24 August, 2010

Katuni ya leo

Hapa nani kashinda wadau hahahaha! Kama mambo yenyewe ndio haya gonjwa la UKIMWI tunalikaribisha nyumbani kwetu kwa nguvu zote na mwisho wa siku tuanze kuulizana nani kauleta.Ungejibu nini kama swali kama hilo linakutokea??

Tiger Woods na mkewe watarikiana rasmi..

Tiger Woods na mkewe waachana rasmi kutokana kilichodaiwa kukosa uaminifu kwa muda mrefu kwa bwana Tiger dhidi ya mkewe (Elin Nordegren) mwenye asili ya Sweden mapema jana. Katika maamuzi ya kuvunja ndoa hio katika mahakama ya Bay County Circuit Court huko Florida waliokua wanandoa na wazazi wa watoto wawili walikubaliana kulea watoto wao kwa pamoja.

Hata hivyo katika kesi hio ya mcheza golf machachari na tajiri nambari moja duniani katika anga za michezo hakukuwa na madai kuhusu kugawana pesa kitu kilicho washangaza watu wengi.

Zaidi soma hapa: http://uk.eurosport.yahoo.com/23082010/58/tiger-woods-elin-nordegren-divorce.html

Mabadiliko Angalia Bongo Blog...


Natumaini kuwa mnaendelea vyema na shughuli za kila siku za kujenga taifa..Jambo la msingi tu kuhusu email hii hi kuwaomba wana blog wenzangu kuweza kunisaidia kuwataarifu wasomaji kupitia blog zenu kuhusu mabadiliko ya blog yangu kutoka http://www.angaliabongo.co.tz na sasa kuwa http:// www.angalia-bongo.com. Natumaini mtaweza kunisaidia kwa hilo.
NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI.
SARAH.