Showing posts with label UK. Show all posts
Showing posts with label UK. Show all posts

20 October, 2011

TATIZO LA AJIRA LIPO KILA SEHEMU

                            Watu 500 wapanga mstari kuomba kazi (nafasi 20 tu) UK

Kufuatia kuanguka kwa uchumi kuanzia mwaka 2008/2009 ambako kumeathiri mzunguko wa fedha nchi mbalimbali duniani ambapo kila serikali iliweza jitahidi kunusuru uchumi wake kwa namna yake.Hapa Uingereza Gordon Brown alilazimika kuuza nusu ya dhahabu ya nchi kunusuru uchumi ulio yumba.(soma hapa).USA nao wali inusuru nchi kwa $700 Billion (soma hapa).Anguko hilo la uchumi lilipelekea makampuni mengi kufungwa na kupoteza ajira za watu wengi sehemu mbalimbali duniani.Hapa UK watu zaidi ya 2 million hawana ajira hivi sasa na serikali ndio inawagaramia kwa job seekrs allowance (kwa wazawa na wenye sheria ya kuishi nchi hii)


Sijashangaa kuona msururu ulijitokeza Chuo kikuu Dodoma kwa nafasi 12 za ajira.Ila nimeshangazwa na utaratibu wa kuita watu zaidi  ya 2000 kwa nafasi 12 za ajira.
    Ati msururu wote huu waitwa kwa usaili wa nafasi 12 za kazi!!! hivi inaingia akilini??
   (picha kwa hisani ya Bongo Pix Blog)

Hii ni kuchezea akili za watu huwezi ita (shortlist) watu 2000 kwa nafasi 12.Hawa watu wanasafiri toka sehemu mbalimbali sio ustarabu kuita watu wote hao kwa nafasi hizo chache (soma hapa na hapa).Hii ni sawa na shule/chuo kinachochukua wanafunzi 100 kutoa fomu laki moja za kuomba nafasi tena kwa kulipisha watu pesa huu ni wizi wa hali ya juu sana.Ufisadi sio lazima mtu ale rushwa hata huu ni ufisadi.

09 August, 2011

VURUGU ZA LONDON ZASAMBAA MIJI MINGINE

Kumezuka vurugu jijini London Uingereza baada ya raia mmoja kupigwa risasi na polisi.Vurugu hizo zilizuka baada ya polisi kuzuia maandamano ya amani na kuhoji kwanini raia Mark Duggan (29) aliuawa na polisi kwa kupigwa risasi? Tukio hilo lilitokea Tottenham Alhamis Tar 04 na Jumamosi ya tarehe 06/08/2011 ndipo vurugu zilipozuka eneo hilo na kusambaa miji kadhaa hapa England.
Mark Duggan,29 wakati wa uhai wake


Hali hiyo ya vurugu imeingia kwa kasi miji mingine kama Birmingham,Liverpool,Manchester na Bristol.Ukiachia mbali huyu jamaa kuwa chanzo maisha magumu,ukosefu wa ajira unaozidi kukua na ubaguzi wa rangi vimetajwa kuchangia vurugu kuungwa mkono kwa kasi.Waziri mkuu David  Cameron aliyekua mapumzikoni Italy amelazimika kurudi kwani hali ni tete.Jana 08/08/2011 Birmingham palikua hapatoshi.

 Jengo limechomwa moto Croydon
 Polisi ambao walizidiwa nguvu wakiwa wanaangalia kinacho endelea kama kideo!
 maduka,magari yalichomwa moto
 Mtaani kulikua kama hivi
Jamaa  wenye mask wakiiba dukani na kuvunja ATM machine na kuiba Pound!
Picha zote toka Aljazeera na BBC
Kwa habari zaidi soma HAPA na HAPA

28 April, 2011

MALAWI WAMWAGA UGALI,UINGEREZA WAMWAGA MBOGA!!!

Ni katika sakata la uongozi unaodaiwa kuwa ni mbovu nchini Malawi ambapo aliye kua boss wa Malawi enzi za ukoloni ikiitwa Nyasaland (Uingereza/UK) ambaye pia ndio mtoa misaada mkuu nchini humo amesiitisha misaada hio tangu mwaka jana kwa kiasi cha Pauni Million 3 kutokana na matumizi mabovu ya serikali ya Malawi.Kwa mujibu wa gazeti la 'The Telegraph' matumizi mabovu ni pamoja na ununuzi wa ndege ya Rais Bingu Wa Mutharika kwa kiasi cha pauni million 8 kwa nchi masikini kama Malawi.

Katika sakata hilo Balozi wa Uingereza nchini Malawi  Mr Fergus Cochrane-Dyet ameamriwa kuondoka nchini humo kwa kosa la kuikosoa Serikali ya Malawi kwa matumizi mabovu na kunyima uhuru wa wananchi kuongea ama kuikosoa serikali kama ilivyo ripotiwa na wana harakati wa haki za binadamu.Kufuatia uamuzi huo wa Malawi, Uingereza nao wamemtaka kaimu balozi wa Malawi nchini Uingereza kuondoka mara moja. Amri hiyo imetolewa jana na  katibu wa Uingereza mambo ya nje William Hague

21 March, 2011

LIBYA SI SHWARI TENA!!

Baada ya vikao kadhaa vya baraza  la usalama la umoja wa mataifa kutafuta mstakabali wa machafuko nchini Libya ambapo China na Russia zilionyesha waziwazi kutoshiriki na lolote huko Libya.Marekani haikua tayari bila tamko la baraza la umoja wa mataifa ambalo limepita na Marekani iko mstari wa mbele kushambulia maeneo muhimu yanayosadikika kutunza silaha inchini Libya.Rais wa Marekani ambaye yupo ziarani nchini Brazil ametoa idhini ya jeshi lake kuendesha mashambulizi ya kijeshi inchini Libya.


Jengo la kijeshi lilio haribiwa Tripoli-Libya

Shambulizi la kwanza limeripotiwa kuharibu jengo kubwa la kijeshi na kuangusha ndege 4 za kijeshi za jeshi la Gaddafi.Hata hivyo Gaddafi ametangaza kuangusha ndege yeyote itayo onekana juu au eneo lote la Mediteranian sea zikiwemo ndege za abiria huku akitahadharisha kua atatumia silaha nzito ambazo hajaanza kutumia na ameahidi kushinda mashambulizi ya wana muungano wa umoja wa mataifa wakiongozwa na USA,UK & FRANCE.Vita kwa namna yoyote si nzuri Mungu awasaidie.


   
                                       Kituo kimoja cha ulinzi wa anga Libya kikiwa kinawaka moto baada ya kulipuliwa na majeshi ya muungano wa UK,USA na FRANCE.

Kwa habari zaidi soma hapa
>> http://abcnews.go.com/International/libya-international-military-coalition-launch-assault-gadhafi-forces/story?id=13174246

>> http://abcnews.go.com/wnt/video/special-report-target-libya-president-politics-war-obama-military-13175613&tab=9482930&section=1206853&playlist=1363340