14 October, 2011

LEO NI SIKU NA MWEZI AMBAO BABA WATAIFA ALIIAGA DUNIA


Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 – 14 October 1999)

LEO TAREHE 14 MWEZI WA 10 NI SIKU NA TAREHE AMBAYO TUNA ADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.SIKU HII NI SIKU MUHIMU KITAIFA NA PENGINE KIMATAIFA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA.KATIKA KUMBUKUMBU HII NI VEMA SERIKALI NA WATANZANIA KWA UJUMLA KUKUMBUKA MAMBO MUHIMU AMBAYO MWALIMU ALIKEMEA KW ANGUVU ZAKE ZOTE.MFANO WA MAMBO HAYO NI RUSHWA (CORRUPTION) MAARUFU KAMA KITU KIDOGO.

RUSHWA IMEKUA KAMA  MCHEZO AMBAO UMEZAGAA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA.SASA HIVI HATA UKITAKA HUDUMA YA AFYA YA HARAKA NI LAZIMA UTOE KITU KIDOGO.HUDUMA YA BURE BILA KITU KIDOGO HUWEZI PATA KWA MUDA UNAOTAKIWA.MCHEZO HUU MCHAFU UMEKUA KWA KIASI KIKUBWA KIASI KWAMBA KUNA WATANZANIA WANA AMINI BILA RUSHWA HUWEZI FANYA LOLOTE.

MADHARA YA RUSHWA NI PAMOJA NA KUTO KUWAJIBIKA KWA VIONGOZI WETU,UONGOZI USIO WA SHERIA,MAADILI WALA HAKI,AJALI,VIFO,MAENDELEO DUNI,HUDUMA MBOVU KWA JAMII MFANO HUDUMA ZA AFYA,ELIMU,BARABARA  N.K.ITAMBULIKE WAZI KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU KUA RUSHWA BADO NI ADUI MKUBWA ALIYEKOMAA NA KUIDIDIMIZA TANZANIA KATIKA NYANJA ZA KIUCHUMI,KIJAMII,KISIASA NA KIUTAMADUNI.TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) IWE CHOMBO HURU NA CHENYE NGUVU KUWAJIBISHA WATUHUMIWA WA RUSHWA WANAPO BAINIKA BILA KUJALI NANI,CHEO,DINI WALA KABILA.ITAKUA HAINA MAANA KILA SIKU TUWE TUNASIKIA TAKUKURU WAMKAMATA  KAMANDA FEKI HUKO SIJUI WAPI!


MANENO HAYA YA MWALIMU YAPO AU HAYAPO? KAMA YAPO MBONA HATUONI WALIO KULA FIMBO 12 NA KUWAONYESHA WAKE ZAO WAKIWA WANATOKA JELA?.RUSHWA NI ADUI MKUBWA WA HAKI!


SOMA ZAIDI HAPA KUHUSU HISTORIA YA MWAL.NYERERE

Umar Farouk Abdulmutallab to face life sentence!!

                                                              Umar
 Umar Farouk Abdulmutallab pleaded guilty to trying to blow up a transatlantic flight on Christmas Day 2009.Having pleaded guilty at his trial in Detroit, he is set to face life in prison when he is sentenced on 12 January 2012.Umar is a Nigerian born man aged 24 year old,privileged,very religious and teacher's dream.According to Michael Rimmer, a Briton who taught him history, told the BBC Umar Farouk Abdulmutallab had been "every teacher's dream - very keen, enthusiastic, very bright, very polite".[BBC]


Abdulmutallab's father, Alhaji Umaru Mutallab, said he had approached the US and Nigerian authorities to warn them about his son's views in November - weeks before the attempt to destroy the flight to Detroit with at least 300 passengers on board.


