30 April, 2010

Sitaacha kusema hii....

Niseme tu mwenye kupata habari kama hizi ajaribu kuwapa na ndugu jamaa na marafiki kwani wanao ibiwa kwa mtindo huu ni wengi japo ni kimya kimya,trust me watu hawasemi kama wameibiwa.Mimi kabla sijawa mtaalamu wa internet nimewahi shuhudia watu kama watatu hivi ambao waliibiwa na wadanganyifu wa aina hii na nilijua kwani ni watu wangu wa karibu vinginevyo nisinge jua watu hawasemi haya mambo!. Kwahio namaanisha kutoa habari za aina hii ili mtu akija kuibiwa kwa style hii unless alikua hajui ila kama kapuuzia hakuna lawama, Nadhani nimeeleweka, kwahio ukiona hii jua ni wizi mtupu kwani hujashiriki LOTTERY/bahati nasibu yoyote jiulize kwanini uipate tufrom no where? hii ni kukuvuta tu ujione umenahatika na kwakua baadhi yetu tunapenda short cut katika kutafuta maisha unajikuta umeingia kwenye utapeli wa aina hii. Kama nilivyosema post zilizo pita huu utapeli unakuja kwa namna mbali mbali kwahio kua makini.Tujiunge....


The National Lottery Winner
Customer Service
PO Box 227
W10 CRUMA ROAD
BURKINA FASO.

Dear Lucky Winner
The Board of Directors, members of staff and the International Awareness Promotion Department of the BURKINA FASO National Lottery, wishes to congratulate you on your success as one of our FIVE (5) STAR PRIZE WINNER in this new years' National Lottery promotion draw held here in Burina Faso.

We are pleased to inform you that your email address has won you a consolation cash prize of 950, 000 Euro (Nine Hundred and fifty thousand euro) credited to file NL/209463-7644. We found your e-mail from an exclusive list of 52,000 e-mail addresses of individual and corporate bodies picked by an advanced automated random computer search from the internet for the e-mail ballot promotion organized for the (ECONOMY CRISES) by the National Lottery to support individuals from different part of the globe, no tickets were sold but all email addresses were assigned to different ticket numbers for representation and privacy. After this automated computer ballot, your e-mail address emerged as one of the lucky winners in the category "A".
How to claim your winning, send your information.

These are your Winning Information and Identification Numbers:
Batch Number........................ .... 123/08/09474
Winning Numbers...................... 02,07,19,24,35
Reference Number..................... YLINC/09697809
Payment No............................ .... YML27536
NAMES.....................................
ADDRESS: 3.............................
SEX.........................................
AGE.........................................
COUNTRY................................
OCCUPATION/POSITION.........
TELEPHONE NO......................
COMPANY...............................
EMAIL ADDRESS....................
Yours Sincerely,


DR WILLIAMS DUKE
Mega Millions Payment Officer.
TEL: +226 75743540

Endeavour to email your event manager the following information above including your file number (UKNL/20511465463-7644) for immediate processing, verification and legalization of claims in order for payment to be made to you as required, in accordance with our payout policy.
Congratulations once more from our members of staff.
Yours Sincerely,

Dr Williams Duke
Best Regard

(NB: Huu ni wizi mitandaoni usijibu chochote ifute tu)

26 April, 2010

Haibiwi mtu....

Nimepata hii email kutoka kwa my best friend ambaye anaishi Tanzania lakini si yeye ndiye alietuma. Hii inamaana kuna mtu anatumia account yake kutumia watu email kama hivi ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Nina uhakika watu wengi sana watakua wamepata emails za mtindo huu.Ni scam tu kwa hio unless stated otherwise email za hivi ni wizi pia, mjulishe na mwenzio ukipata ujumbe kama huu

Am sorry i didn't inform you about my urgent trip to London, i don't have much time on the PC here,so i have to brief you my present situation which requires your urgent response actually,

I had a trip to London but unfortunately for me all my money got stolen at the hotel where i lodged due to a robbery incident that happened in the hotel.I had been so restless since last night because i have been without any money moreover the Hotel's telephone lines here got disconnected by the robbers and they are trying to get them fixed back i have access to only emails at the library because my mobile cant work here so i didn't bring it along,please i want you to help me with money so please can you send me 850 Pounds or any amount you can afford so when i return back i would refund it back to you as soon as i get home,Am so confused right now and don't know what to do,

I had been to the embassy and they are currently looking into my case,Please send the money through Western Union Money Transfer so i will get it immediately its sent,i want you to please transfer the money as soon as possible.Here is the details you need for the transfer below,

Receivers Names: (Jina kapuni)
Receivers Address: 328 Mile End Road
City- London
Country- UK
Zip Code- E1 4NS

Please get back to me as soon as you have the money sent,once you are done with the transfer just help me to scan a copy of the receipt given to you by Western Union or help me to write out the Money Transfer Control Number(MTCN)

I will be waiting for your help. Thank you so much

Best Regards,
(Jina kapuni).

Wizi mtupu......

