13 February, 2011

Jumapili njema wadau wangu...

Natumaini mmekua na mapumziko mazuri ya mwisho wa wiki na sasa mnajiaandaa na kuanza wiki nyingine kesho jumatatu.Nawatakia mwanzo na mwisho mzuri wa wiki mpya inayokuja.Najua wengi(si wote)mnaisubiri siku ya kesho (jumatatu)kwa hamu (Valentine day) kwa nia mbalimbali (wengine) ikiwemo dating(wasio na wakutoka nao) na wenye wapenzi wao kudumisha mahusiano yao ikibidi (sio lazima).Ni vizuri japo tafsiri ya siku ya wapendanao imekua kinyume sana siku hizi kwani wengine hii ndio siku ya kungonoana ovyo-Kumbuka kuvaa condom kama sio mkeo, au mpenzi wako mmoja wa kudumu na unaye mwamini.

Kwa wale wazembe hii ndio siku ya kufanya ngono zembe tena wakiwa wamelewa kuambukizana magonjwa,kuvunja ndoa au uhusiano kwa sababu ambazo si za msingi na kusingizia shetani TULIA NA WAKO KAMA UNAYE.Ushauri wangu tumia siku hii kujadili mambo muhimu ya maisha na mpenzi wako (kwa wenye nao).Ni hayo tu kwa leo mfalme wa amani akawa ongoze-Amen.