Chuo United Kingdom (UK) au Gari i.e.Vogue 4x4, Toyota VX,Lexus,Rav4,Avensis Saloon BMW X5,Jaguar,Vw Touareg Passat,Golf,Ford,Land Rover TDi;TD5-6,Freelander, Honda-CRV, Nissan, Mercedes Benz,Q7/AUDI,Suzuki Vitara,Grand Vitara,Volvo,Cadillac,etc,Scania 113,124 n.k. Burudani i.e Original Plasma TV, Powerful Home Theatres,Projectors,Speakers, Dj Mixers,Digital Cameras, Laptops, Massive Data Storage Facilities(External/Internal HDD).Contact me via rijaki@ymail.com
20 June, 2011
MHESHIMIWA AMESEMA.....
Mh Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini CHADEMA afunguka na Fiesta kama ifuatavyo.''Mbeya hatuhitaji upuuzi unaoitwa FIESTA,kwahiyo isije na naapa...uamuzi huu ni sehemu ya mapambano yetu dhidi ya maadui hawa wa maendeleo ya sanaa,and we are very serious on this one!!! Ujmbe huu umepatikana kwenye ukurasa wa muheshimiwa huko Facebook au kitabu cha uso.
Katika kuthibitisha kua hajiwakilishi mwenyewe au kutumia nafasi yake kuzuia fiesta Mbeya muheshimiwa Sugu ameongeza nanukuu ''HATUHITAJI FIESTA MBEYA,MI NAWAKILISHA TU MATAKWA YA VIJANA WA MBEYA...HASA WA MWANJELWA(SIDO) NDO WAMELILETA HILI KWANGU NA NINA FURAHA KUWA NAO NA KUHAKIKISHA MATAKWA YAO YANAKUWA...BY ANY MEANS NECESSRY'' mwisho wa nukuu.
Kibaraza hiki kina imani kwamba ujumbe huu una mengi yaliyojificha nyuma ya pazia na pengine watanzania wangependa kujua hayo yaliyojificha kabla ya kutoa maoni yao.Ukiangalia kwenye ukurasa wenye huo ujumbe (Facebook) maoni ni mengi na yenye mitazamo tofauti.Ni vema na haki muheshimiwa kuwakilisha watu wake lakini pia kuonyesha hao maadui wa sanaa ni wapi na uadui wao ukoje vinginevyo kila mtu ATASEMA MHESHIMIWA ANATUMIA MABAVU KWA MWAVULI WA CHEO CHAKE KULIPIZA VISASI AU KUTOA KERO ZAKE BINAFSI huo ndio mtazamo wa kibaraza hiki kwani unaposema hili lifanyike/ lisifanyike ni bora kusema kwanini.
K wa habari zaidi:
18 June, 2011
KWELI WALIPA KODI WAKUBWA HATUPENDWI!!!
Nasema hivi kwa sababu wanywaji (sio walevi lol) ndio wanao lipa kodi sana kwa kunywa pombe.Sasa hio parking yao ndio sijaelewa maana hapo hata kama hujanywa hii haiwezi kuwa maegesho ya gari lakini ukisoma hayo maandishi parking imekua reserved for drunk drivers!! kazi kweli kweli..
15 June, 2011
NCHI HATARI KWA WANAWAKE...
Afghanistan, Congo na Pakistan zimetajwa kua nchi hatari sana kwa wanawake duniani.Ripoti ya shirika liitwalo Trust Law imethibitisha kuwepo kwa vitendo vya kinyanyasaji kwa wanawake ikiwemo ubakaji wa wanawake kila siku.India na Somalia zinafuata mkumbo na hatimaye kufanya idadi ya nchi hatari kwa wanawake kufika tano.Kwa mujibu wa ripoti hio Congo imefikisha idadi ya wanawake 1150 wanao bakwa kwa siku.
Kwa habari zaidi soma HAPA
Kwa habari zaidi soma HAPA
KWIKWI ZA FACEBOOK...
Kwa sisi wapenzi wa 'Facebbok' kuna taarifa kwamba watu wengi wameanza kufunga akaunti za facebook kwa sababu mbalimbali ambazo hazija wekwa wazi kwa sasa.Ripoti ya awali inaonyesha watumiaji wakuu wa facebook ni wa hapa Uingereza na Marekani ambapo kwa Uingereza nusu yao wamefungua akaunti facebook kwa makadirio ya watu million 30-34 na mpaka sasa akaunti 100,000 zimefungwa wakati Marekani akaunti zimepungua kutoka Million 155.2 mpaka 149.4.Hali kadharika Canada zaidi ya akaunti Million 1.5 zimefungwa.