Kama ilivyo ada nimekua nikitoa hapa taarifa mbalimbali kuhusiana na na wizi wa habari mitandaoni. Ifuatayo ni moja kati ya emails ambazo zinalenga kuendeleza wizi wa taarifa zako unazotumia kufungua email account yako.Unaweza shangaa kwanini taarifa za namna hii ni nyingi humu kwenye blog lakini kwa kuzingatia umuhimu wa watumiaji wa internet popote pale walipo nimekua interested kutoa taarifa za hivi kwa sababu sio wote wanajua huu ni udanganyifu ulio kithiri mtandaoni.Kwahio basi ukipata email ya namna hii wewe ifute endelea na shughuli zako wala usihangaike kwa lolote.Chini hapa ni email yanyewe ninayo zungumzia na ni vizuri kutambua email za hivi zinakuja kwa mifumo tofauti lakini ujumbe unaweza kua ule ule ama ukawa na tofauti kidogo lakini lengo ni moja tu kupata habari zako watakazo tumia watakavyo hawa hackers.

Dear User,

We are sorry to inform you that we are currently working on securing our
server, during this process accounts which are not manually verified by us
will be deleted, Please confirm and submit your information for manual
verification by one of our customer care.

Information which is to be provided is below:
User Name:
User Id:
Password:
Date Of Birth:
Country (At Sign up):

Upon confirmation of information from you, we will manually verify your
Yahoo! Account and reserve it from being deleted, we are sorry for any
inconveniences this might have caused providing your information over the
email.

Warning!!! Account owner that refuses to update his/her account after two
weeks of receiving this warning will lose his or her account permanently.
______________________________________________________________________________

Copyright © 2010 Yahoo! Inc. All rights reserved. Copyright/IP Policy
Terms of Service Guide to Online Security

NOTICE: We collect personal information on this site.

To learn more about how we use your information, see our Privacy Policy

23 April, 2010

Tuna kwenda sawa.....

Twende sawa yani pasu kwa pasu wewe chukua watoto mie nachukua dolari hehehehe kazi kweli kweli. Sasa sijui dolari hizi bata atapeleka wapi? mmmh!

22 April, 2010

your life is no longer beautiful..kanya boya please be informed!

Kama nilivyokua nikisema mara kwa mara kuhusu wizi wa taarifa zetu mbalimbali mitandaoni na hawa HACKERS ambao inasemekana wana fikiri 5 Minutes ahead of any ordinary computer (PC)/Internet user. Nimepata hii taarifa dakika chache zilizopita toka kwa rafiki yangu Deo Shakiula toka Mwanza Tanzania. Nashukuru sana mkuu.

Kanya boya yenyewe inaenda kama ilivyo hapa chini, mjulishe na mwenzio

This information arrived this morning, Direct from both Microsoft and Norton. Please send it to everybody you know who has access to the Internet..
IF A PERSON NAMED SIMON ASHTON ( SIMON25@HOTMAIL.CO.UK ) CONTACTS YOU
THROUGH EMAIL DON'T OPEN THE MESSAGE. DELETE IT BECAUSE HE IS A HACKER!!

TELL EVERYONE ON YOUR LIST BECAUSE IF SOMEBODY ON YOUR LIST ADDS HIM THEN YOU WILL GET HIM ON YOUR LIST. HE WILL FIGURE OUT YOUR ID, COMPUTER ADDRESS, SO COPY AND PASTE THIS MESSAGE TO EVERYONE EVEN IF YOU DON'T CARE ABOUT THEM AND FAST BECAUSE IF HE HACKS THEIR EMAIL HE HACKS YOUR MAIL TOO!!!!!

Anyone using internet mail such as Yahoo, Hotmail, AOL and so on is at risk. You may receive an apparently harmless e-mail titled, 'Mail Server
Report.'

If you open the file, a message will appear on your screen saying:
'It is too late now, your life is no longer beautiful.'

Subsequently you will LOSE EVERYTHING IN YOUR PC,
and this person will gain access to your name, e-mail and password.

This is a new virus which started to circulate on Saturday 6/3/10 afternoon.
AOL has already confirmed the severity, and the anti virus softwares are not capable of destroying it .

The virus has been created by a hacker who calls himself 'life owner'.

PLEASE SEND A COPY OF THIS E-MAIL TO ALL YOUR FRIENDS, And ask them to PASS IT ON IMMEDIATELY

Man u iko juu kama kawa!!

(Image from desktoprating.com)

A.K.A mashetani wekundu maarufu kama man u wazidi kung’ara. Ripoti ilotolewa na Eurosport Thu, 22 Apr 10:28:00 2010 kwa hisani ya Forbes inaonyesha Manchester United kua ni club ya kwanza yenye thamani kubwa kimichezo kwa thamani ya takribani £ 1.2 Billion na kuipita NFL the Dallas cowboys ya marekani yenye thamani ya £1.072 billion. Club inayofuata kwa utajiri kimichezo ni baseball's number one club the New York Yankees yenye thamani ya takribani £1.040 billion. Wakati huo huo ripoti hio katika Nyanja ya soka imeonyesha Man u kua ya kwanza na kufuatia na Real Madrid kwa thamani ya takribani £ 859 Million na watunza silaha maarufu kama Asernal kushika nafasi ya tatu kwa thamani ya £ 767 Million; Barca nafasi ya 4 kwa thamani ya £ 650 Million (but debt free club) unaweza malizia kwa kuangalia top 20 hapa chini.

