIFUNGO CHA MAISHA KWA FAIDA YA NANI? JE KUNA WAZAZI WANGAPI WA NAMNA HII? MTAZAMO WANGU MZAZI WA UMAR AMESHINDWA KUWAJIBIKA KIASI FULANI KAMA AKWELI ALIONA MTOTO WAKE ANAPOTEA ANGEFANYA KITU KUMUOKOA. JE UNGEKUWA WEWE MZAZI WA UMAR UNGEFANYAJE UNAPOONA MTOTO WAKO ANAPOTEA? KUTOA TAARIFA VYOMBO VYA DOLA BILA KUFANYA JITIHADA ZAKO KAMA MZAZI HAITOSHI NA HAIKUSTAHILI MTAZAMO WANGU. JE WEWE UNASEMAJE?


ZAIDI SOMA HAPA NA HAPA

MONEY vs HUMANITY


Nionavyo mimi pesa na utu wa mtu ni vitu viwili muhimu katika maisha ya kila siku, bahati mbaya siku zinavyo zidi kwenda uwepo wa pesa umekua na maana zaidi kuliko utu wa mtu.Kwanini? Mtu anaweza muondoa uhai mwenzie kisa anataka kupata pesa..Mtu yupo tayari kutafuta pesa hata kwa gharama ya maisha ya mtu mwingine.Sasa hivi imekua kawaida mtu ukisema kitu kama huna pesa basi husikilizwi kama umeongea cha maana.Aidha ukiwa na pesa unaweza fanya chochote kihalali au kinyume chake bila wasiwasi kwani pesa itakulinda.Hii ni sifa kubwa katika nchi zinazo endelea japo hata zilizo endelea kuna nafasi ya pesa lakini utu wa mtu una maana zaidi na hivyo pesa haiwezi kukulinda unapo hatarisha utu wa mtu kwa kutumia pesa zako.Je nchi yetu Tanzania inaona hili?


Ukitaka kuona kama pesa inamaana zaidi angalia picha hapo juu, sasahivi kuna maelfu ya watu Somalia na nchi jirani wakiwa na janga la njaa, maisha ya watu wengi yapo hatarini na muamko wa watu kutangaza janga hilo ni mdogo sana kulinganisha alipo kufa mwanzilishi wa kampuni ya Apple ambapo kila mtu ameonyesha kuguswa naye kwa namna moja ama nyingine.Je ni kwasababu alikua na pesa?, alitoa ajira nyingi? katoa bidhaa inayopendwa? mbunifu wa kihistoria katika maendeleo ya teknolijia?.jibu linaweza kua ni ndio lakini kwanini watu hawaguswi na hawa watu wanaokufa kila siku kwa kukosa chakula? ajali za kizembe kama zile za kuzidisha mizigo kwenye vyombo vya usafiri kwa manufaa ya watu fulani?.Je ni lini utu wa mtu utathaminika?

Things are back to normal on BlackBerry

This  made a headline  on various media after many of its users in Europe, the Middle East and Africa lost services on Monday.The BB users suffered problems with email, BBM and internet that were reported by customers later that day.Canadian firm Research in Motion (RIM) has apologised for the inconvenience and says that all services have now been restored.
Apparently there's no official word yet from RIM on what caused the problem but it's reported to be linked to a crashed server at a BlackBerry data centre.This  indeed will be another huge blow to the company and its reputation apart from the weaker sales in the face of strong competition from Android handsets and Apple's iPhone.

12 October, 2011

BLACKBERRY BLACKOUT ENTERS 3RD DAYA global BlackBerry outage has entered its third day with users more fed up than ever with the disruption to their e-mails, instant messaging and Internet.

The BlackBerry outage, which began at 11am BST on Monday, left 10 million smartphone owners across Europe, the Middle East and South America with limited access to data services.

In an update from the BlackBerry maker last night, Canadian company Research in Motion(RIM) explained the glitch. “The messaging and browsing delays being experienced by BlackBerry users in Europe, the Middle East, Africa, India, Brazil, Chile and Argentina were caused by a core switch failure within RIM’s infrastructure.

TUKO WAWILI PEKEE YETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Ni kweli Mungu anasamehe lakini unapomueleza binadamu mwenzio ubaya huu
unategemea nini................????????????
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.
"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana "
"endelea"
... "bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?
"utasamehewa"
"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"
"utasamehewa"
"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo ?"
- kimya........
"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo ?"
- kimya.........
Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.
"sasa baba mbona umenikimbia?"
padri kwa taabu akajibu "nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili tu peke yetu........"

                 ''AISEE ULIYE ANDIKA HII HONGERA KWA UBUNIFU''

09 October, 2011

NYERERE DAY 2011 IN WASHINGTON DC

Maadhimisho ya nne ya kuenzi maisha na kazi za Mwl Julius K. Nyerere yatafanyika Oktoba 15, 2011 hapa Washington DCMmoja wa waasisi wa Julius Nyerere Comemoration Bwn Rick Tingling akielezea maandalizi ya siku hiyo katika video hapa chini


      **NYOTE MNAKARIBISHWA**

Itafanyika

Howard University Basement Auditorium
725, 2225 Georgia Ave, NW, Washington, DC 20059
FROM 3PM-6PM

MAELEKEZO KUELEKEA Howard University Hospital Basement Auditorium:

  1. Ingilia mlango wa mbele wa Hospitali unaotazamana na Georgia Avenue.
  2. Pita kwenye dawati la maelezo kwa utambulisho
  3. Endelea mbele mpaka kwenye "lift" zilizo kama yadi 50 toka dawati la mapokezi.
  4. Chukua "lift" / elevator kuelekea sakafu ya chini (basement).
  5. Elekea upande wa kulia ukifuata alama zinazoelekeza ulipo ukumbi.
AMBATANISHO: MAELEZO KUHUSU MAADHIMISHO HAYO.
NOTE: Mabadiliko pekee niliyojulishwa ni kuwa Balozi Mwanaidi Maajar hataweza kuhudhuria kwa kuwa atakuwa nje ya mji.

    BARAKA KWAKO NA ASANTE KWA USHIRIKIANO


07 October, 2011

HAPPY 61ST BIRTHDAY H.E.DR JAKAYA KIKWETE

Today ‎7th October 2011 His Excellency Dr Jakaya Mrisho Kikwete,The 4th and current President of the United Republic of Tanzania celebrates his 61st birthday.UKURASA WAKE KATIKA MTANDAO WA KIJAMII FACEBOOK  KASEMA ''‎7th October 2011 is my 61st birthday.Grateful for the opportunities that my nation and the world have given me to serve through all my life and looking forward to do it more.Thank you all for the birthday wishes'' KWA NIABA YA WASOMAJI WA KIBARAZA HIKI NIKUTAKIE MAADHIMISHO MEMA NA YENYE FURAHA YA SIKU YAKO YA KUZALIWA,MUNGU AKUZIDISHIE NGUVU,HEKIMA NA AFYA NJEMA UZIDI KUWATUMIKIA WATANZANIA AMBAO PAMOJA NA MATATIZO YALIYOPO BADO WANA MATUMAINI NA WEWE.HAPPY 61ST BIRTHDAY MR PRESIDENT.