22 September, 2011

WAASI LIBYA WAUA FAMILIA WALIYODHANI YA GADDAFI

Links to this post
Waasi nchini Libya wameua watu  wanne  wakidhani ni familia ya Gaddafi kutokana majina yao ya ukoo kua GADDAFI.Familia hio ambayo ilikua mbioni kuhamia Uingereza kwa usalama zaidi ilikumbana na dhahma hilo saa chache baada ya safari yao kuanza huko Libya.Msemaji wa familia hio akiongea kwa masikitiko makubwa amesema familia hio haina uhusiano wowote na Muammar Gaddafi.Lakini kwakua walijua majina yao yangeweza waponza na kuamua kuondoka bila kufanikiwa mpaka mauti yalipowafika.


Zaidi soma HAPA

JAYGONGA'S WHITE PARTY IN COVENTRY,UK SAT.24TH,SEPT 2011

Links to this post

14 September, 2011

MABADIRIKO TAREHE YA HARAMBEE KUCHANGIA MAAFA ZANZIBAR KWA WATANZANIA UK

Links to this post

Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza TANZ- UK  inawaomba radhi wanajumuiya na watanzania wote kuwa shughuli za fund-RaƬsing zilizokuwa  zifanyike katika ubalozi wetu london siku ya jumamosi tarehe 17 septemba 2011 saa nane mchana zimeahirishwa. 

Taarifa zaidi zitawafikia hapo baadaye, tutawajulisha punde tu tutakapo pata habari kamili. Tafadhali mjulishe na mwenzako

ASANTENI
 MWENYEKITI, 
TANZ-UK

MIDA YA KAZI- DULLAYO (VIDEO)

Links to this post

13 September, 2011

VITUKO AJALI YA MELI ZANZIBAR

Links to this post
ati mMILIKI WA MV SPICE ISLANDERS HAJULIKANI!!.HII HAIINGII AKILINI HIVI KWELI CHOMBO KIKUBWA KAMA HIKI KILIKUA KINAFANYA BIASHARA NA MMILIKI HAJULIKANI HII INA MAANA GANI?.NDIO TUSEME NDIO MFANO WA BIASHARA BUBU ?.NINA IMANI KAMA KIMEKUA KIMESHINDA TUZO ZA KAZI NZURI BASI MMILIKI ANGEJITOKEZA HARAKA LAKINI KWAKUA KIMELETA AIBU KWA TAIFA NDIO MMLIKI HAJULIKANI.MAMLAKA HUSIKA ZITAWAAMBIA NINI WATANZANIA AMBAO WAMEPOTEZA NDUGU ZAO KWA UZEMBE.JE MV BUKOBA HAIKUTOA FUNZO? JE WAKATI INAONDOKA BANDARINI HAIKUKAGULIWA KAMA INA MZIGO UNAO STAHILI TUKIACHIA MBALI UCHAKAVU WAKE? JE HII NI MOJA YA BIASHARA KUBWA AMBAZO HAZILIPIWI KODI? HAPA SERIKALI ISIPO WAJIBISHA WAHUSIKA BASI NI WAZI WATANZANIA WATAJUA KUNA MWANYA WA RUSHWA WA WAZIWAZI.NA KAMA HII HABARI HAPA CHINI NI KWELI BASI NI AIBU KUBWA!!


                                      >>>>>> SOMA ZAIDI HAPA CHINI NI AJABU>>>>>
BY DR. WOLFGANG H. THOME, ETN UGANDA | SEP 12, 2011
(eTN) - In an extraordinary, though not unprecedented turn of events, the government of Zanzibar has reportedly denied having any knowledge of the registered owners of the MV Spice Islander. The Spice Islander is the ferry between Unguja - commonly referred to as Zanzibar - and Pemba, that capsized and sunk on September 10, 2011 with over 600 or 800 people on board - the number has yet to be determined - leaving scores of passengers dead in the water and others struggling to survive by clinging on to debris until they could be pulled out of the water by rescuers.
Registration and licensing of ocean going vessels, however, has been confirmed to be a function of government by tourism stakeholders, one of whom said this in an email overnight:
"This is not just unreal but almost mocking those seeking answers, those who lost relatives on the islands. How can a government claim not to be aware of the owners and it is the same government giving them a license.
"We are also disturbed about conflicting figures, some of which put the total passengers to over 800 and then government mouthpieces try to shrink these figures to within the licensed number. What is going on here?
"The tragedy was avoidable if only rules were enforced. There is notorious corruption across all outlets of public services, and they are now just trying to whitewash the whole thing.
"It is high time that government brings us new safe ferries, which can be used to travel from one island to the other without risking our lives every time one sets foot on board."
The central government in Dar es Salaam did, according to media reports, release 300 million Tanzania Ssillings to assist bereaved families with funeral expenses.
The official number of casualties was given by a Zanzibar government spokesperson as just under 200 with nearly 600 survivors, which would put the overall number of passengers on board well over the licensed figure permitted. There is also no certainty over the number of bodies not yet recovered, as apparently no complete passenger manifest was produced prior to the ferry leaving for its last ill-fated journey to Pemba.
Reconciling survivors and casualties is, therefore, literally impossible for the authorities in Zanzibar. It is understood that Kenyan authorities are now also keeping a watch along the shores from across the Pemba Channel, in case any bodies would be spotted across the international border.
A legal aid organization is planning to sue Zanzibar's government and others involved for negligence. For more READ