Rank ---- Team ---- Country ---- Value
1 ---- Manchester United ---- England ---- £1,192m
2 ---- Real Madrid ----Spain ---- £859m
3 ---- Arsenal ---- England ---- £767m
4 ---- Barcelona ---- Spain ---- £650m
5 ---- Bayern Munich ---- Germany ---- £643m
6 ---- Liverpool ---- England ---- £534m
7 ---- AC Milan ---- Italy ---- £520m
8 ---- Juventus ---- Italy ---- £426m
9 ---- Chelsea ---- England ---- £420m
10 ---- Internazionale ---- Italy ---- £268m
11 ---- Schalke ---- Germany ---- £249m
12 ---- Tottenham Hotspur ---- England ---- £242m
13 ---- Lyon ---- France ---- £216m
14 ---- Hamburg ---- Germany ---- £214m
15 ---- Roma ---- Italy ---- £200m
16 ---- Werder Bremen ---- Germany ---- £178m
17 ---- Marseille ---- France ---- £170m
18 ---- Borussia Dortmund ---- Germany ---- £170m
19 ---- Manchester City ---- England ---- £168m
20 ---- Newcastle United ---- England ---- £129m
-------------------------------------------------------------------------------------
(Source:Eurosport)
Read more:- http://uk.eurosport.yahoo.com/22042010/58/premier-league-united-named-world-most-valuable-club.html

Ukisikia customer kero...

(picha toka wavuti.com)
Customer care ama customer kero? Hehehe nadhani ifike wakati sekta ya umma na mashirika yake bila kusahau sekta binafsi yaangalie utendaji kazi wa customer care zao ili zisiwe customer kero kama ilivyo kwenye cartoon. Kuangalia utendaji wake wa kazi ni pamoja nakuangalia namna mteja anaweza pewa huduma bila adha yoyote kuanzia kumpata mtoa huduma mpaka huduma yenyewe. Nadhani hili ni tatizo hata nchi zilizo endelea kwa baadhi ya makampuni na mashirika. Mfano makampuni yanayotoa huduma za internet na simu. Utakuta wameweka namba ya simu mathalani ya maulizo,mauzo n.k.


Tatizo liko hapa ukipiga hio namba unaanza kupewa matangazo kwanza then options kibao hufuata mfano: umepiga hio huduma kwa wateja/customer care unaambiwa ukitaka kuongea na technical advisor press 1,financial advisor press 2 reporting new fault press 3, reporting existing fault press 4 n.k. ukisha press hio unapewa options nyingine mfano: reporting existing fault una press 4, unapata hii if you need updates on the fault reported press 1, (unapewa na hii:- you only need to call if the solution given does not seem to sort you out…….we know you are call is very important to us and one of our advisor will be happy to help you time zinaenda hivo na mziki umewekewa), nyingine: to get updates over 1 week or so press 2, updates over 3weeks and mind you hapa hela yako inakwenda kwa speed ya ajabu and yet they are telling us hio call ni free haina charge wakati salio linaisha.


Na hapo they keep us waiting hivo usikute mpokea simu mwenyewe ndio yupo kwenye michapo isiyo husiana na kazi kama hio hapo weekend wapi, lile buzi umefanikiwa lichuna? Vipi Yule demu anaeleweka mzeya ama miyeyusho? Muda wa kazi huo na simu inaita jamaa ndio anaongea mambo hayo. Yani wizi mtupu saa nyingine mtu unajiuliza sasa hio customer care wameweka ya nini au ndio tuseme customer kero??? Naamini kila ofisi ina mwongozo na ethics za kazi kwa ujumla sasa kwanini watu wawe na tabia kama hizo?? Hata kama kampuni ni ya baba mtu afanye kazi inayotakiwa sio kuleta mapozi yasio na maana.Wahusika kwa namna yeyote katika hili tubadirike vinginevyo kama ni biashara basi itakosa wateja! .

20 April, 2010

Kwa scholarships zaidi tembelea hapa!

Kwa wale wenzetu wanaotafuta scholarships mbali mbali basi mnaweza kupitia site hii (nitaiweka hapo chini baada ya maelezo haya) kwa scholarships zaidi. Na kama utaona ipo ambayo unaitaka fanya application haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia masharti yaliyowekwa ili uwe na nafasi kubwa kuipata. Nasema hivyo kwasababu watu wanao hitaji scholarship ni wengi sana kwahio ni vema kufuata masharti na kuzingatia muda ulio wekwa kwa waombaji ili kujiweka katika nafasi kubwa kupata.
------------------------------------------------------------------------------------
Link ni hii hapa, kazi kwenu!! ukiiona hii mjulishe na mwenzio
http://www.wavuti.com/scholarships.html
Hii website ipo pia katika blog kwenye kipendele ''MITANDAO MBALI MBALI KWA JINA ''NUKTA77'' aidha kuna SCHOLARSHIPS hapo hapo kwa juu yake zipitieni pia pengine unaweza pata unayotaka.Pia msisahau kupitia www.makulilo.blogspot.com kwa scholarship zaidi.

19 April, 2010

Anataka mara 10 kwa siku!!!!

