07 June, 2010

Hivi ndivyo ilivyokua leo Tanzania vs Brazil

Angalia mwenyewe kisa toa maoni yako!Aidha sishangai kwa wale walosema hawashabikii Tanzania (Taifa stars )hata kidogo japo kua ni wa Tanzania halisi!.Kama hii ilikua njia ya kutangaza Tanzania kiutalii ama vyovyote ni vema kungekua na njia mbadala kutangaza huo utalii.Tanzania ni nchi masikini sana na haistahili kufuru ya namna hii wakati huu ambao bajeti yetu bado haijitoshelezi bila misaada toka nje.

Au sivyo labda kama Brazil wamecheza na Tanzania kama ile soccer aid ya England vs ROW( The Rest of the World) kwa lengo la kusaidia nchi masikini.Lakini kama ndio tumejifanya kulipa basi walipa kodi hawana haki kwani hakuna asiyejua kama soka ni miongoni mwa michezo ya ghari duniani.Pamoja na kutambua kua ukitaka pesa tumia pesa kuna haja ya kuangalia namna hio pesa unayo wekeza italeta matokeo gani na si kuwekeza tu ilikufurahisha watu.

Nina amini watu wa utali wanao watalaamu wa kutosha kuweza kushauri namna endelevu na yenye manufaa katika kutangaza utalii.Sina hakika kama hii ndio njia nafuu wameweza shauri itumike kutangaza utalii.Na kwa mtindo huu neno 'misuse of public funds' halitakufa midomoni mwa walipa kodi mpaka hapo watakapo zinduka na kusema 'enough is enough bye bye doxa World!'

Mwisho kabisa labda niulize swali Ivi hela za kuwalipa hao Brazil nani anatoa/zimetoka wapi? Na kwa kiasi gani zitakua na manufaa kwa taifa changa kama Tanzania ukizingatia gharama ya kuwaleta? Je hio ndo njia nafuu kabisa ya kutangaza utalii Tanzania?