12 August, 2010

Fine kama hii bongo ingemaliza ajali zote

Raia mmoja wa Sweden aishie Switzerland yamemkuta baada ya polisi kumfuatilia baada ya camera kushindwa kumpiga picha wakati akitembea mwendo hatarishi barabarani.Nchini Switzerland mwendo kasi katika barabara za masafa marefu (Motor ways) ni 74.5mph (120km/h). Kinyume na sheria mtu huyo mwenye miaka 37 amekamatwa anaendesha Mecedes Benz SLS kwa mwendo wa 186mph (299.34km/h) (huu ni mwendo wa kutafuta kifo duuh).

Msweden huyo ambaye ametozwa fine ya 650,000£ (fanya hesabu mwenyewe kupata ni kiasi gani kwa hela zetu za madafu!!!!) .Hiki ni kiasi kikubwa kabisa cha fine zilizowahi tolewa nchini humo na bila shaka mheshimiwa huyo hajawahi kusikia wala kuota fine kiasi hicho katika maisha yake yote tena akiwa anaendesha gari ya bei ndogo kabisa (140,000£ tu).

Jamaa huyo ambaye amejitetea kua speedometer ilikua mbovu kwahio hakuona yuko speed gani ametakiwa kulipa kiasi hicho cha fine bila maelezo.polisi wamedai alihitaji nusu kilometer kuweza kusimama na camera hazikuweza kumpiga picha kwani alikua juu ya kiwango cha uwezo wa camera kupiga picha ambazo ni speed chini ya 125mph (201km/h).Hivi fine kubwa kiasi hiki bongo zingesaidia kupunguza ajali barabarani?

Picha iliyopigwa na camera hio hata haionyeshi kama kimepita kitu gani kwani haionekani vizuri angalia picha hapo chini au angalia hapa http://uk.cars.yahoo.com/12082010/36/swedish-driver-gets-pound-650-000-speeding-fine-0.html