HARAMBEE NCHINI UINGEREZA KUCHANGIA WAHANGA WA AJALI YA MELI ZANZIBAR

Links to this postJumuiya ya waTanzania nchini Uingereza TANZ-UK ikishirikiana na Jumuiya ya Wanzanzibar waishio Uingereza (ZAWA), Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa harambee (fundrising) maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.


Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba mwenye fedha au chochote kile cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana itakuwa sehemu ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.

anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni saa nane mchana (2pm sharp).

Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na:-
Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565,
ZAWA 07538063536,
TA London 07404332910

UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA,Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki Watanzania wote popote pale walipo duniani.
ASANTENI.
MWENYEKITI,
TANZ-UK

POLENI WAFIWA NA MAJERUHI AJALI YA MELI ZANZIBAR

Links to this post

                                        10/09/2011
Kweli ni pigo kubwa kwa mara nyingine Taifa lapoteza ndugu zetu katika ajali ya meli Zanzibar.Pole nyingi ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na wapendwa wao.
Poleni sana ndugu zetu   na tusichoke kumuomba Mungu atujalie hekima na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu pia awajalie viongozi wetu hekima zaidi waweze kukwepa majanga yaliyo ndani ya uwezo.  

Mwenyezi mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi na kuwaponya haraka walio nusurika. AMEN

Zaidi soma HAPAHAPA & HAPA

08 September, 2011

ANASEMA MUACHE KUMCHAFUA!!!

Links to this post
Bila shaka ujumbe umefika japo lugha aliyotumia hajaitendea haki kwa Tanzania ninayo ijua, kuna Holly fu*k na f*ck & Sh*t. Sijajua ilikua hasira au njia mpya ya kufikisha ujumbe! Kikawaida hayo maneno ni makali ukizingatia hii video imekusudiwa kuwekwa hadharani via youtube. Well, is freedom of speech/expression  lakini ujumbe ungefika vizuri kwa lugha nzuri na sio matusi.NI MTAZAMO TU WA KIBARAZA HIKI   KWA DADA YETU NA PIA IWE CHANGAMOTO KWA CELEBS WENGINE MNAPO AMUA KUONGEA YANAYO WAHUSU!

HII BADO NI CHANGAMOTO KUBWA KWA SERIKALI

Links to this post
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay akikabidhi ambulansi ya "kisasa" aina ya bajaj kwa mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dk Rajab Rutengwe (kushoto). Ambulansi za miguu mitatu zimesambazwa na serikali kusaidia kutoa huduma za afya vijijini ambapo mkoa wa Rukwa utapokea miguu hii mitatu 20. Picha na Hamza Temba!!! 

Maswali:
>>Je huyo mgonjwa atapataje huduma ya kwanza?
>>Je dereva atakua daktari/muuguzi ama?
>>Je kwa barabara tulizo nazo hii miguu mitatu  inakidhi kiwango?

Maoni:

>>Serikali tunashukuru kwa kutoa huduma ambayo ni tatizo sehemu nyingi Tanzania lakini hii haikidhi mahitaji kwa karne hii ya 21 bila kusahau miundombinu yetu ambayo bado sio mizuri sehemu nyingi.

>>Ni bora zinunuliwe gari hata za kawaida (kama lengo ni kubana matumizi of which sina hakika kama hizo bajaji ni bei ndogo!) japo kufikisha mgonjwa hospitali ila sio pikipiki kwani ni rahisi mgonjwa kudhurika na jua,mvua (utelezi wa barabara kipindi cha masika), vumbi,au hata ajali kwani ni rahisi kupata ajali kwa pikipiki kuliko gari.

