Watu 500 wapanga mstari kuomba kazi (nafasi 20 tu) UK
Kufuatia kuanguka kwa uchumi kuanzia mwaka 2008/2009 ambako kumeathiri mzunguko wa fedha nchi mbalimbali duniani ambapo kila serikali iliweza jitahidi kunusuru uchumi wake kwa namna yake.Hapa Uingereza Gordon Brown alilazimika kuuza nusu ya dhahabu ya nchi kunusuru uchumi ulio yumba.(soma hapa).USA nao wali inusuru nchi kwa $700 Billion (soma hapa).Anguko hilo la uchumi lilipelekea makampuni mengi kufungwa na kupoteza ajira za watu wengi sehemu mbalimbali duniani.Hapa UK watu zaidi ya 2 million hawana ajira hivi sasa na serikali ndio inawagaramia kwa job seekrs allowance (kwa wazawa na wenye sheria ya kuishi nchi hii)
Sijashangaa kuona msururu ulijitokeza Chuo kikuu Dodoma kwa nafasi 12 za ajira.Ila nimeshangazwa na utaratibu wa kuita watu zaidi ya 2000 kwa nafasi 12 za ajira.
Ati msururu wote huu waitwa kwa usaili wa nafasi 12 za kazi!!! hivi inaingia akilini??
(picha kwa hisani ya Bongo Pix Blog)
Hii ni kuchezea akili za watu huwezi ita (shortlist) watu 2000 kwa nafasi 12.Hawa watu wanasafiri toka sehemu mbalimbali sio ustarabu kuita watu wote hao kwa nafasi hizo chache (soma hapa na hapa).Hii ni sawa na shule/chuo kinachochukua wanafunzi 100 kutoa fomu laki moja za kuomba nafasi tena kwa kulipisha watu pesa huu ni wizi wa hali ya juu sana.Ufisadi sio lazima mtu ale rushwa hata huu ni ufisadi.
No comments:
Post a Comment