FIKIRIA HUYU NI MTOTO WAKO!!..HIVI KAMA MZAZI UNAPOONA MTOTO ANAENDA KUSIKO UNAKAA KUMUANGALIA AU UNACHUKUA HATUA? JE MZAZI WA UMAR ANAJISIKIAJE KUMKOSA MTOTO WAKE KWA MAISHA YAKE YOTE? JE ANGEMUONYA AMA KUMLAZIMISHA KUBADILI MISIMAMO YAKE SI ANGELISAIDIA KUOKOA MTOTO WAKE? KIJANA MDOGO KAMA HUYU SASA ATATUMIKIA KIFUNGO CHA MAISHA KWA FAIDA YA NANI? JE KUNA WAZAZI WANGAPI WA NAMNA HII? MTAZAMO WANGU MZAZI WA UMAR AMESHINDWA KUWAJIBIKA KIASI FULANI KAMA AKWELI ALIONA MTOTO WAKE ANAPOTEA ANGEFANYA KITU KUMUOKOA. JE UNGEKUWA WEWE MZAZI WA UMAR UNGEFANYAJE UNAPOONA MTOTO WAKO ANAPOTEA? KUTOA TAARIFA VYOMBO VYA DOLA BILA KUFANYA JITIHADA ZAKO KAMA MZAZI HAITOSHI NA HAIKUSTAHILI MTAZAMO WANGU. JE WEWE UNASEMAJE?


ZAIDI SOMA HAPA NA HAPA

MONEY vs HUMANITY


Nionavyo mimi pesa na utu wa mtu ni vitu viwili muhimu katika maisha ya kila siku, bahati mbaya siku zinavyo zidi kwenda uwepo wa pesa umekua na maana zaidi kuliko utu wa mtu.Kwanini? Mtu anaweza muondoa uhai mwenzie kisa anataka kupata pesa..Mtu yupo tayari kutafuta pesa hata kwa gharama ya maisha ya mtu mwingine.Sasa hivi imekua kawaida mtu ukisema kitu kama huna pesa basi husikilizwi kama umeongea cha maana.Aidha ukiwa na pesa unaweza fanya chochote kihalali au kinyume chake bila wasiwasi kwani pesa itakulinda.Hii ni sifa kubwa katika nchi zinazo endelea japo hata zilizo endelea kuna nafasi ya pesa lakini utu wa mtu una maana zaidi na hivyo pesa haiwezi kukulinda unapo hatarisha utu wa mtu kwa kutumia pesa zako.Je nchi yetu Tanzania inaona hili?


Ukitaka kuona kama pesa inamaana zaidi angalia picha hapo juu, sasahivi kuna maelfu ya watu Somalia na nchi jirani wakiwa na janga la njaa, maisha ya watu wengi yapo hatarini na muamko wa watu kutangaza janga hilo ni mdogo sana kulinganisha alipo kufa mwanzilishi wa kampuni ya Apple ambapo kila mtu ameonyesha kuguswa naye kwa namna moja ama nyingine.Je ni kwasababu alikua na pesa?, alitoa ajira nyingi? katoa bidhaa inayopendwa? mbunifu wa kihistoria katika maendeleo ya teknolijia?.jibu linaweza kua ni ndio lakini kwanini watu hawaguswi na hawa watu wanaokufa kila siku kwa kukosa chakula? ajali za kizembe kama zile za kuzidisha mizigo kwenye vyombo vya usafiri kwa manufaa ya watu fulani?.Je ni lini utu wa mtu utathaminika?

Things are back to normal on BlackBerry

This  made a headline  on various media after many of its users in Europe, the Middle East and Africa lost services on Monday.The BB users suffered problems with email, BBM and internet that were reported by customers later that day.Canadian firm Research in Motion (RIM) has apologised for the inconvenience and says that all services have now been restored.
Apparently there's no official word yet from RIM on what caused the problem but it's reported to be linked to a crashed server at a BlackBerry data centre.This  indeed will be another huge blow to the company and its reputation apart from the weaker sales in the face of strong competition from Android handsets and Apple's iPhone.