29 June, 2011

WAZIRI WA FEDHA UFARANSA AWA MKUU WA IMF

                                                                 Christine Lagarde Boss mpya wa IMF


Hatimaye aliyekua waziri wa fedha nchini ufaransa (France)  Bi Christine Lagarde, 55 awa mkuu wa IMF baada ya aliyekua mkurugenzi wa shirika hilo bwana Dominique Strauss-Kahn kujiuzulu kutokana na kashifa ya kutaka kubaka mhudumu wa hoteli nchini Marekani May 2011.


Bi Lagarde ni mwanamke pekee ambaye aliingia katika kinyang'anyiro hicho na watu wengine tisa akiwemo Mohamed El-Erian (Egypt),Stanley Fischer (Israel),Gordon Brown (UK),Kemal Dervis (Turkey),Peer Steinbrueck (Germany),Montek Singh Ahluwalia (India),Agustin Carstens (Mexico),Trevor Manuel (South Africa) na Axel Weber kutoka Ujerumani (Germany)


Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari Bi Lagarde alichuana vikali na Agustin kutoka Mexico na hatimaye kushinda baada ya kuungwa mkono na jumuiya ya Ulaya pamoja na Marekani.Bi Lagarde anatarajia kuanza kazi rasmi kama mkurugenzi wa IMF tarehe 5 July 2011.Wanawake nao wanaweza tuwape nafasi!


Kwa habari zaidi SOMA HAPA






28 June, 2011

SULTAN KOSEN MTU MREFU KUPITA WOTE DUNIANI ANATAFUTA MCHUMBA!!

       Sultan Kosen na He Pingping (picha toka the Telegraph)


Pichani juu ni Sultan Kosen ambaye ndio mtu (mwanaume) mrefu kupita wote duniani kwasasa ambaye ameingia kwenye kumbukumbu za guinness toka February 2011.


Sultan ana urefu wa 251 cm (8 ft 3 inch) na uzito wa 168.2kg na amezaliwa 10 December 1982 huko Mardin Turkey (Uturuki).Hapo yupo na aliyekua mtu mfupi kupita wote He Pingping ambaye kwasasa ameshakufa na amekufa akiwa na umri wa miaka 21, urefu wake ulikua  2 ft 5.37 in (74.61 cm)

Sultan alipo ulizwa ni nini matumaini yake baada ya kuingia kwenye rekodi ya watu warefu akajibu ''napenda kusafiri kote duniani, kupata gari ambayo inanitosha na kuwa na watoto'' Sultan anasema anatafuta mchumba hivi sasa kwahio wadada mnaotaka kuolewa jaribuni bahati yenu!!

Kwa habari zaidi soma HAPAHAPA na HAPA

27 June, 2011

ICC YATOA KIBALI CHA KUMKAMATA GADDAFI LIBYA

International Criminal Court (ICC) imetoa kibali cha kukamatwa kwa Kanali Muammar Gaddafi kiongozi mkuu wa serikali ya Libya na wasaidizi wake wakuu kwa kile kilichodaiwa kutumia jeshi la nchi hiyo kushambulia wananchi waliokua wakiandamana kudai haki.Kibali hicho kina ambatanisha watuhumiwa wa karibu na wasaidizi wakuu kabisa wa Gaddafi akiwemo mtoto wake Saif al-Islam Gaddafi  na mkuu wa usalama wa Libya bwana Abdullah al-Sanussi.
                                                          
Muammar Gaddafi


                                                        Saif al-Islam Gaddafi










Habari zaidi

LIBRARY...

Kwa wale wapenda kusoma vitabu hasa unaposomea maktaba haya mambo yapo sana (angalia picha hapo chini).Hata madarasani kuna wadada wanaova nguo ambazo ukikaa kiti cha nyuma yake unaona shanga,nguo ya ndani n.k.Mie hua najiuliza kama msomi ana vaa vile tena akiwa katika mazingira ya kusoma huko mtaani ana vaa vipi na je jamii inamchukuliaje? Je ndio kuishi kisasa au kishamba? Kwani ukijisitiri vizuri unapungukiwa na nini?






