Showing posts with label Changamoto-Elimu. Show all posts
Showing posts with label Changamoto-Elimu. Show all posts

12 June, 2011

CHANGAMOTO YA LEO

Hakika kwa mtu ambaye hajui mazingira ya elimu tuliyonayo Tanzania hususani vijijini hawezi amini mazingira kama haya, kama haitoshi anaweza dhani Haki elimu wanataka kuiumbua tu serikali lakini huu ndio ukweli wenyewe. Mazingira ya kusomea sio mazuri kabisa katika shule nyingi hata walimu wanavumilia tu jamani  haya mazingira sio kabisa. Darasa utadhani gofu?

Ni imani yangu serikali inaona hivi vielelezo basi kipaumbele kiwekwe katika elimu maana huo utakua msingi moja wapo mzuri wa kuondoa umasikini Tanzania kwani kwa mazingira haya sidhani kama kuna mtoto anaweza fauru masomoyake.Na saa nyingine watoto tunawalaumu bure mazingira wanayo somea ni magumu kiasi kwamba shule inakua kama jela matokeo yake wanafunzi kutoroka shule.

Angalia video hii  uone mazingira wanayo somea viongozi wa kesho(sijui ndio lini?)
                  Kwa hisani ya Hakielimutz

Yaani hapa wakisema kila mtu apige picha ya shule ya msingi aliyosoma kuna watu tutashindwa kuonyesha hio picha maana ni aibu hata watu kuiona japokua sasahivi mtu uko kwenye nafasi fulani (Boss).Ni wachache tutafurahia kuonyesha shule tulizosoma.Sasa tunazisaidiaje hizi shule? 

03 May, 2011

NANI ALAUMIWE??

Hivi mwanafunzi kama huyu akifeli ata mlaumu nani?. kweli walimu wetu wana kazi kubwa sana kama mambo yenyewe ndio haya.Hivi kwani mtu huwezi zima simu ukiwa darasani ok, kuzima ngumu weka silent basi kwani simu kuita darasani mbali na kukupotezea muelekeo katika kipindi inaharibu utulivu na mwendelezo wa kipindi darasani.Mie naona wanafunzi wa aina  hii aidha wanyang'anywe simu kama hawaweza fata masharti au watolewe nje ya darasa waka ongee vizuri huko nje kama simu ina umuhimu kuliko kipindi.

Maadili Mashuleni (Kazi safi ya Haki Elimu)


Ni wazi kwamba serikali haiwezi kufanya kila kitu kudhibiti maadili ya wanafunzi ila inawezekana kwa ushirikiano wa wazazi, walimu ama walezi.Kwa wazazi kama unamnunulia mtoto wako simu ni vema umwambie matumizi ya hio simu akiwa shule, kwa walimu ni vema kuwaambia au kuweka tangazo linalo zuia matumizi ya simu muda wa masomo au darasani.Pia wazazi tuwe karibu na watoto wetu kujua hata wanaishi vipi na shule wanaendeleaje,utakuta mtoto ana simu ambayo hata baba au mama hawana (nina maana ya Gharama sana) mnunuzi hajulikani na simu hio hutumika wakati wa shule na usiku nyumbani wakati hata wazazi hio namba hawaijui.

Kama wazazi tunajiweka mbali na watoto wetu wa shule basi hata wasipo faulu tusilalamike.Ijulikane kwamba kusoma inahitaji moyo na faraja ya wazazi ni muhimu katika masomo.Ni lazima mzazi ujue maendeleo ya mwanao angalau kwa kila muhula.Kwakuto fatilia maendeleo ya mwanafunzi ndio siku ya siku unakuta mtoto wako ni mvuta bangi tu shule inamboa haitaki tena, kafukuzwa ana mimba (kwa wasichana) au tu amekua mtoto aliyekosa maadili kwa namna zote.Zamani mtu anaweza sema hajui sasa haki elimu ndio hao wanafichua maovu mashuleni.Wazazi,Waalimu pamoja na Serikali ni lazima tuwajibike sehemu zinazo tuhusu.

09 June, 2010

Maswali yangu leo!

