30 August, 2011

EID MUBARAK WADAU WOTE POPOTE MLIPO



SINA MENGI KWA LEO NIWATAKIE TU EID NJEMA MSHEREKEE KWA UPENDO NA AMANI,MSISAHAU KUOMBEA WAGONJWA, KUSAIDIA WENYE SHIDA,MASIKINI,YATIMA WENYE NJAA N.K.KIBARAZA HIKI KINAWATAKIA KUSHEREKEA VYEMA MWISHO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

29 August, 2011

MAANA HALISI YA VIJISENTI HII HAPA

Kama hii ni kweli basi mtu yeyote ambaye amewahi sikia kuhusu ''vijisenti'' angekubali kua kauli hio ilikuwa na ukweli ndani yake!!Kwa habari zaidi kuhusu vijisenti SOMA HAPA.

21 August, 2011

KUTOKA LIBYA:WAASI WAINGIA MJI MKUU TRIPOLI

Habari zilizojiri kutoka Libya zinasema mapigano makali yatikisa mji mkuu Tripoli kati ya waasi na wanajeshi wa serikali nchini humo.Watu zaidi ya 1000 wadaiwa kufa na wengine 5000 kuumia vibaya.Katika mapigano hayo makali yaliyozuka mida ya saa asubuhi leo waasi nchini Libya wamedai kumteka mtoto wa Gaddafi Saif Al-Islam. Kwa habari zaidi soma HAPA

19 August, 2011

HABARI NJEMA ZA SCHOLARSHIP UGHAIBUNI

Kama ilivyo ada kutoa habari mbalimbali zinazo husu scholarship leo nimeona nilete link ambazo zinaendana na mambo kama hayo.Zisome hizo link kwani nina imani zitakua na msaada kwa namna moja ama nyingine iwe kwako,nduguyo au rafiki yako.Hata hivyo ukipata habari kama hii si vibaya kumpa na mwenzio hivyo ndivyo tunaweza sambaza taarifa hii mpaka kwa wahitaji.


Soma hii kuhusu scholarship kupitia Michuzi blog kwa KUBOFYA HAPA
Pata habari za scholarship kwa kujiunga mjadala kwa KUBOFYA HAPA
Habari muhimu za scholarship bonyeza HAPA na HAPA
Soma zaidi habari  za scholarship   HAPA
Kuwa makini na utapeli wa scholarship  SOMA HAPA

17 August, 2011

SCHOLARSHIP KWA WATANZANIA SHEFFIELD UNIVERSITY-UK


Wadau mnaotafuta scholarship nimepita  The habari leo ambao unaweza kuwasoma HAPA kwamba chuo cha Sheffield kinatoa Scholarship kwa wanafunzi wa Kitanzania walioonyesha uhodari mkubwa katika masomo yao, na wana dhamiria kujiunga na Chuo hicho Septemba, 2011. Kwahio changamkieni hio muda ndio huo ushayoyoma
Ukitaka  maelezo zaidi, fika ofisi za wawakilishi wa Chuo hicho waliopo Tanzania kwa anuani ifuatayo:
Wawakilishi Tanzania

Wawakilishi maalum wa Chuo cha Sheffield Tanzania ni:

Uniserv Tanzania
Haidery Plaza, 1st Floor
A. H. Mwinyi Road/Kisutu Street.
Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 0(22) 2129036
Mobile: +255 787 019037 or +255 787 019047.
Fax: +255 0(22) 2129037
Kwa habari zaidi  toka chuo cha Sheffield wenyewe BONYEZA HAPA
Aidha kujua zaidi kuhusu scholarship za Uingereza na maisha  kwa ujumla tembelea British Council  kwa ku  BONYEZA HAPA 

Au wasiliana nao kwa anuani ifuatayo.
Samora Avenue / Ohio Street
P.O BOX 9100
Dar es Salaam,Tanzania
Simu:+255 (0) 22 2165300
Fax:  +255 (0) 22 2112669/2116577

 


16 August, 2011

TUNES OF THE WEEK (BONGO FLAVA)

Hii leo ndio list yangu ya Miziki mizuri ya Tanzania (Bongo flava) ikiongozwa na AY ft Lil Romeo,Lamyia.Hizi ni baadhi ya nyimbo bora za wasanii wetu siunajua mcheza kwao hutuzwa basi unaweza sikiliza kwa kubonyeza moja baada ya nyingine .Raha jipe mwenyewe usisubiri kupewa.




HIVI KWELI MAPENZI SUMU?