Kwa walio soma UDSM pale chini ya mti wanaita mdegree haya mambo ndio usiseme sijui kama kuna mtu anasomea pale anaelewa! labda kipindi cha mitihani ambapo unaweza somea sehemu yenye kelele za kutosha na ukaelewa kama kawaida.Kama mdegree bado ipo mtazamo wangu naona inafaa kwa mijadala ya vikundi ama kupumzika baada au kabla ya kipindi. Mwisho kabisa ushauri wa bure kwa dada zetu vyuoni na popote pale wapatapo ujumbe huu wavae vizuri kusitiri miili yao wengine inakua vigumu kuvumilia unapo ona maungo ya kike na wakati mwingine kama unasoma unaweza shindwa kuelewa unachosoma

25 June, 2011

WAZIRI AFUNGWA MAISHA RWANDA

Aliyekua waziri wa haki za familia na maendeleo ya wanawake Bi Pauline Nyiramasuhuko afungwa maisha kufuatia madai ya kushiriki katika mauaji ya watusi nchini Rwanda mwaka 1994.Bi Pauline amehukumiwa kifungo cha maisha sambamba na mtoto wake Arsene Shalom Ntahobali ambaye alikua mgambo mashuhuri katika mauaji hayo.Mauaji ya kikabila nchini Rwanda yalianza rasmi mara baada ya kutunguliwa ndege na kumuua aliyekua Rais wa nchi hio JUVENAL HABYARIMANA April 1994 hatimaye kuanza mauaji ya kikabila baina ya wahutu na watusi na kufanya idadi ya waliopoteza maisha hususani kabila la watusi na wahutu kidogo kufikia laki nane (800,000).


Kwa habari zaidi SOMA HAPA


24 June, 2011

NYIMBO MPYA: ALI KIBA-DUSHELELE


HAYA MANENO YAKO SAWA??

No offence intended ni swali tu je haya maneno hapa chini ni sawa? mimi na wewe tunajifunza nini kutokana na haya maneno?. why not wife?

20 June, 2011

MHESHIMIWA AMESEMA.....



Mh Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini CHADEMA afunguka na Fiesta kama ifuatavyo.''Mbeya hatuhitaji upuuzi unaoitwa FIESTA,kwahiyo isije na naapa...uamuzi huu ni sehemu ya mapambano yetu dhidi ya maadui hawa wa maendeleo ya sanaa,and we are very serious on this one!!! Ujmbe huu umepatikana kwenye ukurasa wa muheshimiwa huko Facebook au kitabu cha uso.


Katika kuthibitisha kua hajiwakilishi mwenyewe au kutumia nafasi yake kuzuia fiesta Mbeya muheshimiwa Sugu ameongeza nanukuu ''HATUHITAJI FIESTA MBEYA,MI NAWAKILISHA TU MATAKWA YA VIJANA WA MBEYA...HASA WA MWANJELWA(SIDO) NDO WAMELILETA HILI KWANGU NA NINA FURAHA KUWA NAO NA KUHAKIKISHA MATAKWA YAO YANAKUWA...BY ANY MEANS NECESSRY'' mwisho wa nukuu.


Kibaraza hiki kina imani kwamba ujumbe huu una mengi yaliyojificha nyuma ya pazia na pengine watanzania wangependa kujua hayo yaliyojificha kabla ya kutoa maoni yao.Ukiangalia kwenye ukurasa wenye huo ujumbe (Facebook) maoni ni mengi na yenye mitazamo tofauti.Ni vema na haki muheshimiwa kuwakilisha watu wake lakini pia kuonyesha hao maadui wa sanaa ni wapi na uadui wao ukoje vinginevyo  kila mtu ATASEMA MHESHIMIWA ANATUMIA MABAVU KWA MWAVULI WA CHEO CHAKE KULIPIZA VISASI AU KUTOA KERO ZAKE BINAFSI huo ndio mtazamo wa kibaraza hiki kwani unaposema hili lifanyike/ lisifanyike ni bora kusema kwanini.


K wa habari zaidi:

18 June, 2011

KWELI WALIPA KODI WAKUBWA HATUPENDWI!!!

Nasema hivi kwa sababu wanywaji (sio walevi lol) ndio wanao lipa kodi sana kwa kunywa pombe.Sasa hio parking yao ndio sijaelewa maana hapo hata kama hujanywa hii haiwezi kuwa maegesho ya gari lakini ukisoma hayo maandishi parking imekua reserved for drunk drivers!! kazi kweli kweli..


15 June, 2011

NCHI HATARI KWA WANAWAKE...

Afghanistan, Congo na  Pakistan zimetajwa kua nchi hatari sana kwa wanawake  duniani.Ripoti ya shirika liitwalo Trust Law imethibitisha kuwepo kwa vitendo vya kinyanyasaji kwa wanawake ikiwemo ubakaji wa wanawake kila siku.India na Somalia zinafuata mkumbo na hatimaye kufanya idadi ya nchi hatari kwa wanawake kufika tano.Kwa mujibu wa ripoti hio Congo imefikisha idadi ya wanawake 1150 wanao bakwa kwa siku.

Kwa habari zaidi soma HAPA




KWIKWI ZA FACEBOOK...