Wengine wamefunguka kwamba ----->
Je wewe unasemaje facebook is like-------------------------------!!!?
Cha ajabu kabisa wakati akaunti zikifungwa nchi zilizo endelea na zenye watumiaji wakubwa hali imekua kinyume na nchi zinazo endelea kwani watu wanajiunga na mtandao wa facebook kwa wingi iwezekanavyo na kuanika habari zao huko bila kujali kama kuna madhara yoyote.Hali hio imepelekea idadi ya watumiaji facebook kufika karibia Million 700.Kwa mujibu wa ripoti hio watu wanafunga akaunti facebook kwa sababu za kiusalama zaidi kwani ulinzi wa taarifa wanazo weka facebook hauna guarantee mtu anaweza iba na kufanya chochote atakacho kwa mazuri au mabaya.Hivyo wapenzi na watumiaji wa facebook kumbukeni kufanya security na privacy settings kulinda akaunti zenu ili nanyie msiwe waathirika wa hujuma zinazo endelea kwenye hicho kitabu cha sura maarufu kama facebook
Kwa habari zaidi bofya HAPA
14 June, 2011
MAMBO YA MPANGALA!!!!
Chanzo:komic first
Tuseme ukweli ukiachana na hii ya Mpangala kama hali iko hivi Bungeni basi hio posho iondolewe maana sio haki kama mtu unalala fofo bungeni hio michango ya maendeleo ya jimbo lako unatoa wapi na saa ngapi? Yaani kulala ulale na ukiamka ulipwe? Angali huyu!! sasa akiamka hapo ni kugonga meza hoja imepita hata kama hajui inahusu nini (hapa ndipo ninapo wapendea wapiga picha)
Kwa katuni zaidi SOMA HAPA

12 June, 2011
CHANGAMOTO YA LEO
Hakika kwa mtu ambaye hajui mazingira ya elimu tuliyonayo Tanzania hususani vijijini hawezi amini mazingira kama haya, kama haitoshi anaweza dhani Haki elimu wanataka kuiumbua tu serikali lakini huu ndio ukweli wenyewe. Mazingira ya kusomea sio mazuri kabisa katika shule nyingi hata walimu wanavumilia tu jamani haya mazingira sio kabisa. Darasa utadhani gofu?
Ni imani yangu serikali inaona hivi vielelezo basi kipaumbele kiwekwe katika elimu maana huo utakua msingi moja wapo mzuri wa kuondoa umasikini Tanzania kwani kwa mazingira haya sidhani kama kuna mtoto anaweza fauru masomoyake.Na saa nyingine watoto tunawalaumu bure mazingira wanayo somea ni magumu kiasi kwamba shule inakua kama jela matokeo yake wanafunzi kutoroka shule.
Angalia video hii uone mazingira wanayo somea viongozi wa kesho(sijui ndio lini?)
Kwa hisani ya Hakielimutz
Yaani hapa wakisema kila mtu apige picha ya shule ya msingi aliyosoma kuna watu tutashindwa kuonyesha hio picha maana ni aibu hata watu kuiona japokua sasahivi mtu uko kwenye nafasi fulani (Boss).Ni wachache tutafurahia kuonyesha shule tulizosoma.Sasa tunazisaidiaje hizi shule?
10 June, 2011
BHOKE:We Had Sex In The House,Not On The Street!!!!!!!!!!!!!!!!
Habari zilizo zagaa mitandaoni zinatonya kwamba aliyekua mshiriki wa BBA kutoka Tanzania Bhoke Egna mbali na kufanya madudu dunia nzima ikiwa inaangalia amezidi kuwakera watu hususani Waafrica baada baada ya kujiachia facebook kama ilivyonukuliwa ''"What's the big deal? People were just making a lot of noise about the whole issue as if we were having sex on the street. BBA Amplified house is for adults and whoever cannot 'suck it' up should not even be watching." Hii imedaiwa kua facebook status ya bibie Bhoke baada ya watu kushangaa mauza uza yake na katika kuthibitisha kua alichofanya na Ernest hakihitaji kujutia.
