17 November, 2012

MHE.JACKSON MAKWETA AFARIKI DUNIA,SERIKALI YATANGAZA

17 Novemba, 2012  
 
                                                          
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA
 
SERIKALI inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta kilichotokea leo saa 11 jioni katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.
 
Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa
Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye. 
 
Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri
katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu,
Kilimo na Utumishi.
 
Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya
miaka 35.
 
 
 (mwisho)
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012.