09 June, 2010

Maswali yangu leo!

Tazama hii picha kisa niambie wewe ungekua ndo mkuu wa Mkoa/Wilaya ya nanihii na watoto ndio wako darasani kama hivi je ungekubali kutembelea LANDCRUISER VX/GX/TX tena V6 /V8 yenye injini size 4.7 Litres au zaidi???
Au ungesema upewe Escudo/Vitara,Hilux Surf, Rav4,Discovery,Freelander,Honda –CRV???? Nimetaja hizi gari kwani zote ziko na 4WD (kama kigezo ni 4WD) tena injini size haizidi 3 Litres. Tutasema hatuna hela au katika vipaumbele vyetu Elimu haipo??? Sijawahi sikia serikali imekosa hela ya kununua shangingi!!! Na kama wanapata ya mkopo basi wakope wajenge shule hii sio haki!!Je mtoto aliesoma shule kama hii na kwa mazingira haya ataelewa anacho fundishwa maana hapo MAKALIO YANA WAKA MOTO!!

Akifeli huyu nwanafunzi nani alaumiwe?? (mbaya zaidi siku zote mwanafunzi akifeli atalaumiwa HASOMI,JINGA, HALI HUDHURII VIPINDI(TRUANT) na maneno mengi ya aina hio) Hapa hata ningekua mimi kwa kuheshimu umuhimu wa makalio yangu nisinge soma!!! Niite jina lolote sawa tu (Lol!) kisa cha kuota sugu ya makalio?!!

Je mwalimu pamoja na wanafunzi wana raha gani kukaa katika pagari kama hili??? Hapo kuna kuelewana kweli?!! Kwani ni wazi hapa mwalimu ana woga jengo laweza anguka muda wowote, hali kadhalika wanafunzi!! Hivi wimbi la wanafunzi watoro likiongezeka nani alaumiwe?? Je tuseme sehemu kama hii hakuna viongozi?? Kama wapo nini mchango wao kwa jamii au ndo tuseme aliye shiba hamjui mwenye njaa?? Au tuseme eneo kama hili halina mgao wa bajeti?? Ok je hata wananchi imeshindikana kukusanya nguvu kupitia viongozi (kupitia mpango wa kushirikisha wananchi kujenga shule) ili kuboresha mazingira kama haya?? Ni kweli serikali haiwezi fanya kila kitu ila hii haijakaa sawa!

Cha ajabu kabisa ukute kiongozi aliye pewa dhamana na eneo hili hana habari kama kuna shule ipo namna hii kwani yeye na ofisi ofisi na yeye.Swali la mwisho…Kuna haja gani kua na VX/GX nyingiiiiiii wakati kuna sehemu kama hizi zinazo hitaji kuboreshwa? Hii ni sehemu moja tu ya Elimu sasa tukienda mambo ya Afya sijui hali ikoje sehemu kama hii!! Sitashangaa kama wamama wale wajawazito wanajifungulia PORINI!! Na vitanda hospitali zilizo na aspirin na panado tu au kukosa vyote na kulala mzungu wa nne ni anasa!!

Kwakweli nilishindwa kushangaa kuona eti Mbunge wa CHADEMA Mh Ndesamburo alitaka toa gari kituo cha afya huko moshi kama alivyo ahidi kwenye kampeni badala yake akapewa masharti magumu ikiwemo kufuta jina la mtoa msaada!! Hii sijui niite nini kwani hakuna asiyejua kama magari ya misaada yana majina ya wafadhili ubavuni, huyu ni MTanzania kabisa kaambiwa afute jina lake kama sio chuki za kisiasa ni nini? (hio ni aka Cheap politics) Siku nyingine mtu kama huyu/mwingine mwenye huruma kama hio atakua na moyo wa kusaidia??

Kwa habari zaidi soma hapa : http://www.habaritanzania.com/articles/2624/1/Moshi-waukana-msaada-wa-mbunge-wa-upinzani.

Pamoja na mambo mengine changamoto yangu ya leo kama kweli tunahitaji maisha bora kwa kila Mtanzania tuwe makini na vipaumbele vyetu na tusiweke chuki za kisiasa mbele kwani mwisho wa siku 'fahari wawili wakigombana nyasi ndio huumia' hapa wananchi/walipa kodi ndio wanaoumia. Tubadirike!