20 May, 2010

Walofukuzwa kazi baada ya kuandika udaku facebook!!

Kama nilivyo ahidi kutoa mwendelezo wa 'Namna ya kufukuzwa kazi kwa kutumia facebook'' leo nawaletea baadhi tu ya walio fukuzwa baada ya kupatikana wameandika 'udaku' facebook tena bila kufikiri kama siku hizi ma-boss hawako nyuma kupitia mitandaoni kujua yanayo jiri.Siku hizi unaweza itwa interview wakati wameshakusoma mambo yako yote ya facebook sasa wale tunaopenda kujiachia huko unaweza jikuta unakosa kazi. Haya tujiunge kupata habari za waliofukuzwa chanzo kikiwa facebook!!

Msichana mmoja aitwaye Ashley Johnson ,22 huko North Calorina kafukuzwa kazi baada ya kuandika udaku facebook.Msichana huyo alisema wateja ambao yeye anaita ‘WA BEI RAHISI’ kwa kimatumbi ‘CHEAP CUSTOMERS’ wamemkalisha kwa saa moja zaidi ya muda aliotakiwa kumaliza kazi na baadae kumpa shukrani maarufu kama ‘tip’ ya $5.

Mwanadada huyo mhudumu wa Brixx Pizza alikasirika kwa kupewa 'tip' ndogo hata akadiriki kuwaita CHEAP wateja na kutaja na jina la mgahawa huo kama status message yake facebook.Bahati mbaya mdada huyu hakujua kama waajiri siku hizi wanapitia Facebook kusoma soma yaliyojiri.Hivyo dada huyo yakamkuta siku chache baadae baada ya meneja wake kuona alichoandika facebook ikiwa ni moja ya vitu ambavyo mfanyakazi huyo kakiuka kwani kawasema vibaya wateja, na kukiuka sera ya biashara ya mgahawa huo ikiwa ni pamoja na kuchafua jina kibiashara kwa jamii ya watumiaji wa mahali hapo . Hata hivyo mdada huyo baada ya kufukuzwa aliomba msamaha na hivi sasa yuko mbioni kutafuta kazi mpya.

Hii imefanya idadi ya wanaofukuzwa kutokana matumizi ya facebook kua kubwa siku hadi siku.Mfano mfanyakazi wakike (31) wa shirika la bima inchini Uswisi mwaka jana (2009) alifukuzwa kwa kubainika kutumia facebook akiwa kaomba ruhusa kua ni mgonjwa hawezi tumia computer siku hio kwani mwanga una msumbua. Zaidi soma hapa http://www.reuters.com/article/idUSTRE53N4JF20090424.

Sambamba na hio Kimberely Swan (16) mwanzoni mwa mwaka (2009) alifukuzwa kazi kwa kuandika facebook kama kazi inaboa na kuguna kwa sana tu. Zaidi soma hapa http://www.dailymail.co.uk/news/article-1155971/Teenage-office-worker-sacked-moaning-Facebook-totally-boring-job.html .

Si hao tu bali, Dan Leone mnamo April 2009 aliandika facebook kumkashifu mwajiri wake na baada ya kujua kama lilikua kosa alifuta mara moja ila kwa bahati mbaya haikusaidia. Hatimaye siku chache baadae alipigiwa simu kama kafukuzwa kazi. Zaidi soma hapa http://sports.espn.go.com/nfl/news/story?id=3965039.

Mnamo mwezi wa nane mwanamke mmoja mwenye asili ya kiingereza adaiwa kufukuzwa kazi baada ya kuandika facebook ‘’kazi inaboa’’ asikumbuke kwenye friends list yuko boss wake zaidi soma hapa http://stupididiotjerk.com/2009/08/12/another-person-gets-fired-due-to-facebook/ mwaka 2008 kijana kyle doyle wa Australia alifukuzwa kazi kwa kuomba likizo ya kuumwa. Baada ya kejeli za facebook aliombwa cheti cha matibabu aliposhindwa kutoa na kazi ikaishia hapo hapo.Zaidi soma hapa http://bb.nsmb.com/showthread.php?t=116471

Hawa ni baadhi tu ya waliofukuzwa kazi kutokana na kujiachia na facebook. Hata hivyo mijadala mbalimbali mitandaoni imethibitisha kua idadi kubwa ya watumiaji wa facebook ni wafanyakazi kwani ofisi nyingi zina Internet.Hivyo hiyo imepelekea wale wenye facebook accounts kua bize sana wakiwa kazini kwani pamoja na mambo mengine ni lazima wapitie facebook kuchat ama kuangalia yaliyo jiri pamoja na marafiki zao ama kuandikiana meseji.

Utafiti uliofanywa na Nucleus mwaka 2009 upo kama hivi:-

Facebook Usage At Work

Information-----------------------------------% of Respondents

Workers with a Facebook account--------------------77%
Facebook users that access Facebook at work-------61%
Workforce accessing Facebook at work---------------47%
Average minutes accessed per day---------------------15

Total lost productivity to Facebook across the entire employee population 1.47%

(Source: Nucleus Research, July 2009)

Na mwisho kabisa utafiti uliofanywa na Family attitudes hapa Uingereza umebaini kwamba facebook kama ni mtandao uliopendwa zaidi na wasichana kwa asilimia 40 ukilinganisha na wavulana kwa 6%. Katika utafiti huo wasichana walipo ulizwa wataje vitu vitatu muhimu sana kwao katika maisha, waliweza taja ,MARAFIKI,FAMILIA, FACEBOOK NA MSN.Wakati huo huo wavulana walitaja cha kwanza FAMILIA,MARAFIKI NA PESA. Je kwako wewe msomaji ungetaja nini kiwe cha kwanza? Na je iitwe Fail book kama ambavyo watu wameanza kuiita au ibaki kua Facebook??

Gari za kukodi..

Hivi wale jamaa wanao kodisha magari hua wanakagua magari yao kabla na baada ya kukodisha? Duh kama mambo yenyewe ndio haya kazi ipo.Au ndo cha mtu ma**!!!