Kwa sisi wapenzi wa 'Facebbok' kuna taarifa kwamba  watu wengi wameanza kufunga akaunti za facebook kwa sababu mbalimbali ambazo hazija wekwa wazi kwa sasa.Ripoti ya awali inaonyesha watumiaji wakuu wa facebook ni wa hapa Uingereza na Marekani ambapo kwa Uingereza nusu yao wamefungua akaunti facebook kwa makadirio ya watu million 30-34 na mpaka sasa akaunti 100,000 zimefungwa wakati Marekani akaunti zimepungua kutoka Million 155.2 mpaka 149.4.Hali kadharika Canada zaidi ya akaunti Million 1.5 zimefungwa. 


Wengine wamefunguka kwamba ----->


        Je wewe unasemaje facebook is like-------------------------------!!!?    


Cha ajabu kabisa wakati akaunti zikifungwa nchi zilizo endelea na zenye watumiaji wakubwa hali imekua kinyume na nchi zinazo endelea kwani watu wanajiunga na mtandao wa facebook kwa wingi iwezekanavyo na kuanika habari zao huko bila kujali kama kuna madhara yoyote.Hali hio imepelekea idadi ya watumiaji facebook kufika karibia Million 700.Kwa mujibu wa ripoti hio watu wanafunga akaunti facebook kwa sababu  za kiusalama zaidi kwani ulinzi wa taarifa wanazo weka facebook hauna guarantee mtu anaweza iba na kufanya chochote atakacho kwa mazuri au mabaya.Hivyo wapenzi  na watumiaji wa facebook kumbukeni kufanya security na privacy settings kulinda akaunti zenu ili nanyie msiwe waathirika wa  hujuma zinazo endelea kwenye hicho kitabu cha sura maarufu kama facebook


Kwa habari zaidi bofya HAPA




14 June, 2011

MAMBO YA MPANGALA!!!!

                                    Chanzo:komic first

Tuseme ukweli ukiachana  na hii ya Mpangala kama hali iko hivi Bungeni basi hio posho iondolewe maana sio haki kama mtu unalala  fofo bungeni hio michango ya maendeleo ya jimbo lako unatoa wapi na saa ngapi? Yaani kulala ulale na ukiamka ulipwe?  Angali huyu!! sasa akiamka hapo ni  kugonga meza hoja imepita hata kama hajui inahusu nini (hapa ndipo ninapo wapendea wapiga picha)




Kwa katuni zaidi SOMA HAPA

12 June, 2011

CHANGAMOTO YA LEO

Hakika kwa mtu ambaye hajui mazingira ya elimu tuliyonayo Tanzania hususani vijijini hawezi amini mazingira kama haya, kama haitoshi anaweza dhani Haki elimu wanataka kuiumbua tu serikali lakini huu ndio ukweli wenyewe. Mazingira ya kusomea sio mazuri kabisa katika shule nyingi hata walimu wanavumilia tu jamani  haya mazingira sio kabisa. Darasa utadhani gofu?

Ni imani yangu serikali inaona hivi vielelezo basi kipaumbele kiwekwe katika elimu maana huo utakua msingi moja wapo mzuri wa kuondoa umasikini Tanzania kwani kwa mazingira haya sidhani kama kuna mtoto anaweza fauru masomoyake.Na saa nyingine watoto tunawalaumu bure mazingira wanayo somea ni magumu kiasi kwamba shule inakua kama jela matokeo yake wanafunzi kutoroka shule.

Angalia video hii  uone mazingira wanayo somea viongozi wa kesho(sijui ndio lini?)
                  Kwa hisani ya Hakielimutz

Yaani hapa wakisema kila mtu apige picha ya shule ya msingi aliyosoma kuna watu tutashindwa kuonyesha hio picha maana ni aibu hata watu kuiona japokua sasahivi mtu uko kwenye nafasi fulani (Boss).Ni wachache tutafurahia kuonyesha shule tulizosoma.Sasa tunazisaidiaje hizi shule? 

NO CHABO!!!!!


10 June, 2011

Maisha Ni Foleni by musema kweli

BHOKE:We Had Sex In The House,Not On The Street!!!!!!!!!!!!!!!!

                                                 


Habari zilizo zagaa mitandaoni zinatonya kwamba aliyekua mshiriki wa BBA kutoka Tanzania Bhoke Egna mbali na kufanya madudu dunia nzima ikiwa inaangalia amezidi kuwakera watu hususani Waafrica baada baada ya kujiachia facebook kama ilivyonukuliwa ''"What's the big deal? People were just making a lot of noise about the whole issue as if we were having sex on the street. BBA Amplified house is for adults and whoever cannot 'suck it' up should not even be watching." Hii imedaiwa kua facebook status ya bibie Bhoke  baada ya watu kushangaa mauza uza yake na katika kuthibitisha kua alichofanya na Ernest hakihitaji kujutia.


