28 March, 2011

HIVI NDIVYO WENZETU WAKENYA WANASEMA KUHUSU LOLIONDO

Links to this post
Wakenya wataka babu wa Loliondo afungwe kwa kile kinachodaiwa kupotosha watu kwani anajifanya yeye Yesu mponyaji (sijajua wakisikia na ya Mbeya watasema nini!!!!)..Kwa habari zaidi sikiliza hii Video ya kwanza ambayo inataka Babu Mwasapile akamatwe na kufungwa mara moja.Kwa habari zaidi za Loliondo angalia video zinazo fuata kwa hisani ya NTV ya KenyaVideo kwa hisani ya NTV.CO.KE

NAMNA YA KUMKERA MPENZI/MCHUMBA/MKE AU MME

Links to this post
Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza sababisha kuvunjika ama kutoweka uaminifu katika mahusiano.Mie sio mtaalamu sana katika mahusiano lakini mambo nitayo zungumzia hapa hayahitaji utaalamu wowote hasa hiki kipindi cha utanda wazi.Vitu nitavyo taja ni vya maisha ya kawaida ya kila siku kwa wapenzi,wachumba au wanandoa bila kusahau mchango wa vyombo vya mawasiliano katika kubomoa ama kujenga mahusiano Mfano simu, Internet au mitandao ya kijamii kama facebook n.k .

Ni vitu vya kawaida ila madhara yake makubwa kama hutakua makini.Nimezungumza kwa namna vitu hivyo huweza kukera na ukiepuka utakua kwenye safe side.Ungana nami hapa chini:-
1.Ukitumiwa meseji/barua pepe usijibu au jibu siku na saa utakayo jisikia
2.Ukipigiwa simu na mwenza wako usipokee na hata ukiona missed call usipige,wala text,au kuomba kupigiwa!!
3.Ukipigiwa simu mbele ya mwenza wako nenda mbali ukapokee simu huko ukimaliza rudi na muendelee na kile mlikua mnafanya
4.Simu weka password na futa contact records za kila siku kuanzia msg,calls,etc na jina katika contacts andika jina baya baya lisilo lake mfano Jinga,kidumu, kero,msumbufu,wewe nani,wale wale,mzushi etc
5.Akikupunguzia salio kwenye simu wewe mpunguzie mwingine(mke mpunguzie mwaname mwingine),(mme -mpunguzie msichana mwingine) na baada ya hapo uwe una beep tu hata kama umepunguziwa salio.
6.Mkiwa pamoja matembezini kama wewe mke uwe unaangalia sana wanaume wengine na mwanaume uwe unaangalia wasichana wengine na kutokusikilizana.
7.Usiwe na attention yeyote wanasema ''kila mtu ana shida zake usikilize za mwingine za nini''
8.Kuwa bize na vitu visivyo eleweka mfano kutuma text zisizo isha au kuwapigia watu wengine simu na kuongea umbea wakati mwenza wako anataka kuongea na wewe.
9.Uwe mchafu mchafu usiye jipenda
10.Uwe umenuna kila mara
11.Zima simu kila ukiwa na mwenzio ili usipigiwe na yeyote na kuiweka mbali na mlipo.
12.Ukiwa nae sifia (mme-sifia wanawake wengine eti wazuri na wana adabu), (mke-sifia wanaume wengine mbele yake)
13.Toa siri zenu zote watu wajue (hata za chumbani!!)
14.Kusemana mbele za watu au kutukana mwenzio kwa dharau
15.Uwe unachelewa kurudi nyumbani bila sababu za msingi (kwa wanandoa)
16.Kunywa sana ukifika nyumbani tapika (kuny*) kila mahali na usisafishe!!
17.Ukiongozana na mpenzi wako mtambulishe kama rafiki yako kwa rafiki zako
18.Mkiongozana kila mtu atembee pekee yake kama hamjuani vile.
19.Kama mna kawaida ya kwenda club basi kila mtu acheze na mtu anayetaka cheza naye na kwa kujiachia!
20.Kuwa mtu unayetaka kuheshimiwa bila kuheshimu kisa your somebody kazini,ktk biashara,n.k
21.Ukiwa na mwenza wako zungumzia zaidi past relations  zilivyo kua na namna mlivyokua mki enjoy na mengine mengi.

NB.Si kila mtu anachukulia sawa jambo fulani kwahio kuwa makini na tabia zako au mambo unayo fanya.Ukiepuka hii utakua umeepuka mengi.Pia nitafurahi kama kuna mwenye zaidi kwani haya ni baadhi tu ya mambo yanayo kera.Kama una zaidi unaweza acha kwenye comments.Pamoja!