10 May, 2010

Hongera sana Ernest Makulilo


(Picha toka Facebook)

Napenda kutumia fursa hii kukupa hongera Mdau Ernest Makulilo kwa hatua uliofikia ya kufunga pingu za maisha na kuachana ukapera. Japo sijajua watu ( wabongo) wanataka nini hasa waonapo mtu anafanikiwa ama kufanya jambo fulani zuri huishia kuponda na kutoa comments zinazo katisha tamaa! Yaani sasa imekua kama ndo msemo mtu akioa mzungu anataka PAPERS aka MAKARATASI!!! Hua nashindwa kupata jibu kama kwa sasa watu wameanza kupanga maisha ya mtu mwingine ama Mungu pekee ndio anaweza panga?? Na kwanini mtu aponde wakati maisha ni ya kwako si yake na wala haya mhusu?! kwanini kila asiangalie maisha yake?

Nilipoona hii '' MZEE WA NONDOZZZZZZZ ERNEST MAKULILO NA MARIE WAMEREMETA'' nilifurahi lakini nikawa na shauku kuona comments ambazo zilikua nyingi kabisa... kwa muda huo zilikua 52...nilitegemea kuona HONGERA nyingiiiii lakini cha ajabu na kilicho sikitisha zaidi karibia kila comment inasema MAKARATASI,MARA SIJUI AGE IS JUST A NUMBER!!! what is this for? kwa mtindo huu ninathubutu kusema kuna watu wataishia kusema ya watu na kushindwa kufanya yao....kwani MAKARATASI NDIO NINI? MTU BILA MAKARATASI HUWEZI ISHI? wewe maisha yake yanakuhusu nini? kwanini kama huna cha kuongea usikae kimya??!!

LAZIMA TUFIKE MAHALI TUKUBALI MATOKEO...Mtu sijui niite HATER anatoa comment kama hii '' nasikia harufu ya MAKATARATASI AU hapo hakuna kitu ila MAKARATASI halafu mwisho anamalizia HONGERA SANA!!! Kama sio unafiki ni nini??!! kwahio mtu anaponda huku anakubali kimoyo moyo..kiukweli sio nzuri wenye tabia kama hizi ni vema wakabadirika kwani ni wazi kwamba mtu ukiwa na roho ya korosho hutakaa uendelee utabaki kusema ya watu tu, fanya yako..kila mtu ana yake FANYA YAKO!! na ukiwa huna cha kuongea ni vema KUKAA KIMYAA HAIKUPUNGUZII CHOCHOTE kuliko kumaliza muda wako kuongea ya watu!! ( yani comments zimenichefua utadhani nasemwa mimi hahahhaha!!)


(Picha toka Facebook)

picha zaidi toka facebook>>>
http://www.facebook.com/photo.php?pid=12573404&id=623205200

Binafsi natumaini Mungu atakubariki zaidi na maisha yatakua mazuri kwa sasa na huko mbeleni maneno ya watu ni kama mbu nje ya net au kelele za vyura ambazo hazizuii ng'ombe kunywa maji mtoni hehehe!. Pamoja na mambo mengine umekua mtu wa kujitolea kutoa habari mbalimbali za vyuo na scholarship ambazo zimesaidia watu mbalimbali katika kujipatia habari za namna hio kupitia blog yako
ni imani yangu wapenda maendeleo watakubaliana na mimi katika kutambua mchango wako katika swala zima la elimu. Kwa kupata habari zaidi za scholarships tembelea
-------------------------------------------------------------------------------------
http://www.makulilo.blogspot.com/ na
http://scholarshipnetwork.ning.com/