23 May, 2011

UNAIKUMBUKA HII??

Hiki kiatu kilikua maarufu sana zamani siku hizi sikioni tena sijui bado kinavaliwa? Na kama kinavaliwa sijui utaanguka mara ngapi kwenye hizi barabara zetu? Hiki huvaliwa na suruali yake (hasa draft) ambayo ni pana kwa chini nyembamba karibia kubana fulani kwenye magoti.Si kila mtu alikua na kiatu kama hiki jina kama sikosei ni Laison (kama kuna jina lingine usisite nitafurahi kulijua). Pia sikumbuki ni miaka gani ila zamani niliweza ona watu wachache wanavaa na ilikua fashion by then.Wewe je umewahi kuona hiki kiatu? je kina kukumbusha nini??