Kwa wale ambao wamekwisha chukua maamuzi magumu ya kuoa hasa miaka yasasa wanaweza kua na majibu  sahihi ya hili swali.Lakini pia katika harusi zote nilizo hudhuria hua sikosi kusikia ''MKAVUMILIANE NA KUHESHIMIANA'' hivi vitu viwili vikikosekana lazima ndoa iyumbe kwa namna moja ama nyingine.Hata hivyo ndoa sasa hivi hazidumu je tukubali kua mapenzi ni sumu?.Kimtazamo kama usemi huu una ukweli  kwa asilimia kubwa basi ishakua balaa!!

Mie nilikua nadhani ukiwa na mpenzi (Mke/Mme) basi ni raha kumbe inaweza kua kinyume chake.Na kwakua sasahivi ndio wanaita muda wa haki sawa,kwenda na wakati basi talaka ndio nje nje tujiulize kwanini?.Mbali na hio vijana sasahivi wanachelewa kuoa/kuolewa je tatizo ni nini?? Wengine wanasema ndoa ndoano je hii ni sababu ya ambao hawajaoa kutooa mapema?

Mtazamo wangu, kwakua imekua mila na desturi sehemu nyingi Africa hususani Tanzania toka zamani tumeona mwanaume ndio mtoa maumuzi ya mwisho (aka kichwa cha familia) si vibaya kwasasa mwanamke kushirikishwa katika maumuzi mbalimbali katika familia.Kusingizia haki sawa miongoni mwa wanawake na kujenga kiburi mwisho wake talaka.


Ni lazima kuheshimiana na kusikilizana kwa wapenzi/wanandoa (kama mnataka kufurahia).Mambo uliyofanya ukiwa pekee yako lazima uangalie kama yana mchango mzuri katika mahusiano kama sivyo basi achana nayo.Imekua utaratibu sasa hivi wapenzi kusema wanataka uhuru unakuta mtu kaoa/kaolewa na bado ana mawasiliano ya karibu na mpenzi wa zamani ya nini hasa?


 Hii tabia sio nzuri ndo mwanzo wa kupokelea simu chooni,kuzima simu ukiwa na wako,kuweka silent na kuwekeana password ambazo huongeza maswali ni je unaficha nini?? Mambo ya vidumu mpaka lini na magonjwa yaliyozagaa?? Nadhani hii ni moja ya sumu ya mapenzi, na kwanini tusiite mapenzi raha/matamu na maneno kama hayo kwa kuepuka hizo sumu ambazo ziko wazi?

MUWEKEZAJI AKIONA MANENO HAYA LAZIMA AKIMBIE SANA.


Au wewe unaonaje? Hii kwa muwekezaji haina maana tofauti na ile ya mzazi (anaye penda mtoto afauru) kupeleka mtoto wake shule ambayo anaambiwa haina walimu,vifaa vya kufundishia,mtoto atakaa chini (hakuna viti vya kutosha) wakati anasoma,hakuna vitabu,maktaba n.k huyu atakua mzazi wa ajabu katika dunia hii.Sasa tujiulize ni muwekezaji  gani toka ndani/nje atatamani kuwekeza nchi haina umeme,maji na mafuta??.
Kipengele cha hakuna serikali (No Government) siamini labda tuseme haijawajibika katika baadhi ya mambo.

13 August, 2011

KUCHEKA NI.....................................???

Matatizo ya umeme na Orijino komedi
                                     

                             Matumizi ya Lugha....kisa cha chips zege (LOL)

12 August, 2011

...............NEW GADDAFI IN TOWN!!!!!!




Gaddafi Chameleone (LOL)
Msanii nguli wa miondoko ya ragga  nchini Uganda bwana  Joseph Mayanja aka Jose Chameleon ambaye pia anajiita dactari wa muziki abadili dini yake Catholic na kua Muislam.Mwanamziki huyu ambaye miaka michache iliyopita alioa na kufunga harusi katika dini ya kikristo na hata kuokoka (SOMA HAPA) amewaacha watu wengi midomo wazi baada ya uamuzi wake huo wa ghafla.
                                    Gaddafi Chameleone akifuatilia maelezo
Leo Ijumaa ya tarehe 12/08/2011 Chameleone ambaye jina lake kwasasa ni Gaddafi Chameleon ameonekana msikiti wa Kibuli akihudhuria swala ya Ijumaa.Hivi Gaddafi ni jina la kiislam?? Anayejua atujulishe!


Zaidi soma HAPA

KWELI USWAHILINI KUNA VITUKO!!!