Maajabu yaliyotokana na wii fit , hii ni video game ilo tengenezwa na Nintendo maalumu kwa kufanyia mazoezi kwa kufuatiza video. Mwanamke mmoja yamempata baada ya kuanguka akiwa anafanya mazoezi kutumia hio wii fit video game na kuumia mshipa ambao kwa mujibu wa daktari wake mwanamke huyo atakua na misisimko ya mapenzi isiyo isha. Kwahio sasahivi mwanamke huyu ataka apewe mara 10 kwa siku.Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 aishie jijini manchester amekaririwa akisema kuanguka kwake kumempelekea awe mpenda ngono kupita kawaida na anataka afanye angalau mara 10 kwa siku na anaamini ipo siku atapata mwanaume mwenye uwezo huo …lol sijui kama yupo 10x a day????!! duuuh. Habari zaidi zinasema mitetemo kama ya simu, mashine ya kuosha na mingine humfanya huyo dada asisimke na kua tayari kabisa kwa tendo la ndoa.

Hata hivyo waosha vinywa hawakubaki nyuma, wamesikika wakisema lazima wawanunulie mashine ya aina hio wapenzi wao ili nao wawe wanapenda ngono kama huyo dada….sina hakika kama wanauwezo huo wa mara kumi kwa siku kama sio kua wateja wa viagra hehehe kazi kweli kweli.Aidha madai ya watu kuumia kupitia wii fit hapa UK mengi yame postiwa youtube. Kwahio watumiaji wa wii fit wameshauriwa kua makini na matumizi ya hio video game kuepuka madhara mbalimbali yanayo weza hatarisha afya zao.inaonyesha wii fit ina watumiaji wengi sana. Wii fit is an exercise game ambayo imeshika nafasi ya pili kimauzo katika Video games in history).
--------------------------------------------------------------------------------------------------

Kwa habari zaidi soma hapa: http://www.postchronicle.com/news/original/article_212295798.shtml

Kanya boya zaidi mitandaoni...

Wed, 7 April, 2010 15:17:45
DEAR FRIEND,I NEED YOUR ASSISTANCE.
From: Dr Maiga
To: . <.@yahoo.com>


--------------------------------------------------------------------------------


Greetings From Dr David Maiga

Dear Friend,
I am Dr David Maiga the manager auditing and accounting department African Development Bank.(ADB) Ouagadougou Burkina-faso in West Africa.For your kind attention,I will be very glad if you do assist me to relocate this sum of ($26.5M US dollars) to your account for the benefit of our both families.I discovered unclaimed sum of $26.5m US dollars in our bank which belonged to one of our late foreign customer who died with his entire family in Kenya plane crash on July 2003.

This is a genuine business,only that I cannot operate it alone without using a Foreigner who will stand as a beneficiary to the fund.The request of a foreigner as next of kin and beneficiary of the fund is because the foreigner will stand as next of kin to the deceased,that is why I decided to contact you in a good manner to assist me and also to share the benefit together with me.

The banking law and guideline here stipulates that if such money remained unclaimed after seven years,the money will be transferred into the bank treasury as unclaimed fund.You will be entitled to 40 % of this money as foreign partner,since you provide an account for the claim,5 % will be set aside for expenses incurred during the business and 55 % will be for me.There after I will visit your country for disbursement and sharing of the fund according to the percentages indicated if agreed.

By indicating your interest all other necessary vital information will be send to you on how the business will be executed.Please keep this proposal as a top secret and delete it,if you are not interested.

Now my questions are:
1) Can you handle this project?

Please let us get this fund transfer into your account.I look forward to receive your reply as soon as you receive this email.

All the best to you from,
Dr David Maiga.

NB: Sijawahi sikia mtu anataka msaada wa kutumia akaunti ya mtu mwingine zaidi ya hizi za wizi ulio enea mitandaoni, kaeni chonjo wadau. Wizi kama huu umeenea sana mitandaoni kwa style mbali mbali kwahio ukipata e-mail ambayo imekaa kipesa pesa basi ujue umetegwa na kama hutakua makini utaibiwa, watu wengi washaibiwa sana na watu wa design hii.

17 April, 2010

HATER vs UKWELI.....????!!!

Kutokana na kwamba mada ilopita ilikua inahusu maana ya HATER sitatoa tena maana ya neno hilo hapa.Nimekua nikipitia vyanzo vya habari mbali mbali kuhusiana na ma-celebrity wetu ( watanzania), raia wa kawaida hata viongozi pia nje na ndani ya Tanzania. Nimekua nashindwa kupata maana halisi ya HATER hasa pale mtu akisema ukweli ama kinyume kuhusu mtu mwingine ambaye kafanya kitu kwa maendeleo yake binafsi. Pamoja na hayo kuna watu wanawasema watu wengine bila kua na chanzo sahihi ama ukweli wa jambo wanalo ongelea sasa sijui hawa wanaingia kundi gani?.

Mimi kuna siku nimekutana na mtu (jina kapuni) akimuongelea celebrity mmoja wakibongo (Mwana Falsafa ama Mwana FA) eti yuko HARVARD UNIVERSITY (USA) anasoma huko masters. Nikamuuliza kama habari kapata wapi akajibu mie huyo celebrity ni rafiki yangu kaniambia mwenyewe!!! Nikamuuliza anasoma nini huko Harvard? Akajibu sijui ila ni masters degree. Nikamwambia mie huyo celeb.. unaye msema nipo naye Chuo kimoja UK ila tuko kozi tofauti na pia anaishi mji mmoja na mimi. Kabla sijamalizia kuongea nikaitwa labda kama mimi ni HATER ila jamaa anasoma states. Sasa ndio nashindwa kuelewa maana ya HATER ni ipi yaani ni Yule anayesema ukweli ama anaye danganya ama msingizia mtu???!! Na kwanini mtu ukomalie kitu usichojua ukweli halisi??

