21 March, 2011

LIBYA SI SHWARI TENA!!

Baada ya vikao kadhaa vya baraza  la usalama la umoja wa mataifa kutafuta mstakabali wa machafuko nchini Libya ambapo China na Russia zilionyesha waziwazi kutoshiriki na lolote huko Libya.Marekani haikua tayari bila tamko la baraza la umoja wa mataifa ambalo limepita na Marekani iko mstari wa mbele kushambulia maeneo muhimu yanayosadikika kutunza silaha inchini Libya.Rais wa Marekani ambaye yupo ziarani nchini Brazil ametoa idhini ya jeshi lake kuendesha mashambulizi ya kijeshi inchini Libya.


Jengo la kijeshi lilio haribiwa Tripoli-Libya

Shambulizi la kwanza limeripotiwa kuharibu jengo kubwa la kijeshi na kuangusha ndege 4 za kijeshi za jeshi la Gaddafi.Hata hivyo Gaddafi ametangaza kuangusha ndege yeyote itayo onekana juu au eneo lote la Mediteranian sea zikiwemo ndege za abiria huku akitahadharisha kua atatumia silaha nzito ambazo hajaanza kutumia na ameahidi kushinda mashambulizi ya wana muungano wa umoja wa mataifa wakiongozwa na USA,UK & FRANCE.Vita kwa namna yoyote si nzuri Mungu awasaidie.


   
                                       Kituo kimoja cha ulinzi wa anga Libya kikiwa kinawaka moto baada ya kulipuliwa na majeshi ya muungano wa UK,USA na FRANCE.

Kwa habari zaidi soma hapa
>> http://abcnews.go.com/International/libya-international-military-coalition-launch-assault-gadhafi-forces/story?id=13174246

>> http://abcnews.go.com/wnt/video/special-report-target-libya-president-politics-war-obama-military-13175613&tab=9482930&section=1206853&playlist=1363340