17 February, 2011

Maafa Mlipuko wa Mabomu Gongo la Mboto

Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirishwa leo mpaka kesho kufuatia taarifa ya kulipuka mabomu.Waziri mkuu Mh Mizengo Pinda ametoa taarifa bungeni,takribani watu 19 wamepoteza maisha mlipuko wa mabomu kambi ya JWTZ Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.Idadi hiyo inaweza ongezeka

Habari zaidi zinasema kuwa kambi ya Gongo la mboto ndio inayo hifadhi silaha nzito za kijeshi kwahio madhara ya mlipuko wa mabomu hayo huenda ikawa kubwa zaidi ya ile ya April 2009 kambi ya Mbagala


Nyumba iliyo dhurika kwa bomu
(Picha kwa hisani ya The Habari.com)


bomu katika makazi ya watu (Star Tv)


Darasa lililo bomolewa na bomu Pugu sec (Star Tv)


Kipande cha bomu kilichotua mtaani


msururu wa watu wakijaribu kuokoa roho zao

Rijaki blog inatoa pole kwa waathirika wa mlipuko huo wa mabomu Gongolamboto,ndugu,jamaa, marafiki na Mungu azilaze mahala pema peponi roho za walio tangulia mbele ya haki katika tukio hilo.

Sijaelewa hii Lugha..