05 September, 2011

NI AJABU LAKINI KWELI.. MAHUBIRI YA KUIKATAA CCM

HUYU PASTOR/MCHUNGAJI KATOA MAANA YA CCM KAMA CHAMA CHA MAJAMBAZI, KAMA HAITOSHI AZIDI KUKIBOMOA CHAMA HICHO KWA KUSEMA MUNGU HATAKI CCM,SWALI JE ANAPENDA CHADEMA,NCCR AU CUF??.SIKUMBUKI KUSOMA SEHEMU INAYOSEMA KANISANI/MSIKITINI WATU WANAENDA KUJIFUNZA SIASA ZAIDI YA KUFANYA IBADA AU KUSWALI!!


JE WEWE HUA UNAENDA KANISANI/MSIKITINI KUFANYA NINI??
HUYU KWA MTAZAMO TU HANA TOFAUTI NA HUYU
NA KWA HAKIKA ANGEKUA CCM NI HUYU HUYU ANGETUAMBIA MUNGU ANAPENDA CCM.UKISIKILIZA DAKIKA YA 1:37 ANASEMA ''Slaa iko mikononi mwako itumie vizuri kura yako'' MPAKA HAPO MPENZI MSOMAJI UTAJUA YEYE CHAMA GANI NA BILA SHAKA HICHO NDIO ATASEMA  MUNGU ANAKIPENDA!!

TOYOTA LANDCRUISER VX YA 2011

Kampuni ya Toyota inazidi kuwafurahisha wateja wake kwa kuzidi kutoa gari nzuri 4x4 kama Landcruiser VX Toyota Rav4 na nyingine nyingi.Kwakua hii ndio kazi yangu usisite kuniagiza nikutafutie gari (kwa anaye taka gari toka UK aina yoyote mfano Jaguar,Toyota,Range Rover,Suzuki,Scania, Mercedes Benz,BMW n.k)  kama nilivyosema kwenye blog hapo juu sambamba na 'dhumuni la blog' nimeona si vibaya kwa leo nilete japo picha za Landcruiser VX ya 2011 na ili uone muonekano wake na narudia tena ukitaka gari kutoka UK nipigie +447552621975 au niandikie via rijaki@ymail.com.Mwisho niseme asante kwa mlio toa ushirikiano tayari kupitia blog hii.


                  Mwonekano wa ndani sehemu ya mbele kwa dereva na dashboard                                            Kwa nje upande wa ubavu wa kushoto na nyuma
   Kwa mbele na ubavu upande wa kulia kwa dereva

ETI 'VAT' MAANA YAKE VATICAN?????

Kipande hiki cha video kimeeleza mambo kadha wa kadha yenye wasiwasi kama sio upotoshaji eti VAT ambayo ni 'Value Added Tax (Kodi ya Ongezeko la thamani) kama 'Vatican' na watu wanaitikia? Mwl.Nyerere apondwa eti alikua kiungo muhimu wa makanisa na alifanya maisha kuwa magumu na mzee Ali H Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa afagiliwa.Sambamba na hayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimedaiwa kuwa ni chama cha makafiri na kama yeyote aliye serikalini au CCM ngazi yeyote ana swali basi huyu jamaa yupo tayari kujibu.Aidha kanisa katoliki limetajwa kubomoa uislam(udini wa nini Tanzania?)

Kwa mengine mengi sikiliza hii clip ni ajabu na nimeshindwa kushangaa labda sijaelewa sikiliza na wewe mpenzi msomaji wa kibaraza hiki