12 October, 2011

BLACKBERRY BLACKOUT ENTERS 3RD DAY



A global BlackBerry outage has entered its third day with users more fed up than ever with the disruption to their e-mails, instant messaging and Internet.

The BlackBerry outage, which began at 11am BST on Monday, left 10 million smartphone owners across Europe, the Middle East and South America with limited access to data services.

In an update from the BlackBerry maker last night, Canadian company Research in Motion(RIM) explained the glitch. “The messaging and browsing delays being experienced by BlackBerry users in Europe, the Middle East, Africa, India, Brazil, Chile and Argentina were caused by a core switch failure within RIM’s infrastructure.

TUKO WAWILI PEKEE YETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Ni kweli Mungu anasamehe lakini unapomueleza binadamu mwenzio ubaya huu
unategemea nini................????????????
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.
"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana "
"endelea"
... "bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?
"utasamehewa"
"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"
"utasamehewa"
"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo ?"
- kimya........
"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo ?"
- kimya.........
Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.
"sasa baba mbona umenikimbia?"
padri kwa taabu akajibu "nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili tu peke yetu........"

                 ''AISEE ULIYE ANDIKA HII HONGERA KWA UBUNIFU''