Dakika ya  0:59
                 1:07
                 1:32
                 2:23
                 3:50

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI VURUGU ZA UK

 Picha mbili za mwanzoni hapa chini waandishi wa habari wamezipa majina ya pekee kabisa kutokana na matangazo ya biashara nyingi hapa UK. Mfano ''Buy now pay later'' yaani nunua sasa ulipe siku nyingine.Aidha katika vurugu zinazo onyesha kupoa zoezi hilo la kuiba vitu limepewa jina la ''Take now don't pay later'' Yaani chukua sasa na usilipe baadae!.Waziri mkuu David Cameron amesema kila aliyehusika na vurugu,wizi na uharibifu ajue watamfikia na atawajibishwa!
Usemi huo hapo juu naufananisha na ule wimbo wa Twanga 'mtaji wa masikini nguvu zake mwenyewe' ambao majambazi  bongo waliwaimbisha abiria wa mabasi/magari yaliyo tekwa huku wakisachiwa walivyo navyo.
   


                                   Magari yaliyo chomwa moto Serikali imeahidi kulipa fidia

                                Duka likiwa limevunjwa kioo,wenye maduka pia watalipwa fidia

                               Aidha uruke toka juu gorofani au ufe kwa moto dada aliona kuruka ni bora
                       
                               Polisi wakiwa wanaangalia kinacho endelea na wananchi wenye hasira kali
 Jamaa wakiwa tayari kwa vurugu na kubeba kinacho bebeka.Kama unavyowanona wameficha sura nchi hii ni moja wapo ya nchi zenye CCTV camera nyingi duniani kwahi ukifanya kosa ni rahisi kukukamata.Lakini hapo CCTV haina ujanja!


Baba wa kijana miongoni mwa wale vijana watatu waliouwawa katika vurugu jijini Birmingham akiongea kwa uchungu kufuatia kifo cha mwanae ambaye inasemekana alikua akiokoa majirani waliokua wamevamiwa katika vurugu hizo hadi mauti yalimpomfika.


Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

11 August, 2011

UKISIKILZA WIMBO PEKE YAKE UTADHANI CHAMELOENE


Fanya kazi
                                                                    Sweet mama

TANZANIA BILA UMEME/MAFUTA INAWEZEKANA??

Ilikua.........................

Heshima ikajengeka mjini na salamu zikatolewa kama hivi.........

Ghafla bin vuuu mara...........
Vidumu ndio mpango duh kweli Bongo Raha! hapo bado adha ya umeme,maji safi,foleni,stress binafsi n.k

Wauza wese nao wataka heshima!! sijui wanataka salamu kama hio ya Tanesco?.Hakika hivyo vituo vya mafuta  vingekua tu huku kwenye vurugu zilizo anza baada ya mtu mmoja tu kuuawa basi zingebaki historia,magofu ama kuchukuliwa mafuta yao kwa nguvu tena bure 'yaani take now don't pay later' kama ambavyo tutaona matukio zaidi yaliyo jiri hapa UK.Watu wamechoka na blah blah wakati maisha magumu.Siombei tufikie huko lakini huenda ndiko tunako elekea bila kujijua. Je viongozi wetu wanaliona hili? au wao haiwahusu? Nauliza tu!

09 August, 2011

VURUGU ZA LONDON ZASAMBAA MIJI MINGINE

Kumezuka vurugu jijini London Uingereza baada ya raia mmoja kupigwa risasi na polisi.Vurugu hizo zilizuka baada ya polisi kuzuia maandamano ya amani na kuhoji kwanini raia Mark Duggan (29) aliuawa na polisi kwa kupigwa risasi? Tukio hilo lilitokea Tottenham Alhamis Tar 04 na Jumamosi ya tarehe 06/08/2011 ndipo vurugu zilipozuka eneo hilo na kusambaa miji kadhaa hapa England.
Mark Duggan,29 wakati wa uhai wake


Hali hiyo ya vurugu imeingia kwa kasi miji mingine kama Birmingham,Liverpool,Manchester na Bristol.Ukiachia mbali huyu jamaa kuwa chanzo maisha magumu,ukosefu wa ajira unaozidi kukua na ubaguzi wa rangi vimetajwa kuchangia vurugu kuungwa mkono kwa kasi.Waziri mkuu David  Cameron aliyekua mapumzikoni Italy amelazimika kurudi kwani hali ni tete.Jana 08/08/2011 Birmingham palikua hapatoshi.

 Jengo limechomwa moto Croydon
 Polisi ambao walizidiwa nguvu wakiwa wanaangalia kinacho endelea kama kideo!
 maduka,magari yalichomwa moto
 Mtaani kulikua kama hivi
Jamaa  wenye mask wakiiba dukani na kuvunja ATM machine na kuiba Pound!
Picha zote toka Aljazeera na BBC
Kwa habari zaidi soma HAPA na HAPA

WANAWAKE WADAIWA KUBAKA WANAUME!!!

Huko kwa Mugabe nchini zimbabwe kuna tuhuma za wanawake kuwabaka wanaume kwa makusudi .Ubakaji huo umedaiwa kukua siku hadi siku kwani kwasasa ni kila wiki lazima mwanaume abakwe!.Mkuu wa polisi jijini  Harare Angeline Guvamombe amesema “  wanawake wanao endesha magari ya kifahari huwapa wanaume lifti na kuwapulizia maji maji usoni yanayowafanya wasinzie na baadae kulazimisha kufanya nao mapenzi'' Kwa mujibu wa  the Herald  wiki mbili zilizo pita wanaume wawili walitekwa na kulazimishwa kufanya nao mapenzi chini ya usimamizi wa bunduki. Wakati katika tukio lingine wanawake watatu walimteka mwanaume wa miaka 30 na kumlazimisha kufanya nae mapenzi kwa siku 5!!.


Cha ajabu tangu ubakaji huo kuanza hakuna mtu amekamatwa kwa kosa hilo na polisi wamesema wanawake hawawezi shitakiwa kubaka kwani sheria ya Zimbabwe haitambui kama mwanamke anaweza mbaka mwanaume na hivyo mwanamke anayebaka anaweza shitakiwa tu kwa kumvamia mwanaume kwa nguvu (assault) na kupata adhabu ndogo ikilinganishwa na ile ya mwanaume kubaka.


Hii ni changamoto katika nyanja ya sheria kwani mabadiriko ya wakati yamebadirisha mfumo wa mahitaji.Je kwetu Tanzania hali ikoje katika maswala haya? Wanasheria tuambieni ili tujue mie nikibakwa nijue kama haki yangu ipo ama laa kwani kwa mpango huu hakika wanaume watakua hatarini kuambukizwa magonjwa ya zinaa bila kupenda!



Kwa habari zaidi soma: HAPA 


07 August, 2011

WALIO MUUA OSAMA NAO WAUWAWA!

Habari zilizojiri ni kwamba Helicopter ya NATO aina ya Chinook iliyobeba kikosi maalum cha wanajeshi wa kimarekani zaidi ya 20 imetunguliwa na kuua watu wote huko Wardak,Afghanistan.Walio kufa katika shambulizi hilo ni pamoja na wale wanao sadikika kufanikisha kumuua Osama Bin Laden .Kundi la waasi la Taliban limekiri kuhusika na mauaji hayo. Wakati huohuo Rais wa Afghanistani  Hamid Karzai ametoa salamu za rambirambi NATO kufuatia ajali iliyo gharimu roho za watu 31 wa kikosi maalum toka Marekani na 7 kutoka Jeshi la nchi hio


            Helicopter iliyotunguliwa na Taliban


Kwa habari zaidi soma HAPA na HAPA

ATI ALIZALIWA NA PHD??


Big up Said Michael umetisha japo nina swali moja tu dogo la msingi.Je haya ndio matumizi halisi ya Phd au ni utani tu?.Kama hio ndio maana yake basi watanzania watakua na maswali mengi sana kwa wasomi walio katika nyadhifa mbalimbali je nini mchango wao kwa serikali na jamii kwa ujumla?

06 August, 2011

EQUALITY BEFORE THE LAW!!!!!!!!!!!?????

Huyu ndio jamaa anaye sadikika kua mwizi aliye vamia Bank CRDB kwa kutumia mawe na kudhibitiwa na Polisi wanaolinda Bank hio kama unavyo waona wakimpa mateke ya uso.Sina hakika huyu anaweza kuwa jambazi anavamia Bank kwa mawe wakati anaona SMG mbele yake.kweli bongo tambarare!!.Kwa akili ambayo haihitaji kwenda darasani kama mlinzi ana SMG basi jambazi angekua na machine gun sio mawe lakini polisi wetu kama kawa nguvu nyingi bila kupima uzito wa tatizo jamaa kadhibitiwa kama unavyoona!! Hii ni usawa wa sheria (Equality before the law) ya pekee kabisa Tanzania huwezi pata namna hii hata ulaya!!

Mateke ya uso ni bora kuliko kichapo cha wananchi wenye hasira kali....

Ati huyu ndio jambazi??!!! Nadhani watanzania wangefurahi kusikia huyu ni fisadi!
Kwa picha na  habari zaidi soma HAPA

05 August, 2011

TUNE OF THE DAY ,,,FEEL FREE BY ALI KIBA


SIJUI TUNAELEKEA WAPI??

Kuangalia safari ya utamaduni wa ajabu  kuelekea kusiko julikana bonyeeee icheze!!!

            Video kwa hisani ya Tanzagiza!


Mimi sijaelewa lengo la hii disco vumbi  kama ni kufurahia au kufundisha utamaduni mpya kwa watoto? Au mimi ndio nimepitwa na fashion kama waosha vinywa wanavyoweza sema? Sidhani kama kuna maadili yoyote hapa by all means! Na hii haihitaji jitihada za serikali peke yake hata watu baki wanaweza kemea

ORIJINO KOMEDI MPOO?? BASI TUJIUNGE!!!!

Ushawahi sikia ule usemi wa unaruka mkojo  halafu unakanyaga...... basi ndio hapa bonyeza icheze!!
Sir Charlie Chaplin alikua balaa katika uchekeshaji.Na hii style sijui kaiga wapi maana mzaha mzaha mtu unaweza jikuta unaliwa  na simba badala ya watu kucheka wataanza kuomboleza.Nisimalize utamu click and watch for yourself hahahaa!!

Mbinu za masumbwi hahahha sina mbavu unaweza dhani ni rahisi kiasi hicho nawewe ujaribu halafu ukatolewa meno ya barazani yote (Don't try this i'm warning you!).Ila nimependa he is stylish and humorous yaani mbavu zangu hapa zinauma!

04 August, 2011

Professor Jay - Kama Ipo (Video)


TUSIFIKIE TU HATUA HII .....ha ha haa !!!

Kufuatia sakata la kufukuzwa wabunge  toka mjengoni katuni hapa chini imenifurahisha sana kwa namna ujumbe ulivyofikishwa.Sasa tukifikia hatua kama hii sipati picha Bunge litakuwaje.Nadhani mchora katuni  ameonyesha  dawa ya uonevu ipo jikoni ipo siku utapatiwa suluhu ya namna hio ama inayoendana ili kwenda sawa ama kukomesha hali hio kabisa.Tujiunge ha ha haaaa!!! yani sina mbavu.Hongera Abdul




                                      Kesho kutwa!!!!?

Sasa hii ya hapa chini sijui wanamfurahisha nani? Kama bajeti haifai kwanini uipitishe? Huyu ndio mwakilishi wa mpiga kura!! Je tuseme wabunge wa namna hii hawajui majukumu yao bungeni?? Nadhani wabunge wa namna hii ndio wafukuzwe bungeni hawana faida na mwisho wataishia kulala tu wakati mjadala ukiendelea!
                          Kuna mwenye majibu swali ndio hilo, sema usikike!

HOSNI MUBARAK KUVUNA ALICHOPANDA!


Aliyekua Rais wa Misri (Egypt) Hosni Mubarak-83 ambaye alijiuzulu kufuatia maandamano makubwa kufuatia tuhuma za rushwa na uongozi wa mabavu.Mnamo April,2011 aliwekwa chini ya ulinzi bila kujali afya yake iliyozorota na jana (Jumatano Agasti 03,2011)  pamoja na hali yake kiafya kuyumba alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya rushwa iliyo kithiri,kuua waandamanaji jitihada ambazo hazikuzaa matunda mpaka alipo achia ngazi mwezi Januari 2011. Wakati huo huo hali ya Misri bado tete kutokana mvurugano uliopo kati ya serikali ya sasa na waombolezaji ambao walizuiwa kuandamana ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha katika harakati za kumtoa Mubarak


Mubarak pamoja na mwanaye wamekana mashataka dhidi ya Rushwa na mauaji ya waandamanaji na kwa sasa waandamanaji wameahidi kutulia wakisubiri hukumu itolewe kwa Mubarak na vibaraka wake.Japo waliofika mahakamani waliweza wafukuza polisi kwa mawe. HII NI CHANGAMOTO KWA SERIKALI ZETU KATIKA UWAJIBIKAJI NA MATUMIZI YA NGUVU WANAPOWAKOSEA WANANCHI (WAPIGA KURA),KASHFA ZA RUSHWA NA UWAJIBISHWAJI.


Kwa habari zaidi soma HAPA,HAPA,HAPA na HAPA