Tazama hii picha kisa niambie wewe ungekua ndo mkuu wa Mkoa/Wilaya ya nanihii na watoto ndio wako darasani kama hivi je ungekubali kutembelea LANDCRUISER VX/GX/TX tena V6 /V8 yenye injini size 4.7 Litres au zaidi???




Au ungesema upewe Escudo/Vitara,Hilux Surf, Rav4,Discovery,Freelander,Honda –CRV???? Nimetaja hizi gari kwani zote ziko na 4WD (kama kigezo ni 4WD) tena injini size haizidi 3 Litres. Tutasema hatuna hela au katika vipaumbele vyetu Elimu haipo??? Sijawahi sikia serikali imekosa hela ya kununua shangingi!!! Na kama wanapata ya mkopo basi wakope wajenge shule hii sio haki!!Je mtoto aliesoma shule kama hii na kwa mazingira haya ataelewa anacho fundishwa maana hapo MAKALIO YANA WAKA MOTO!!

Akifeli huyu nwanafunzi nani alaumiwe?? (mbaya zaidi siku zote mwanafunzi akifeli atalaumiwa HASOMI,JINGA, HALI HUDHURII VIPINDI(TRUANT) na maneno mengi ya aina hio) Hapa hata ningekua mimi kwa kuheshimu umuhimu wa makalio yangu nisinge soma!!! Niite jina lolote sawa tu (Lol!) kisa cha kuota sugu ya makalio?!!

Je mwalimu pamoja na wanafunzi wana raha gani kukaa katika pagari kama hili??? Hapo kuna kuelewana kweli?!! Kwani ni wazi hapa mwalimu ana woga jengo laweza anguka muda wowote, hali kadhalika wanafunzi!! Hivi wimbi la wanafunzi watoro likiongezeka nani alaumiwe?? Je tuseme sehemu kama hii hakuna viongozi?? Kama wapo nini mchango wao kwa jamii au ndo tuseme aliye shiba hamjui mwenye njaa?? Au tuseme eneo kama hili halina mgao wa bajeti?? Ok je hata wananchi imeshindikana kukusanya nguvu kupitia viongozi (kupitia mpango wa kushirikisha wananchi kujenga shule) ili kuboresha mazingira kama haya?? Ni kweli serikali haiwezi fanya kila kitu ila hii haijakaa sawa!

Cha ajabu kabisa ukute kiongozi aliye pewa dhamana na eneo hili hana habari kama kuna shule ipo namna hii kwani yeye na ofisi ofisi na yeye.Swali la mwisho…Kuna haja gani kua na VX/GX nyingiiiiiii wakati kuna sehemu kama hizi zinazo hitaji kuboreshwa? Hii ni sehemu moja tu ya Elimu sasa tukienda mambo ya Afya sijui hali ikoje sehemu kama hii!! Sitashangaa kama wamama wale wajawazito wanajifungulia PORINI!! Na vitanda hospitali zilizo na aspirin na panado tu au kukosa vyote na kulala mzungu wa nne ni anasa!!

Kwakweli nilishindwa kushangaa kuona eti Mbunge wa CHADEMA Mh Ndesamburo alitaka toa gari kituo cha afya huko moshi kama alivyo ahidi kwenye kampeni badala yake akapewa masharti magumu ikiwemo kufuta jina la mtoa msaada!! Hii sijui niite nini kwani hakuna asiyejua kama magari ya misaada yana majina ya wafadhili ubavuni, huyu ni MTanzania kabisa kaambiwa afute jina lake kama sio chuki za kisiasa ni nini? (hio ni aka Cheap politics) Siku nyingine mtu kama huyu/mwingine mwenye huruma kama hio atakua na moyo wa kusaidia??

Kwa habari zaidi soma hapa : http://www.habaritanzania.com/articles/2624/1/Moshi-waukana-msaada-wa-mbunge-wa-upinzani.

Pamoja na mambo mengine changamoto yangu ya leo kama kweli tunahitaji maisha bora kwa kila Mtanzania tuwe makini na vipaumbele vyetu na tusiweke chuki za kisiasa mbele kwani mwisho wa siku 'fahari wawili wakigombana nyasi ndio huumia' hapa wananchi/walipa kodi ndio wanaoumia. Tubadirike!