Mbali na Blogs na mitandao mbalimbali vikiwemo vituo vya Radio na Tv toka Tanzania huko Nigeria watu wameshindwa kuvumilia na hivyo wamemchambua kama karanga tena kwa hasira isiyo pimika. Nao imewauma utadhani wabongo vile lakini nadhani ile dhana ya uafrica  ndio maana wamefunguka sana kuhusu Bhoke ambaye yeye mwenyewe kakili kutojutia kufanya mapenzi mbele ya camera.Hivi huyu dada kama angekili kosa au hata asingizie alilewa au kupitiwa au kumsingizia shetani angepungukiwa nini? maana matusi wanayo toa watu mengi ni kutokana na kauli zake na kusema hajutii kile kitendo hapa kila mtu anashawishika kutukana maana ameaibisha nchi kwa ujumla ukiachia mbali familia.


 Kwa habari zaidi soma HAPA  pia facebook na twitter HAPA


Huko Twitter Bhoke azidi kuji nafasi kama hivi:
:- Bhoke Egina 

-We Had Sex In The House,Not On The Street. 8 hours ago
:- Bhoke Egina 




TASWIRAZZ...

Unaona nini katika hizi picha?



08 June, 2011

MAISHA BORA KWA KILA....

Ndugu msomaji hapo chini ni picha ya usafiri wa Trekta huko Ludewa.Huu ni mfano tu wa maisha halisi watanzania walio wengi katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania.Kwa anaye ishi mjini atashangaa kuona maisha kama haya ila huo ndio ukweli wenyewe huko vijijini.Hapo walipo sina hakika hata wamevaa chochote miguuni ukimuondoa dereva lakini  wao wanaona ni maisha ya kawaida na wameshazoea..

Je mimi na wewe nani angependa kuishi maisha haya?  Ni kweli serikali haiwezi fanya kila kitu kuboresha maisha ya kila mmoja lakini je  hawa watu wamewezeshwa kujikwamua na maisha magumu? hua tunaambiwa kuna pembejeo za ruzuku je zinawafikia walengwa kwa bei nafuu kama ilivyo pangwa?  Ok tumewapa pembejeo za ruzuku ambazo sina hakika kama ni 'ruzuku' hizo bara bara za kupitisha mazao japo kwenda kuuza zipo?? Na mwisho kabisa niseme tu kama mlikua hamjui hawa ndio wapiga kura wetu kwa asilimia kubwa, swali je maisha  bora kwa kila mtanzania yapo au ni kauli mbiu tu ya kisiasa? maana hata bara bara yenyewe hapo mie sijaona ni kama wanakatisha porini tu au macho yangu?.



                               Picha kwa hisani ya mzee wa matukio: Francis Godwin wa                http://francisgodwin.blogspot.com/. kwa habari na picha zaidi bofya hapo uone maisha bora kwa kila Mtanzania!!


Aidha sehemu kama hii nikiambiwa ambulance au gari ya kubebea wagonjwa ni kama hizi hapa sita shangaa
                                           Ambulance hii sijui ni ya wapi?




                                  Hii sijui niite nini.. ilimradi mgonjwa afike (na sina hakika kama atafika!!!)


 Hakika sitabisha kwasababu maisha haya nayajua na kuna sehemu ambazo nisha tembelea (vijijini) ukiumwa na ukapona mshukuru Mungu maana hata mie nili nusurika kufa huko hata kama una pesa hazitakusaidia maana hakufikiki kirahisi .Na sidhani kuna kiongozi mkubwa wa nchi ashawahi fika huko vijijini japo wana magari mazuri kama Land Cruiser VX/V8 na mengine ambayo wanatembelea mjini kwenye lami ambako hata Rav4 ingefaa!!.


Yaani hata wazungu watoa misaada nina imani hawaishi kushangaa wanavyoona usafiri wetu (viongozi) halafu unaita nchi masikini hapo hapo kuna mtu (Mtanzania) anapanda trekta  kusafiri tena ni mpiga kura (mwananchi)  wakati mpigiwa kura (kiongozi) anapanda  Land Cruiser V8 kwa jasho la mpanda trekta hivi hii ni haki kweli? Na kwanini apande trekta na sio bus? jibu la haraka hapo ni miundo mbinu mibovu hakuna mtu atathubutu kupeleka bus huko labda serikali yenyewe ifanye hivyo kama zamani yale ma bus ya serikali sijui yalifia wapi? Magari ya kusafirisha mizigo mfano Iringa kulikua na IRINGA RETCO,Mbeya MBEYA RETCO yale yalikwenda wapi?

ANATAFUTWA RENATHA BENEDICTO

Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.    

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu.    Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html) 

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio.   Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.