Mbali na Blogs na mitandao mbalimbali vikiwemo vituo vya Radio na Tv toka Tanzania huko Nigeria watu wameshindwa kuvumilia na hivyo wamemchambua kama karanga tena kwa hasira isiyo pimika. Nao imewauma utadhani wabongo vile lakini nadhani ile dhana ya uafrica ndio maana wamefunguka sana kuhusu Bhoke ambaye yeye mwenyewe kakili kutojutia kufanya mapenzi mbele ya camera.Hivi huyu dada kama angekili kosa au hata asingizie alilewa au kupitiwa au kumsingizia shetani angepungukiwa nini? maana matusi wanayo toa watu mengi ni kutokana na kauli zake na kusema hajutii kile kitendo hapa kila mtu anashawishika kutukana maana ameaibisha nchi kwa ujumla ukiachia mbali familia.
Kwa habari zaidi soma HAPA pia facebook na twitter HAPA
Huko Twitter Bhoke azidi kuji nafasi kama hivi:
:-bhokebba Bhoke Egina
:-bhokebba Bhoke Egina
Live your life people.And yes,Ernest is a great guy,a friend;nothing further.
08 June, 2011
MAISHA BORA KWA KILA....
Ndugu msomaji hapo chini ni picha ya usafiri wa Trekta huko Ludewa.Huu ni mfano tu wa maisha halisi watanzania walio wengi katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania.Kwa anaye ishi mjini atashangaa kuona maisha kama haya ila huo ndio ukweli wenyewe huko vijijini.Hapo walipo sina hakika hata wamevaa chochote miguuni ukimuondoa dereva lakini wao wanaona ni maisha ya kawaida na wameshazoea..
Je mimi na wewe nani angependa kuishi maisha haya? Ni kweli serikali haiwezi fanya kila kitu kuboresha maisha ya kila mmoja lakini je hawa watu wamewezeshwa kujikwamua na maisha magumu? hua tunaambiwa kuna pembejeo za ruzuku je zinawafikia walengwa kwa bei nafuu kama ilivyo pangwa? Ok tumewapa pembejeo za ruzuku ambazo sina hakika kama ni 'ruzuku' hizo bara bara za kupitisha mazao japo kwenda kuuza zipo?? Na mwisho kabisa niseme tu kama mlikua hamjui hawa ndio wapiga kura wetu kwa asilimia kubwa, swali je maisha bora kwa kila mtanzania yapo au ni kauli mbiu tu ya kisiasa? maana hata bara bara yenyewe hapo mie sijaona ni kama wanakatisha porini tu au macho yangu?.
Aidha sehemu kama hii nikiambiwa ambulance au gari ya kubebea wagonjwa ni kama hizi hapa sita shangaa
Ambulance hii sijui ni ya wapi?
Hii sijui niite nini.. ilimradi mgonjwa afike (na sina hakika kama atafika!!!)
Hakika sitabisha kwasababu maisha haya nayajua na kuna sehemu ambazo nisha tembelea (vijijini) ukiumwa na ukapona mshukuru Mungu maana hata mie nili nusurika kufa huko hata kama una pesa hazitakusaidia maana hakufikiki kirahisi .Na sidhani kuna kiongozi mkubwa wa nchi ashawahi fika huko vijijini japo wana magari mazuri kama Land Cruiser VX/V8 na mengine ambayo wanatembelea mjini kwenye lami ambako hata Rav4 ingefaa!!.
Yaani hata wazungu watoa misaada nina imani hawaishi kushangaa wanavyoona usafiri wetu (viongozi) halafu unaita nchi masikini hapo hapo kuna mtu (Mtanzania) anapanda trekta kusafiri tena ni mpiga kura (mwananchi) wakati mpigiwa kura (kiongozi) anapanda Land Cruiser V8 kwa jasho la mpanda trekta hivi hii ni haki kweli? Na kwanini apande trekta na sio bus? jibu la haraka hapo ni miundo mbinu mibovu hakuna mtu atathubutu kupeleka bus huko labda serikali yenyewe ifanye hivyo kama zamani yale ma bus ya serikali sijui yalifia wapi? Magari ya kusafirisha mizigo mfano Iringa kulikua na IRINGA RETCO,Mbeya MBEYA RETCO yale yalikwenda wapi?
