29 April, 2011

ZAIDI YA WATU 280 WAFARIKI DUNIA KWA KIMBUNGA ALABAMA-MAREKANI

Watu takribani 280 wafariki dunia kwa kimbunga kikali kwa kimatumbi (Tornadoes) nchini Marekani.Kimbunga hicho kilichotokea kusini mwa Marekani (ALABAMA STATE) kimefanya uharibifu mkubwa wa maisha ya watu pamoja na mali zao.Mbali na kuua watu kimbunga hicho kimeharibu miundombinu kama umeme,nyumba,barabara na mingine mingi na kufanya watu wapoteane katika tafrani hio.

  RAMANI YA MAREKANI NA STATES ZAKE (ALABAMA NDIO SEHEMU YA MAAFA KATIKA RAMANI HII KUSINI KARIBU NA GULF OF MEXICO)

Tornado ni janga la asili kama ilivyo tetemeko la Dunia na hutokea pale upepo nyevu wa vugu vugu unapogongana na upepo mkavu wa baridi ambapo wimbi kali la upepo mkali na wenye nguvu hutengenezwa na kusafiri kwa mwendo wa takribani maili 100 kwa saa.Tornado ni janga ambalo hutokea mara kwa mara karibu na GHUBA YA MEXICO  kila Spring (wakati kama huu) na Summer kutokana na mgongano huo wa upepo nyevu na wa moto unaovuma toka  kusini (Ghuba ya Mexico) na kugongana na upepo baridi toka kaskazini mwa nchi ujulikanao kama 'Colder Dry Canadian Winds'.Huku kuna Watanzania wengi tu tuwaombee salama katika maafa hayo na wenye jamaa/ndugu  huko ni vema wakawasiliana kujua hali zao.

No comments: