18 February, 2011

Uchaguzi mkuu Uganda kufanyika leo..


Yoweri Museveni
VS
Dr Kizza Besigye


Leo ndio siku ya uchaguzi mkuu nchini Uganda.Mpaka mwisho wa kampeni za uchaguzi huo ambao una wagombea 8 kiti cha urais imeonyesha hali ya wasiwasi kwamba kuna uwezekano mkubwa kutokea machafuko ya kisiasa kutokana na mvutano mkubwa uliopo kati ya Museveni na Dr Kizza Besigye.Pia kuna taarifa kuwa police wengi wame ajiriwa kipindi hiki kuhofia machafuko (AfricanNews.com)

Besigye amesema atakubali matokeo ikiwa tu uchaguzi utafanyika kwa uhuru na haki na si vinginevyo.Hata hivyo mkuu wa majeshi nchini Uganda ametangaza kuwa hata vumilia hali yoyote ya vurugu katika uchaguzi huo unaotegemea kufanyika mapema leo.

Habari zaidi zinasema Muveni akishinda atakua ametoa historia ya aina yake kuongoza kwa miaka mingi (30) tangu uhuru wa nchi hio ambapo kwa Africa mashariki ukitoa Mfalme wa iliyokua Buganda (Uganda kwa sasa) Kabaka Daudi Chwa alie ongoza miaka 42(1897-1939), na Emperor Haile Selassie aliyeongoza miaka 44 (1930-1974) mpaka alipo pinduliwa na kuuwawa.Nyerere na Moi waliongoza miaka 24 tu
(Daily Monitor)

Jeshi litatoa taarifa kamili kuhusu Mabomu-JK

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete alonga na na vyombo vya habari na kusisitiza kuwa taarifa kamili ya mlipuko wa mabomu Gongo la mboto ni jeshi tu ndio litatoa taarifa kamili na ''SIO RADIO MBAO'' ikiwa ni pamoja na taarifa itakayo tolewa baada ya kukutana na baraza la usalama wa Taifa.Mimi sijaelewa tu Radio mbao ndo zipi, kuna anayejua anisaidie?wakati nasubiri msaada huo...TUJIUNGE!