08 June, 2011

MAISHA BORA KWA KILA....

Ndugu msomaji hapo chini ni picha ya usafiri wa Trekta huko Ludewa.Huu ni mfano tu wa maisha halisi watanzania walio wengi katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania.Kwa anaye ishi mjini atashangaa kuona maisha kama haya ila huo ndio ukweli wenyewe huko vijijini.Hapo walipo sina hakika hata wamevaa chochote miguuni ukimuondoa dereva lakini  wao wanaona ni maisha ya kawaida na wameshazoea..

Je mimi na wewe nani angependa kuishi maisha haya?  Ni kweli serikali haiwezi fanya kila kitu kuboresha maisha ya kila mmoja lakini je  hawa watu wamewezeshwa kujikwamua na maisha magumu? hua tunaambiwa kuna pembejeo za ruzuku je zinawafikia walengwa kwa bei nafuu kama ilivyo pangwa?  Ok tumewapa pembejeo za ruzuku ambazo sina hakika kama ni 'ruzuku' hizo bara bara za kupitisha mazao japo kwenda kuuza zipo?? Na mwisho kabisa niseme tu kama mlikua hamjui hawa ndio wapiga kura wetu kwa asilimia kubwa, swali je maisha  bora kwa kila mtanzania yapo au ni kauli mbiu tu ya kisiasa? maana hata bara bara yenyewe hapo mie sijaona ni kama wanakatisha porini tu au macho yangu?.                               Picha kwa hisani ya mzee wa matukio: Francis Godwin wa                http://francisgodwin.blogspot.com/. kwa habari na picha zaidi bofya hapo uone maisha bora kwa kila Mtanzania!!


Aidha sehemu kama hii nikiambiwa ambulance au gari ya kubebea wagonjwa ni kama hizi hapa sita shangaa
                                           Ambulance hii sijui ni ya wapi?
                                  Hii sijui niite nini.. ilimradi mgonjwa afike (na sina hakika kama atafika!!!)


 Hakika sitabisha kwasababu maisha haya nayajua na kuna sehemu ambazo nisha tembelea (vijijini) ukiumwa na ukapona mshukuru Mungu maana hata mie nili nusurika kufa huko hata kama una pesa hazitakusaidia maana hakufikiki kirahisi .Na sidhani kuna kiongozi mkubwa wa nchi ashawahi fika huko vijijini japo wana magari mazuri kama Land Cruiser VX/V8 na mengine ambayo wanatembelea mjini kwenye lami ambako hata Rav4 ingefaa!!.


Yaani hata wazungu watoa misaada nina imani hawaishi kushangaa wanavyoona usafiri wetu (viongozi) halafu unaita nchi masikini hapo hapo kuna mtu (Mtanzania) anapanda trekta  kusafiri tena ni mpiga kura (mwananchi)  wakati mpigiwa kura (kiongozi) anapanda  Land Cruiser V8 kwa jasho la mpanda trekta hivi hii ni haki kweli? Na kwanini apande trekta na sio bus? jibu la haraka hapo ni miundo mbinu mibovu hakuna mtu atathubutu kupeleka bus huko labda serikali yenyewe ifanye hivyo kama zamani yale ma bus ya serikali sijui yalifia wapi? Magari ya kusafirisha mizigo mfano Iringa kulikua na IRINGA RETCO,Mbeya MBEYA RETCO yale yalikwenda wapi?

ANATAFUTWA RENATHA BENEDICTO

Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.    

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu.    Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html) 

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio.   Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.