Ok! Kama nilivyosema katika pita pita vyombo mbali mbali vya habari mtandaoni nikakutana na mtandao wa ma-celebrity mtu yule yule kasemwa kwamba yuko UK anasoma masters. Wakati huo huo kuna watu wakasema ni uwongo UK hasomi kwa sababu kozi anayodhaniwa kuisoma haipo katika hicho chuo. Kama haitoshi wakaendelea kudai kwamba kasoma na kumaliza kwa certificate level pale IFM. Pamoja na kwamba haiwahusu ila wamefatiliana kupata taarifa isiyo sahihi na kwa vigezo wanavyo vijua wao wakalalama kapata CERTIFICATE tu how comes asome Masters?? Kutokana na mjadala huo mkali waungwana wakasema sio CERTIFICATE bali ni Adavanced Diploma ndio maana kapata nafasi ya kusoma COVENTRY UNIVERSITY hapa UK.

Sasa sijui hawa ambao hawakua na habari sahihi kuhusu Mwana FA tuwaitaje? Maana sina hakika kama hawakutaka jamaa asome ama vipi? ivi kwanini mtu uongee vitu kwa msisitizo wakati huna FACTS? Na asingesoma wangefurahi ama kununa na inawahusu nini? Na zaidi ya hapo wanadai kama kasoma basi wanataka ona japo picha za mahafali dahh!!. Sina hakika hata kama wanajua mahafali ni lini? Pamoja na hayo mtu kumaliza chuo sio kufikia mahafali kwa sababu mbali mbali mfano:kushindwa kuhudhuria siku ya tukio,matokeo yasio ridhisha (Failed Report/dissertation), kuto maliza kulipa ada na mengine.

ANGALIZO…. Sina maana moja ya haya yana mhusu muhusika…!!! Sasa sijui kama wasipo ona hizo picha atakua hajasoma ama ni vipi duh!! wali mwengu bana!!

Hali kadharika neno HATER limekua maarufu kwa raia tu na hata viongozi. Mtu akifanya jambo la mafanikio katika maisha yake waosha vinywa hua hawakosi jambo liwe la kujenga ama kubomoa.Mfano: kuna watu kadhaa, nitatoa mfano mmoja, mtu mmoja katika kijiji chetu ambako miaka ya mwishoni mwaka 1980 nyumba za bati zilikua za kuhesabu. Sasa huyo jamaa alikua anataka jenga nyumba ya bati alichofanya ni kujenga mpaka akamaliza ndipo akaenda kununua bati bila hata kuchukua vipimo vya nyumba yake kwa madai WANAOTENGENEZA BATI WANAJUA SIZE YA NYUMBA ZOTE IKIWEMO YAKE KWAKUA YEYE NI FUNDI KUJENGA KWAHIO HANA HAJA KUPIMA JAPO ALISHAURIWA AKABISHA NA KUTAKA KUPIGANA NA KUSEMA ‘’HATERS WANANIZONGA KISA NAJENGA NYUMBA YA BATI’’….Mbaya zaidi mambo ya shop with confidence maarufu kama mali iliyo nunuliwa yaweza rudishwa hayakuwepo ama hayapo tofauti na huku UK ambako mtu una shop with full confidence!! wakati huo huo sisi mambo haya Africa ni nadra sana sana ipo MALI ILIYO NUNULIWA HAIRUDISHWI!!

Sasa kwa huyu jamaa na umbali wa sehemu duka lilipo pamoja na gharama za usafiri ilikua ni karibia nusu ya gharama ya bati zote bila kusahau MALI ILIYONUNULIWA HAIRUDISHWI kwa maana hio alishanunua mbuzi kwenye gunia ni zake hana kwakuzipeleka!. Ikafika siku ya kuezeka kuweka bati hazitoshi ni fupi akitaka zitoshe basi apige paa iliyo flat juu na ndivyo alifanya na kuhamia kabisa katika hiyo nyumba kwa shangwe na mbwe zote eti mvua imkome hanyeshewi tena hehehhe!! in 3 weeks time zile bati ziliondolewa na upepo na kubomoa sehemu kubwa ya nyumba! Wale walioambiwa HATERS ndio ilikua kimbilio…sasa mimi bado sielewi maana halisi ya HATER ni nini, je ni yule anayesema ukweli ama mwongo???? Mnisaidie maana ya HATER please!!

Tukija kwa upande wa siasa na uongozi kila mara twasikia Fulani kala rushwa mtu akiinua mdomo kusema basi ni HATER maarufu kama ‘’MTU MWENYE CHUKI BINAFSI AMA ZA KISIASA’’ Hii ipo pia kwa watu wa kawaida mfano mtu ununue gari basi ukipita mtu utaambiwa unaringa na kama haitoshi inaweza jengwa nyumba barabara unayopita ili ukose kwa kupita na gari lako sasa sijui hapa ni HATER ni yupi?

