02 July, 2011

HATIMAYE ALIYEKUA MKURUGENZI WA IMF AACHIWA HURU

                                Aliyekua boss wa IMF akiwa anafuraha baada ya kuachiwa huru


Aliyekua  mkurugenzi wa shirika la fedha duniani (IMF) bwana Dominique Strauss Kahn (62) aachiwa huru baada ya madai ya kutaka kubaka muhudumu wa Hotel  May 14,2011  jijini New York kutiliwa mashaka.Uamuzi huo umetolewa na mahakama iliyokua ikisikiliza kesi hio Ijumaa ya tarehe 1 July (jana) baada ya kufanya uchunguzi wa madai na kukuta mdai amedanganya na  kuchanganya maelezo kitu kinacho ashilia ni mwongo na kumfanya mdaiwa kuachiwa huru bila dhamana na kuondolewa vikwazo vyote.Aidha kesi hio ambayo inaelekea kufutwa haina haraka ya kusikilizwa tena kama mwanzo na mdaiwa ameombwa kuhudhuria mahakamani mara kesi itapo tajwa!.


Kesi zote zingekua zinasikilizwa haraka hivi watu wasingekesha na kupata shida mahabusu tena kwa muda mrefu au huyu kwasababu ana vijisenti?


Kwa habari zaidi SOMA HAPA