08 April, 2010

Vitu vinavyo udhi katika maisha ya kila siku

1.kutaka usalimiwe ikiwa wewe hutaki kusalimia
2.kutafsiri mtu kwa namna aonekanavyo mfano: mkimya anadharau, hapendi ongea na watu, anajiona; muongeaji sana: atasemwa mwongo, mr/miss misifa, anajifanya mjuaji (maarufu kama much know!!!); ukiwa mnene a.k.a bonge: watasema manyama uzembe, mvivu na usiombe uwe na kitambi simalizii watakayosema hehehe!! ( au sema wewe, unadhani watasemaje?)
3.kudharau mtu mwingine labda kwa kipato chake kidogo ili hali mwenye kipato cha wastani ama kikubwa hana uhusiano wowote na asiye nacho na hata kama kuna uhusiano kuwa nacho si kudharau asiye nacho kwani riziki ya mtu hupangwa na Mungu
4. Kulewa na kusumbua wengine
5.kudharau kazi, wadhifa,elimu,kipato,maisha,kabila,makazi,mavazi ya wengine
6. Kutongoza demu/mchumba/mke wa rafiki/ndugu yako (Tena bila aibu!!!!)
7.Kushika simu ya mwenzio na kuanza ku-browse phone book, gallery (kuangalia picha),kusoma meseji n.k
8. kuweka pass word kwenye simu ( hasa wapenzi!!!), unaficha nini????
9.kushika simu/computer ya mtu na kuanza kufanya settings bila ruhusa. Mfano simu: kubadiri ring tone, theme, menu n.k; Computer: kubadiri back ground,menu na kufungua files na kuanza kusoma ya humo
10.kutaka heshimiwa bila kuheshimu
11.Kuchunguza na kuzungumzia maisha ya mtu asiye kuhusu nap engine humjui na mbaya zaidi unajua haya kuhusu!
12.kumdharau usiye mjua
13. kumwelezea mtu usiye mjua kwa lolote.

Endeleza nyingine unazo zijua wewe hapo!
-----------------------------------------