26 February, 2011

Marekani yafunga ubalozi wake Libya

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha kufungwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Libya mapema leo.Hilo limeenda sambambamba na kuiwekea Libya vikwazo.Pia Rais huyo amenukuliwa akisema machafuko ya kisiasa yanayo endelea nchini Libya yana hatarisha usalama wa raia wake katika balozi hio.

Sambamba na hio Rais Obama pia ame idhinisha kuiwekea vikwazo Libya.Vikwazo vilivyo wekwa ni pamoja na kufuta umiliki wa mali za Gaddafi, watoto wake na utawala mzima zilizomo nchini Marekani isipokua mali za nchi yaani Libya.

Pamoja na hayo Rais Obama anatarajia kukutana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon jumatatu kujadili hatua za kisheria dhidi ya Libya kwa mauaji yanayo endelea nchini Libya.
(voanews.com)

Soma zaidi kwa kiingereza hapa: http://www.voanews.com/english/news/US-Imposes-Sanctions-Closes-Embassy-in-Libya-116974548.html