>>Kununua pikipiki kama nyenzo ya kusafirishia wagonjwa wakati wewe unatembelea  Landcruiser V8 (4.7Litre posh and expensive) hakuleti picha nzuri kwa wapiga kura na walipa kodi kwa ujumla au kwa maneno mengine serikali haijali wananchi ambao wameipa ridhaa ya kuwatumikia kwani hata 
matunda ya kodi zao hayaridhishi!


Free Thinking aka Mpayukaji  naye katoa  maoni yake kuhusiana na changamoto hii yasome  HAPA

TMK CHEGGE & TEMBA NDANI YA COVENTRY KESHO IJUMAA

Links to this post
Ijumaa hii ya tarehe 09/09/2011  wapenzi wa TMK watakua wanapata burudani ya nguvu toka kwa Chegge
 & Temba hapa |Coventry.Wale tusio penda stress basi tukanyooshe mkono mmoja juu pale PALMS BAR, Address ni 116 FAR GOSFORD CV1 5EA.Tuonane huko!!

                          Tukaweke mkono mmoja kama hivi!!

07 September, 2011

RAFIKI ZANGU WAKUMBANA NA FRAUD!!!!

Links to this post
Wanasema kuuliza sio ujinga na ni kweli rafiki zangu wawili wakumbana na michezo ya wizi mitandaoni lakini wakaamua kuuliza baada ya kupata wasiwasi na kushinda pound kibao na wakati huo huo kutakiwa kutoa kiasi kidogo cha pesa ili wapewe pesa wanazo dai wameshinda.Sasa mie najuuliza kama nimeshinda kweli si wapunguze zile ambazo nimeshinda na zilizo baki wanipe kwanini wanataka niongeze pesa? well tujiunge na kisa hapa chini


Mdau  wa kwanza:
 To: rijaki@ymail.com
Sent: Sunday, 4 September 2011, 14:51

Leo nimepata email toka huko uingereza kwa mtu aliyejitambulisha kama Angelina Keith mwenye umri wa miaka 87 ambaye mumewe alikufa kwenye ajali ya ndege. Kwa kuwa walikuwa na uwezo sana basi sasa anadai ameamua kuishi katika ranch yao na karibu asilimia 30 ya mali zake amegawia charity mbalimbali na kiasi kingine ameandikia check kwangu na kuiacha DHL london kwa lengo la kutuma huku. katoa jina, namba ya simu na namba ya siri ya bahasha (brown envelope) yenye hiyo check nikatuma email kwa hao DHL wakasema ni kweli kuna hiyo bahasha ninachotakiwa ni kupeleka taarifa zangu kama jina, anuani namba siri na kisha nitatakiwa kulipia security fee pound 160 kisha wataleta.


 Nimeona kama vile hata wazungu wanaweza kuwa matapeli hebu niambie aina hii ya wizi ipoje hapo Uingereza. maana nimepiga simu yamepokea na kufuatilia kisha yakajibu lakini nimeona haiji akilini.....................Nikamshauri aachane mara moja na hao wezi mitandaoni kama haitoshi mdau huyu akataka kujua zaidi kwa kufuatilia DHL ndipo akabaini mchezo huo wa wizi na akanijibu......


Tuesday, 6 September 2011, 10:01


>>>kweli bwana majamaa haya ni majizi inavyonesha maana yanajifanya yanafanya kazi DHL Express lakini nimefungua mtandao wa DHL sijaona namba za simu yenyewe yanapiga simu karibu kila siku kuulizia nimelipa na kama nimelipa ni scan risiti ya malipo nitume kwa mtandao haraka.


Mdau wa pili:
Huyu alianza na kuulizasorry,eti unafahamu mashindano ya iphone mobile promo,mama yangu katumiwa meseji ya kushinda unaweza kunichunguzia maana isije ikawa matapeli,naomba 
uniulizie,kama ni kweli


