29 April, 2011

LEO MAMBO YOTE ROYAL,KAZI TUTAFANYA AKISHAOA!!

                                                                      Kate & William

Ni ile siku iliyokua ikisubiriwa kwa hamu ambayo mjukuu wa Malikia Elizabeth wa pili Prince William anamuoa mchumba wake wa siku nyingi Kate Middleton.Ni siku ya kihistoria zaidi ambapo maandalizi ya harusi hii ya  familia ya malikia yamechukua muda mrefu kutokana na uzito wa tukio lenyewe.Katika kuwahi kujionea tukio live (sikwamba hawana Tv nyumbani) waingereza wengi wamekesha katika Tents nje ya jengo ambapo wawili hao wataoana mapema leo.

Katika tukio hilo ambalo litakua katika ulinzi mkali watu zaidi ya million moja wanatarajia kuhudhuria katika eneo hilo na watu Billion mbili wataona/sikia tukio hilo kupitia vyombo mbalimbali ikiwemo Live Tv,Internet,Radio etc.Habari zaidi zinasema wengine wata jiachia kwa party za mitaani katika kusherekea siku hii ya mapumziko wakati prince William anaoa  jijini London mapema leo. SI VIBAYA KWA WENYE MA HOTELI TANZANIA NA MAHALI PENGINE KUZINGATIA UMUHIMU WA SIKU  HII  KWA KUWABURUDISHA WATEJA WAO (WAINGEREZA) AMBAO KWA TANZANIA WAKO WENGI TU ILI WASIJIONE WAKO MBALI WAKATI WENZAO HUKU (UK)  WALA BATA SIKU NZIMA!

                               Mke na Mme watarajiwa Kate & William                                               

Wageni rasmi katika harusi hii ni 2000 na katika hali isiyo ya kawaida, pamoja na ukaribu uliopo kati ya UK na USA Rais Obama haja alikwa!! Kwa maana hio naye ataona kwenye Tv kama mimi (kama atakua na muda) hii kali  lol.

Kupata Ratiba ya Royal Wedding ingia hapa: http://www.theroyalweddingwilliamkate.com/the-wedding-day-schedule

Kuangalia ROYAL WEDDING LIVE ingia hapa: http://www.royalweddinglive.tv/kate-and-william-wedding-day/

ZAIDI YA WATU 280 WAFARIKI DUNIA KWA KIMBUNGA ALABAMA-MAREKANI

Watu takribani 280 wafariki dunia kwa kimbunga kikali kwa kimatumbi (Tornadoes) nchini Marekani.Kimbunga hicho kilichotokea kusini mwa Marekani (ALABAMA STATE) kimefanya uharibifu mkubwa wa maisha ya watu pamoja na mali zao.Mbali na kuua watu kimbunga hicho kimeharibu miundombinu kama umeme,nyumba,barabara na mingine mingi na kufanya watu wapoteane katika tafrani hio.

  RAMANI YA MAREKANI NA STATES ZAKE (ALABAMA NDIO SEHEMU YA MAAFA KATIKA RAMANI HII KUSINI KARIBU NA GULF OF MEXICO)

Tornado ni janga la asili kama ilivyo tetemeko la Dunia na hutokea pale upepo nyevu wa vugu vugu unapogongana na upepo mkavu wa baridi ambapo wimbi kali la upepo mkali na wenye nguvu hutengenezwa na kusafiri kwa mwendo wa takribani maili 100 kwa saa.Tornado ni janga ambalo hutokea mara kwa mara karibu na GHUBA YA MEXICO  kila Spring (wakati kama huu) na Summer kutokana na mgongano huo wa upepo nyevu na wa moto unaovuma toka  kusini (Ghuba ya Mexico) na kugongana na upepo baridi toka kaskazini mwa nchi ujulikanao kama 'Colder Dry Canadian Winds'.Huku kuna Watanzania wengi tu tuwaombee salama katika maafa hayo na wenye jamaa/ndugu  huko ni vema wakawasiliana kujua hali zao.

SIJUI SASA WATASEMA AMECHAKACHUA CHETI???!!

Born August 4, 1961 Honolulu, Hawaii,USA 

Barack Obama (Rais wa Marekani)


Baada ya utata kuhusu uraia wa Rais wa Marekani Barack Hussein Obama II,Whitehouse yaachia cheti cha kuzaliwa cha Rais huyo kuvunja utata uliovuma kwa muda mrefu sasa, Cheti kinaonyesha uraia wake kama Mmarekani na sio 'MKENYA' ukitaka kuona cheti bofya link hapa chini
http://www.whitehouse.gov/sites/default/files/rss_viewer/birth-certificate-long-form.pdf