02 May, 2011

BREAKING NEWS:OSAMA BIN LADEN IS NO MORE!!


                                                Osama  Bin Laden enzi za uhai wake.

Kiongozi namba moja wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda (pichani juu) Osama Bin Laden ameripotiwa kuuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan baada ya mapigano makali ya kurushiana risasi kabla ya kifo chake.Habari zilizo tapakaa mitandaoni zinathibitisha kifo cha Osama ikiwa ni baada ya taarifa ya ikulu ya Marekani kuthibitisha kifo hicho kupitia hotuba ya Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye amekaririwa akisema''to those families who have lost loved ones to Al-Qaeda's terror justice has been done''

Osama wakati akitafutwa kwa dili la dola million moja kwa atakaye mpata

Hata hivyo Rais Obama ame tahadharisha balozi zake zote duniani kuwa makini kwa sasa kwani kuna uwezekano wa washirika wa Osama kulipiza kisasi kufuatia kifo cha kiongozi wao. Osama amekua akitafutwa na Marekani kwa muda sasa kufuatia shambulizi la Sept 11,2001 huko New York na Washington ambapo watu karibia 3000 walipoteza maisha.Huko Marekani watu leo wanasherekea kifo cha Bin Laden kwa shangwe zote.Watu mbali mbali pia wamesema Al-Qaeda sio Osama pekee (lile ni kundi kubwa sana) kwahio kazi haijaisha.

Zaidi soma hapa:http://www.bbc.co.uk/news/world-us-canada-13256676
                           :http://latimesblogs.latimes.com/washington/2011/05/osama-bin-laden-dead-al-qaeda-islamabad-navy-seals.html
                           : http://www.guardian.co.uk/world/2011/may/02/osama-bin-laden-arab-reaction
                           :http://www.msnbc.msn.com/id/42852700/ns/world_news-south_and_central_asia/