11 April, 2010

kichina china hapa!!

Katika shughuli/mpango mzima wakuongeza nanihii aka ndombolo kwakutumia teknolojia ya wale jamaa zetu wachina basi matokeo yake baadhi ndio kama haya. Ni vizuri watu kuchukua tahadhari unapo tumia madawa hayo ya kuongeza nanihii. Nasema hivo kwasababu mtaka yote siku zote hukosa yote.Pamoja na habari hii kuna waume kwa wanawake wengi ambao wamekwisha tumia hizi dawa za jamaa zetu wachina na wengine kwa lengo la kuongeza nanilii ila matokeo yake si kama walivyotaka. Mfano kuna mwanaume ambaye alikua na nanihii ndogo kakimbiwa sana na wake kwa udogo wa nanihii yake akaona suluhisho ni mchina matokea nanihii ilikua kubwa kupita size za kawaida kwahio akaanza kukimbiwa kwa ukubwa wa mzigo.

Hali kadhalika wanawake waliotaka kuongeza kidogo ndombolo/makalio waliharibikiwa na shepu na mpango mzima makalioni kwani panaweza ongezeka ambapo hapatakiwi hivo kuharibu mpango mzima wa eneo hilo.Tuwe makini na hizo dawa vinginevyo ukiwa kama hawa usimlaumu mtu kwani ni uamuzi wako kumkosoa muumba!



.




kazi ni kazi tu...

Ule msemo wa kazi ni kazi na riziki ni popote ili mradi mkono uende kinywani unaji dhihirisha katika picha hii. Mimi nilidhani haya mambo ni ya ngozi nyeusi tu! kumbe hata weupe wamo!! sasa tuache ubitozi tufanye kazi!!!! Katika pita pita zangu nimegundua kufanya baadhi ya kazi ulaya kumepewa jina maarufu kama KUPIGA BOX kwa baadhi ya kazi ( kama hio kazi yako........heheheh), kwahio TUPIGE BOX kama tunataka pesa of which najua kila mtu anazitaka kwahio tupige kazi kwa bidii kama huyu mama japo kwa namna mbali mbali kutokana na nafasi zetu ili tuweze peleka mkono kinywani vitu kama Burger, wings,vodka na mbege kama ipo unaweza nunua ukiwa na pesa!!! Ulaya kila kitu pesa ati!




Fanya kazi!!!!