13 September, 2011

VITUKO AJALI YA MELI ZANZIBAR

ati mMILIKI WA MV SPICE ISLANDERS HAJULIKANI!!.HII HAIINGII AKILINI HIVI KWELI CHOMBO KIKUBWA KAMA HIKI KILIKUA KINAFANYA BIASHARA NA MMILIKI HAJULIKANI HII INA MAANA GANI?.NDIO TUSEME NDIO MFANO WA BIASHARA BUBU ?.NINA IMANI KAMA KIMEKUA KIMESHINDA TUZO ZA KAZI NZURI BASI MMILIKI ANGEJITOKEZA HARAKA LAKINI KWAKUA KIMELETA AIBU KWA TAIFA NDIO MMLIKI HAJULIKANI.MAMLAKA HUSIKA ZITAWAAMBIA NINI WATANZANIA AMBAO WAMEPOTEZA NDUGU ZAO KWA UZEMBE.JE MV BUKOBA HAIKUTOA FUNZO? JE WAKATI INAONDOKA BANDARINI HAIKUKAGULIWA KAMA INA MZIGO UNAO STAHILI TUKIACHIA MBALI UCHAKAVU WAKE? JE HII NI MOJA YA BIASHARA KUBWA AMBAZO HAZILIPIWI KODI? HAPA SERIKALI ISIPO WAJIBISHA WAHUSIKA BASI NI WAZI WATANZANIA WATAJUA KUNA MWANYA WA RUSHWA WA WAZIWAZI.NA KAMA HII HABARI HAPA CHINI NI KWELI BASI NI AIBU KUBWA!!


                                      >>>>>> SOMA ZAIDI HAPA CHINI NI AJABU>>>>>
BY DR. WOLFGANG H. THOME, ETN UGANDA | SEP 12, 2011
(eTN) - In an extraordinary, though not unprecedented turn of events, the government of Zanzibar has reportedly denied having any knowledge of the registered owners of the MV Spice Islander. The Spice Islander is the ferry between Unguja - commonly referred to as Zanzibar - and Pemba, that capsized and sunk on September 10, 2011 with over 600 or 800 people on board - the number has yet to be determined - leaving scores of passengers dead in the water and others struggling to survive by clinging on to debris until they could be pulled out of the water by rescuers.
Registration and licensing of ocean going vessels, however, has been confirmed to be a function of government by tourism stakeholders, one of whom said this in an email overnight:
"This is not just unreal but almost mocking those seeking answers, those who lost relatives on the islands. How can a government claim not to be aware of the owners and it is the same government giving them a license.
"We are also disturbed about conflicting figures, some of which put the total passengers to over 800 and then government mouthpieces try to shrink these figures to within the licensed number. What is going on here?
"The tragedy was avoidable if only rules were enforced. There is notorious corruption across all outlets of public services, and they are now just trying to whitewash the whole thing.
"It is high time that government brings us new safe ferries, which can be used to travel from one island to the other without risking our lives every time one sets foot on board."
The central government in Dar es Salaam did, according to media reports, release 300 million Tanzania Ssillings to assist bereaved families with funeral expenses.
The official number of casualties was given by a Zanzibar government spokesperson as just under 200 with nearly 600 survivors, which would put the overall number of passengers on board well over the licensed figure permitted. There is also no certainty over the number of bodies not yet recovered, as apparently no complete passenger manifest was produced prior to the ferry leaving for its last ill-fated journey to Pemba.
Reconciling survivors and casualties is, therefore, literally impossible for the authorities in Zanzibar. It is understood that Kenyan authorities are now also keeping a watch along the shores from across the Pemba Channel, in case any bodies would be spotted across the international border.
A legal aid organization is planning to sue Zanzibar's government and others involved for negligence. For more READ

HARAMBEE NCHINI UINGEREZA KUCHANGIA WAHANGA WA AJALI YA MELI ZANZIBAR




Jumuiya ya waTanzania nchini Uingereza TANZ-UK ikishirikiana na Jumuiya ya Wanzanzibar waishio Uingereza (ZAWA), Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa harambee (fundrising) maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.


Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba mwenye fedha au chochote kile cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana itakuwa sehemu ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.

anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni saa nane mchana (2pm sharp).

Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na:-
Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565,
ZAWA 07538063536,
TA London 07404332910

UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA,Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki Watanzania wote popote pale walipo duniani.
ASANTENI.
MWENYEKITI,
TANZ-UK

POLENI WAFIWA NA MAJERUHI AJALI YA MELI ZANZIBAR


                                        10/09/2011
Kweli ni pigo kubwa kwa mara nyingine Taifa lapoteza ndugu zetu katika ajali ya meli Zanzibar.Pole nyingi ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na wapendwa wao.
Poleni sana ndugu zetu   na tusichoke kumuomba Mungu atujalie hekima na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu pia awajalie viongozi wetu hekima zaidi waweze kukwepa majanga yaliyo ndani ya uwezo.  

Mwenyezi mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi na kuwaponya haraka walio nusurika. AMEN

Zaidi soma HAPAHAPA & HAPA