AU unakuta mtu kanunua mziki mkubwa kama ule wa club kaweka ndani halafu anapiga sauti ya juu tena usiku watu wamelala akiambiwa apunguze anasema HATERS wameanza majungu wanaona wivu sasa wanataka nikasikilizie wapi mziki wangu kwani na wao si wakanunue? Sasa hapa HATER ni yupi kati anaye nyima usingizi watu na anaye sema punguza sauti? Msanii akiambiwa track yake mbovu atasema aliyesema hivo ni HATER tena hawa ndo kabisa wanapenda kusifiwa tu sio kupondwa ama kukosolewa, japo wapo wanaoponda kwa maana ya kua HATER lakini wapo ambao wanakosoa kwa maana yakutaka mtu ajirekebishe Ivi HATER ni nani?......visa vya ma-HATER ni vingi hata wewe msomaji wangu wavijua waweza endeleza kuandika tujumuike wote hapa ila twambie HATER ni nani ok? hehehehe!

Well, nijuavyo mimi ni kweli jamaa kasoma COVENTRY UNIVERSITY kuanzia mwanzoni mwa 2009 na kumaliza mwanzoni mwa mwaka 2010. Na ratiba ya mahafali iko hivi kwa wenye kozi ya mwaka mmoja ( Masters): wale walioanza masomo mwanzoni mwa mwaka watamaliza mwanzoni mwa mwaka kwa mwana unaofata mfano: January na February Mahafali ni July, hali kadharika walio anza September intake wanamaliza September mwaka ujao na mahafali yao ni November ya mwaka huo Mfano:kuanza September 2009, kumaliza September 2010 na mahafali November 2010 yaani miezi miwili baada ya kukusanya dissertation yako ama kumaliza chuo kwa maana ya kumaliza kazi za chuo zinazo kamilisha degree yako.

Pamoja na mambo mengine, COVENTRY UNIVERSITY ni moja wapo ya vyuo vya bei rahisi ukilinganisha na vyuo vingine hapa UK pande za WEST MIDLANDS. Na kimekua kikipata umaarufu mwaka hadi mwaka kutokana na kuchukua wanafunzi wengi toka Africa wakiongozwa na Africa magharibi, Africa mashariki ikifuata, Africa kusini, Africa ya kati na kaskazini zikimalizia na hii yote ni kutokana na urahisi wa ada,maisha na usalama katika hili jiji la COVENTRY. Na kwa wale wenzetu wanaojua UK ni London basi si haba Coventry University wana Branch huko pia japo sina hakika kama ADA kwa London itakua sawa na ya Coventry ambayo ndio main campus.

Wakusoma karibuni ulaya ila uwe na moyo wa kipiganaji usiunge tu tela eti ''Naenda ulaya''!!!!huo ndo ukweli wa mambo, nikipata muda nitaleta''maisha halisi ya ulaya'' kaa mkao wa kula. Kwa leo naishia hapa, much love to you all by rijaki

T.I.D Live in Coventry usiku huu...



Picha kutoka Michuzi Blog!

Kwa wale tunapenda kuonyesha/kujenga heshima bar basi hii ndio siku murua kabisa paleeeee PALMS BAR ambako Top In Dar (TID) atakua anawasha moto ya kitanzania.Kwakua mwaka huu party sio nyingi basi hii itakua mwake na ni weekend pia kwahio si vibaya wau kwenda kubanjuka na kutoa stress za wiki nzima maana hii nchi kama hupo makini unakua chizi bila kujijua...too much stress lol. Haya tukaruke ruke ruke huko stress zipungue

I hope ma-song atayo piga hili la ''Nyota yako'' halita kosa hehehehe, maana hili songi hata kwenye party watu hua makoti yapo viunoni...yani ni viuno kwenda mbele.cheza kidogo basi hiyo hapo.... japo napata hii sijui nani kaiiba toka EATV wapi Video orijino?? duh wabongo kwa kudesa mpaka video? lol cheza nayo hivo hivo maana inasikika tu vizuri. Mimi namtakia kila lakheri na makamuzi mazuri mtu mzima TID...

13 April, 2010

Who is a Hater?

Haters By Maya Angelou
A hater is someone who is jealous and envious and spends all their
time trying to make you look small so they can look tall.
They are very negative people to say the least. Nothing is ever
good enough!

When you make your mark, you will always attract some haters...

That's why you have to be careful with whom you share your
blessings and your dreams, because some folk can't handle seeing
you blessed...

It's dangerous to be like somebody else... If God wanted you to be
like somebody else, He would have given you what He gave them! Right?

You never know what people have gone through to get what they
have...

The problem I have with haters is that they see my glory, but they
don't know my story...

If the grass looks greener on the other side of the fence, you
can rest assured that the water bill is higher there too!

We've all got some haters among us!

Some people envy you because you can:
a) Have a relationship with God
b) Light up a room when you walk in
c) Start your own business
d) Tell a man/woman to hit the curb (if he/she isn't about the right thing)
e) Raise your children without both parents being in the home

Haters can't stand to see you happy.
Haters will never want to see you succeed.
Most of our haters are people who are supposed to be on our side.

How do you handle your undercover haters?
You can handle these haters by:

1. Knowing who you are & who your true friends are
*(VERY IMPORTANT!!)

2. Having a purpose to your life: Purpose does not
mean having a job. You can have a job and still be
unfulfilled.

A purpose is having a clear sense of what God has called you to be.
Your purpose is not defined by what others think about you.

3. By remembering what you have is by divine
prerogative and not human manipulation.

Fulfill your dreams! You only have one life to live...when its your
time to leave this earth, you want to be able to say, 'I've lived my
life and fulfilled my dreams, Now I'm ready to go HOME!

