11 July, 2011

NILICHOGUNDUA:UDANGANYIFU SIMU ZA MIKONONI

Baadhi ya hii mitandao ya simu za mikononi na nyumbani ni wezi kuliko tunavojua,hivi inawezekanaje unipigie simu na kuacha ujumbe wa promotion  za kampuni nizisikilize kwa gharama zangu? As if hio promotion ni lazima kuisikiliza!! yaani usipo pokea simu wakipiga wanakuachia ujumbe wa sauti ambao kuusikiliza unakatwa salio.Hata hivyo wanaotupigia simu toka nyumbani bongo tunashukuru kutupigia ila kama mtu hapokei acha ujumbe.Unakuta mtu kaacha voicemail hajaongea chochote wakati mie nasikiliza hio voicemail na nakatwa salio.


Anyways tuache hio mimi binafsi ni Tomaso haswaa na nimejaribu kutumia mitandao mingi kwa kufuata masharti ya mtandao wa simu nikitaka kupiga simu bongo lakini ukweli ni kwamba matangazo tunayo ona ni tofauti na hali halisi mfano juzi juzi nimejiunga na mtandao mmoja hapa Uingereza matangazo yao ni kwamba ukipiga Tanzania ni pence 1 kwa dakika nimetumia pound 5 na simu imekata chini ya dakika 25!!!. Leo tarehe 11,July 2011 nimekutana na Tangazo la kampuni hio hio  linasema kupiga simu Tanzania ni 10 pence kwa dakika nikafungua ukurasa wao kuhakiki ukweli  nilichokuta sikuamini macho yangu DAKIKA 1 NI  PENCE 19 NA SIO 10!!!.
                                             Tangazo lao la leo
Kwa mujibu wa tangazo lao la kwanza kama kupiga simu Tanzania ni pence moja kwa dakika inamaana nilitakiwa kupata dakika 500  kwani Pound 5 ni sawa na pence 500 sasa nikawa najiuliza mbona imekata mapema?  Nilichogundua ni kwamba dakika moja wanakata pence 20 na sio penny 1 kama tangazo linavyosema ..hio 20 ukiizidisha na dakika 25 unapata pence 500. Ina maana kama sasa imekua 10 pence kwa dakika basi ni dakika 50 kupiga Tanzania kwa Pound 5. Ila tangazo linakinzana na ukweli kwa maana ya viwango walivyopanga ukipiga simu Tanzania. kwa wale tunaopenda kupiga simu bongo kua makini na hii


Ukienda kwenye mtandao wao kuona bei halisi unakuta habari tofauti angalia mwenyewe hapo chini

PAYG Rates

International PAYG Rates
Select your destination to check the rates.
Destination 
Rates
Landlines5 pence per minute
Mobiles19 pence per minute
SMS10 pence  
READ MORE