21 June, 2010

Kazi kweli kweli...

Kufuatia maandalizi ya kombe la Dunia ambalo kwa sasa limepamba moto na timu za Kiafrica kuendelea kuadabishwa huko kwa mzee madiba/South Africa.Kuna habari kwamba maandalizi hayo yali enda sambamba na kung'arisha jiji la Cape Town kwa kuhamisha masikini wote kwenda sehemu nyingine kwa kile kilicho daiwa kuweka mji safi 'wageni/waheshimiwa wanakuja!.

Hio imesemekana kutokea ili kujenga taswira nzuri ya mazingira kwa kuzingatia ujio wa kombe la dunia ambalo South Africa ndio wenyeji.Kutokana tukio hilo maalum kabisa na kuzingatia ujio wa mastaa/matajiri/viongozi mbalimbali duniani, wenyeji hao wamelazimika 'kung'arisha mji'.

Habari zinasema kiini macho hicho ni kwajili ya kufanya wageni watambue kua nchi hio imeendelea na haina matatizo makubwa ya umasikini kwa kuficha masikini wote walio kua wakiishi karibu na uwanja ambako mashindano ya kombe la dunia yana fanyika/endelelea hivi sasa.Hii haina tofauti na ile ya kujenga barabara vizuri mara tu kiongozi mashughuli akiwa anatembelea eneo fulani, ni kiini macho cha kawaida kwa nchi nyingi za Africa.

Soma zaidi hapa http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2010/06/10/AR2010061002060.html.