When God gives you favour, you can tell your haters, 'Don't look at
me...Look at who is in charge of me...'

Read this and share with all of your family & friends who you know are
not hating on you.Just pray for them haters,so that their life can be as fulfilled as
yours! Watch out for Haters...BUT most of all don't become
a HATER!

"Love your enemies for they are your mirror to reality..."

11 April, 2010

kichina china hapa!!

Katika shughuli/mpango mzima wakuongeza nanihii aka ndombolo kwakutumia teknolojia ya wale jamaa zetu wachina basi matokeo yake baadhi ndio kama haya. Ni vizuri watu kuchukua tahadhari unapo tumia madawa hayo ya kuongeza nanihii. Nasema hivo kwasababu mtaka yote siku zote hukosa yote.Pamoja na habari hii kuna waume kwa wanawake wengi ambao wamekwisha tumia hizi dawa za jamaa zetu wachina na wengine kwa lengo la kuongeza nanilii ila matokeo yake si kama walivyotaka. Mfano kuna mwanaume ambaye alikua na nanihii ndogo kakimbiwa sana na wake kwa udogo wa nanihii yake akaona suluhisho ni mchina matokea nanihii ilikua kubwa kupita size za kawaida kwahio akaanza kukimbiwa kwa ukubwa wa mzigo.

Hali kadhalika wanawake waliotaka kuongeza kidogo ndombolo/makalio waliharibikiwa na shepu na mpango mzima makalioni kwani panaweza ongezeka ambapo hapatakiwi hivo kuharibu mpango mzima wa eneo hilo.Tuwe makini na hizo dawa vinginevyo ukiwa kama hawa usimlaumu mtu kwani ni uamuzi wako kumkosoa muumba!



.




kazi ni kazi tu...

Ule msemo wa kazi ni kazi na riziki ni popote ili mradi mkono uende kinywani unaji dhihirisha katika picha hii. Mimi nilidhani haya mambo ni ya ngozi nyeusi tu! kumbe hata weupe wamo!! sasa tuache ubitozi tufanye kazi!!!! Katika pita pita zangu nimegundua kufanya baadhi ya kazi ulaya kumepewa jina maarufu kama KUPIGA BOX kwa baadhi ya kazi ( kama hio kazi yako........heheheh), kwahio TUPIGE BOX kama tunataka pesa of which najua kila mtu anazitaka kwahio tupige kazi kwa bidii kama huyu mama japo kwa namna mbali mbali kutokana na nafasi zetu ili tuweze peleka mkono kinywani vitu kama Burger, wings,vodka na mbege kama ipo unaweza nunua ukiwa na pesa!!! Ulaya kila kitu pesa ati!




Fanya kazi!!!!

09 April, 2010

Helpful kids......

Ni vizuri sana na ni furaha kwakweli kuona mtoto wako anakusaidia kazi za nyumbani.Japo familia nyingi wanaonekana kusaidia kazi hizo ni wasichana. Hata hivyo wapo walio sikika wakilalamika kwanini watoto wakike ndio wafanye hizo kazi hususani wale wakusoma ambao wanahitaji pata muda wa kujisomea warudipo nyumbani! kama ilivyo ada kwa watoto wakiume ambao kazi za jikoni si kawaida kuona wakisaidia.(hii ni kwa watoto walio day) mie ningetaka kusoma boarding straight kama mambo yenyewe ndo hayo hehehe japo unakua unajifunza kazi za jikoni pindi utapoa anza maisha yako.

Mtu anaweza cheka hili jambo ila ni aibu kuna watu unakuta ashakua mtu mzima hajui hata kuosha sahani ama kijiko.Zamani kuna baadhi ya shule walikua wanafundisha cookery course ambayo sijawahi ona mtoto wa kiume anasoma (Late 90s pale Njombe secondari maarufu kama NJOSS) Ila sina shaka na wale ambao wameishi ulaya maana ifikapo muda wa kurudi makwao wanakua wanakaribia kua ma-chef kabisa maana huku lazima ujue kupika ama sivyo utaishia kula burger na junk food ukaharishe vizuri nyumbani kwako hahahhahha.... Well, nilichotaka kusema hapa ni kua makini na mtoto anayekusaidia na kile anacho kusaidia vinginevyo haitakua kusaidia bali uharibifu wa vitu vyako kama ionekanavyo kwa hio picha. yaani sina mbavu na hio picha naona mama mtoto ashituka na kushindwa kushangaa....

kuwa makini na facebook maana......

yaani hii ni sawa na ile ''if walls could sing'', kuta zinaficha mengi ama kila mtu anacho fanya kingekua visible kwa wote. hehehhe nadhani watu labda watu wangekua makini na matendo yao. Kama uonavyo pichani mdada yamempata anajua mwenyewe alicho kosea lakini hayo ndo mambo yanayo jiri kwenye inbox nyingi facebook, sasa ukikosea ukaandika kwenye wall mambo yanakua kama yanavyo onekana hapo kwa picha. Tujiunge....!!






ungekua wewe ndo hii imekutokea ungefanyaje?

Pata ujumbe mzuri kwa kusoma hii

This is beautiful. Read it to the end...the message is awesome!!!

By T. D. Jakes

There are people who can walk away from you.

