20 February, 2010

Tujikumbushe wosia wa Baba wa Taifa na Rushwa

Ivi kama kweli hali halisi ya wala rushwa ingekua hivi kiutendaji na sio maneno matupu ingekuaje?? wenzetu wachina mla rushwa hawana mjadala nae wanamuua fasta akale rushwa awezavyo huko peponi. Hali kadharika drug dealers anauawa bila kuangalia ni nani, ana rangi gani, cheo, anatokea wapi. Mfano mzuri wa drug dealer/smuggler ni wa yule raia wa uingereza (Akmal Shaikh) ambaye pamoja na madai kwamba alikua chizi alihukumiwa bila kujali anatoka taifa kubwa. Nadhani msimamo kama huu ukitumika tz rushwa itaisha. Kwa maneno mengine wanasema ukitaka kumuua nyani usiangalie uso kwani utamuonea huruma.Na mafanikio zaidi yanawezekana kama adhabu kali itaanzia na wala rushwa wakubwa aka nyangumi na kumaliza na wadogo aka dagaa.Bila hivyo rushwa utabaki kua wimbo.Kwasababu kama mkubwa anakula rushwa mdogo unategemea afanye nini? Na kama mkubwa ataachwa wakati mdogo ana kamatwa basi hio ni sawa na usemi wa mkubwa akichafua hewa (jamba) kapumua wakati huo huo mdogo akifanya tendo hilo kachafua hewa.haki iko wapi?????? Tujiunge kumsikia Baba kwanza >>>>>
-------------------------------------------------------------------------------------