*Nikaomba kupata maelezo aliyopata kwenye ujumbe nayo ni:-


message imetoka iphone mobile promo UK, iliandikwa kuwa your cell phone number has won 715000 pounds from I- PHONE-UK,for claims of prize wakatutumia email iphoneclaims @gmail.com.ss tulivyo watumia meseji ya kupata huo ushindi waka tutumia verification form ambayo tulijaza jina la mama,namba ya cm ya ushindi anuani,network name ,maana wanasema ni mashindano ya kwanza yaliyo tumia automated ramdom computer kwa kutumia namba za simu,sasa walipotoa option ya kupata pesa kuna ya kufuata huko london hadi adress wametoa,au njia ya ndege ambayo ni cheki au kutumia bank ya western union .sisi tuliomba watumie njia ya barclays ,wametutumia form ya barclays lkn ukitumia njia hiyo wanatuma kama dollars.na mtu ambaye amepewa jukumu hilo ni stephen elop na namba za simu wametoa ambazo ni+4915118186861
naomba unitafitie maana wametoa hadi Adress zao za hapo london na iko under BRITISH LAW.**Ndugu wasomaji hizi ni fraud (kudanganya ili kupata pesa) na nime post nyingi sana katika blog hii.Wanaweza kukupata kwa njia ya simu,email au hata barua kwa njia ya posta kwa hio ukipata ujumbe kama huo si vibaya kuuliza au kuupotezea ukifanya kimya kimya basi jiandae kulia kilio cha samaki!!.Dar es salaam na sehemu nyingine watu wameibiwa eti mtu anakuambia ananunua paka mweusi kwa MILLION 2 hivi mtu huwezi shituka kama ni wizi unataka kufanyika?.Kiufupi nimefurahishwa na hawa ambao wameuliza na nimesha wajibu huu ni wizi tu wa mitandaoni waachane nao**


Kwa habari zaidi kuhusu fraud bonyeza HAPAHAPAHAPA HAPA NA HAPA  05 September, 2011

NI AJABU LAKINI KWELI.. MAHUBIRI YA KUIKATAA CCM

Links to this post
HUYU PASTOR/MCHUNGAJI KATOA MAANA YA CCM KAMA CHAMA CHA MAJAMBAZI, KAMA HAITOSHI AZIDI KUKIBOMOA CHAMA HICHO KWA KUSEMA MUNGU HATAKI CCM,SWALI JE ANAPENDA CHADEMA,NCCR AU CUF??.SIKUMBUKI KUSOMA SEHEMU INAYOSEMA KANISANI/MSIKITINI WATU WANAENDA KUJIFUNZA SIASA ZAIDI YA KUFANYA IBADA AU KUSWALI!!


JE WEWE HUA UNAENDA KANISANI/MSIKITINI KUFANYA NINI??
HUYU KWA MTAZAMO TU HANA TOFAUTI NA HUYU
NA KWA HAKIKA ANGEKUA CCM NI HUYU HUYU ANGETUAMBIA MUNGU ANAPENDA CCM.UKISIKILIZA DAKIKA YA 1:37 ANASEMA ''Slaa iko mikononi mwako itumie vizuri kura yako'' MPAKA HAPO MPENZI MSOMAJI UTAJUA YEYE CHAMA GANI NA BILA SHAKA HICHO NDIO ATASEMA  MUNGU ANAKIPENDA!!

TOYOTA LANDCRUISER VX YA 2011

Links to this post
Kampuni ya Toyota inazidi kuwafurahisha wateja wake kwa kuzidi kutoa gari nzuri 4x4 kama Landcruiser VX Toyota Rav4 na nyingine nyingi.Kwakua hii ndio kazi yangu usisite kuniagiza nikutafutie gari (kwa anaye taka gari toka UK aina yoyote mfano Jaguar,Toyota,Range Rover,Suzuki,Scania, Mercedes Benz,BMW n.k)  kama nilivyosema kwenye blog hapo juu sambamba na 'dhumuni la blog' nimeona si vibaya kwa leo nilete japo picha za Landcruiser VX ya 2011 na ili uone muonekano wake na narudia tena ukitaka gari kutoka UK nipigie +447552621975 au niandikie via rijaki@ymail.com.Mwisho niseme asante kwa mlio toa ushirikiano tayari kupitia blog hii.


                  Mwonekano wa ndani sehemu ya mbele kwa dereva na dashboard                                            Kwa nje upande wa ubavu wa kushoto na nyuma
   Kwa mbele na ubavu upande wa kulia kwa dereva

ETI 'VAT' MAANA YAKE VATICAN?????

Links to this post
Kipande hiki cha video kimeeleza mambo kadha wa kadha yenye wasiwasi kama sio upotoshaji eti VAT ambayo ni 'Value Added Tax (Kodi ya Ongezeko la thamani) kama 'Vatican' na watu wanaitikia? Mwl.Nyerere apondwa eti alikua kiungo muhimu wa makanisa na alifanya maisha kuwa magumu na mzee Ali H Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa afagiliwa.Sambamba na hayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimedaiwa kuwa ni chama cha makafiri na kama yeyote aliye serikalini au CCM ngazi yeyote ana swali basi huyu jamaa yupo tayari kujibu.Aidha kanisa katoliki limetajwa kubomoa uislam(udini wa nini Tanzania?)

Kwa mengine mengi sikiliza hii clip ni ajabu na nimeshindwa kushangaa labda sijaelewa sikiliza na wewe mpenzi msomaji wa kibaraza hiki