And hear me when I tell you this! When people can walk away from you: let them walk. I don't want you to try to talk another person into staying with you, loving you, calling you, caring about you, coming to see you, staying attached to you. I mean hang up the phone.

When people can walk away from you let them walk. Your destiny is never tied to anybody that left.

The bible said that, they came out from us that it might be made manifest that they were not for us. For had they been of us, no doubt they would have continued with us. [1 John 2:19]

People leave you because they are not joined to you. And if they are not joined to you, you can't make them stay..

Let them go.

And it doesn't mean that they are a bad person it just means that their part in the story is over. And you've got to know when people's part in your story is over so that you don't keep trying to raise the dead.. You've got to know when it's dead.

You've got to know when it's over. Let me tell you something.. I've got the gift of good-bye. It's the tenth spiritual gift, I believe in good-bye.. It's not that I'm hateful, it's that I'm faithful, and I know whatever God means for me to have He'll give it to me. And if it takes too much sweat I don't need it. Stop begging people to stay.

Let them go!!

If you are holding on to something that doesn't belong to you and was never intended for your life, then you need to.......

LET IT GO!!!

If you are holding on to past hurts and pains .......

LET IT GO!!!

If someone can't treat you right, love you back, and see your worth......

LET IT GO!!!

If someone has angered you.

LET IT GO!!!

If you are holding on to some thoughts of evil and revenge.....

LET IT GO!!!

If you are involved in a wrong relationship or addiction... ..

LET IT GO!!!

If you are holding on to a job that no longer meets your needs or talents

LET IT GO!!!

If you! u have a bad attitude.... ...

LET IT GO!!!

If you keep judging others to make yourself feel better......

LET IT GO!!!

If you're stuck in the past and God is trying to take you to a new level in Him.........

LET IT GO!!!

If you are struggling with the healing of a broken relationship. ....

LET IT GO!!!

If you keep trying to help someone who won't even try to help themselves.. ....

LET IT GO!!!

If you're feeling depressed and stressed ............

LET IT GO!!!

If there is a particular situation that you are so used to handling yourself and God is saying 'take your hands off of it,' then you need to......

LET IT GO!!!

'The Battle is the Lord's!'

During the next 60 seconds, Stop whatever you are doing, and take this opportunity.. ..

(Literally it is only ONE minute!)

All you have to do is the following:

You simply say 'The Lords Prayer' for the person that sent you this message:

The Lords Prayer

Our Father, who are in Heaven, Hallowed be Thy Name, Thy Kingdom Come, Thy Will be done, on Earth as it is in Heaven. Give us this day, our daily bread and forgive us our trespasses as we forgive those who trespass against us. And lead us not into temptation but deliver us from evil.

For Thine is the Kingdom, and the Power, and the Glory, forever.

Amen.

Next, send this message to everyone you know. In a while, more people will have prayed for you and you would have obtained a lot of people praying for others!

Next, stop and think and appreciate God's power in your life, for doing what you know is pleasing to Him.


If you are not ashamed to do this, follow the instructions!

Jesus said, If you are ashamed of me, I will be ashamed of you before My Father'


'Yes, I love my God. He is my fountain of Life and My Savior.

He Keeps me going day and night. Without Him, I am no one. But with Him, I can do everything, Christ is my strength.' This is a simple test.

If you love God and you are not ashamed of all the great things that He has done for you, send this to everyone you know.

God loves you and watches over you everyday

08 April, 2010

Vitu vinavyo udhi katika maisha ya kila siku

1.kutaka usalimiwe ikiwa wewe hutaki kusalimia
2.kutafsiri mtu kwa namna aonekanavyo mfano: mkimya anadharau, hapendi ongea na watu, anajiona; muongeaji sana: atasemwa mwongo, mr/miss misifa, anajifanya mjuaji (maarufu kama much know!!!); ukiwa mnene a.k.a bonge: watasema manyama uzembe, mvivu na usiombe uwe na kitambi simalizii watakayosema hehehe!! ( au sema wewe, unadhani watasemaje?)
3.kudharau mtu mwingine labda kwa kipato chake kidogo ili hali mwenye kipato cha wastani ama kikubwa hana uhusiano wowote na asiye nacho na hata kama kuna uhusiano kuwa nacho si kudharau asiye nacho kwani riziki ya mtu hupangwa na Mungu
4. Kulewa na kusumbua wengine
5.kudharau kazi, wadhifa,elimu,kipato,maisha,kabila,makazi,mavazi ya wengine
6. Kutongoza demu/mchumba/mke wa rafiki/ndugu yako (Tena bila aibu!!!!)
7.Kushika simu ya mwenzio na kuanza ku-browse phone book, gallery (kuangalia picha),kusoma meseji n.k
8. kuweka pass word kwenye simu ( hasa wapenzi!!!), unaficha nini????
9.kushika simu/computer ya mtu na kuanza kufanya settings bila ruhusa. Mfano simu: kubadiri ring tone, theme, menu n.k; Computer: kubadiri back ground,menu na kufungua files na kuanza kusoma ya humo
10.kutaka heshimiwa bila kuheshimu
11.Kuchunguza na kuzungumzia maisha ya mtu asiye kuhusu nap engine humjui na mbaya zaidi unajua haya kuhusu!
12.kumdharau usiye mjua
13. kumwelezea mtu usiye mjua kwa lolote.

Endeleza nyingine unazo zijua wewe hapo!
-----------------------------------------