ANATAFUTWA RENATHA BENEDICTO
Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.
Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu. Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html)
Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio. Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.

01 June, 2011
26 May, 2011
LEO TUCHEKE KIDOGO...
chanzo:orijino komedi
25 May, 2011
24 May, 2011
FACEBOOK KIBONGO BONGO..
Mimi nimejiunga facebook ili kukutana na marafiki niliopotezana nao muda mrefu mfano Classmates,School mates, University mates,Work/field mates na wengine ili kujuliana hali (kuwasilina kama marafiki), kudumisha urafiki na kupashana habari zinazo tokea kila mtu alipo kwa wakati ule.Facebook inasaidia kupata marafiki mlipotezana nao hata marafiki wapya na kuwakutanisha
Facebook logo
Facebook inasaidia kukutanisha watu kwa matukio mbalimbali ya kijamii mfano weddings,parties,kucheza games mbalimbali,kutangaza biashara; kisiasa mfano: mikutano,maandamano; kisayansi mfano: kuendesha mijadala ya kitaaluma na mambo ya teknolojia i.e IT,.Huko Egypt (Misri) Facebook imesaidia kukutanisha watu ambao wameweza hata kuing'oa serikali ya muda mrefu ya Hosni Mubarak (14 October 1981 – 11 February 2011) na hata watoto kubatizwa 'Facebook' kama kumbukumbu ya tukio hilo.
Watanzania wengi tumejiunga Facebook kwa kasi kubwa tu,ni vizuri japo sijajua kama matumizi ya huu mtandao yapo sawa! Kwa mtumiaji wa facebook unaweza kua unanielewa.Wengine picha tunazoweka humo ni utata mtupu mfano mtu kaweka picha ya makalio yake tu yakiwa tupu ama nguo inayo onyesha maungo,shanga kiunoni,lips peke yake,au mwili wote ukiwa na chupi tu,kifua wazi ili iweje? au mtu kaweka picha yenye maneno 'I've the p**sy (ni tusi siwezi andika lote) so I make the rules' ili iweje?.
Tujiulize tumejiunga facebook ili iweje?.Mtu unakuta yupo ofisini the whole day yuko online (sio idle) facebook hio kazi anafanya saa ngapi? Mimi nimeona facebook kwa bongo ni 'more of a dating site' je wewe unaionaje? au unaichukuliaje?.Kiufupi madhara ya facebook ni makubwa kuliko, mfano watu wengi wamefukuzwa kazi,ndoa nyingi zimevunjika,watu wengi wameuawa kwa kupitia facebook hasa wale wasio ogopa kukutana mtu usiye mjua,kubakwa,kufungwa, mahusiano mengi yamevunjwa,na watu wengi sasahivi hufuta (deactivate) akaunti facebook wanapooa,kuolewa ama kugonganisha wapenzi.Be careful na facebook kabla huja umbuka...na pia nijibu......
Wewe umejiunga facebook ili iweje?
Kiraka amejiunga facebook ili......
Ochu anajibu hilo swali msikilize hapa chini
UFUNGUKAJI WA WASANII WETU OVYO!!
Hapa chini ni video ya Clouds Tv 'Take one' 'MTU KATI' na Zamaradi.Angalia vizuri hii Video clip then sikiliza mtu kama msanii ambaye ni kioo cha jamii anapo ongea katika chombo cha habari.Kuna kipengele anasema usanii wake umemuweka karibu na mabinti,imempa mademu,imemuongezea upendo kwa mademu!!! huyu ndio kioo cha jamii!! ...Ninge elewa angesema usanii wake umemuweka karibu na watu SIO MADEMU (HII NI PUMBA).Pia anasema hua anafanya ukauzu kwa mademu wanao mtega kwa kuvaa miwani tinted kwa maana hio ''katufanyia ukauzu Watanzania tunao angalia hii interview kwa kutuvalia hio miwani'' MAELEZO YAKE HAYAJA JITOSHELEZA!!
Si kwamba na 'hate' kwanza simfahamu namsikia tu....Kiukweli ameongea kituko cha mwaka coz movie hawangalii mademu peke yao,aidha kwenye hii interview MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.. nimependa kipengele cha matumizi mabaya ya lugha katika movie zetu (movie editors kama wapo wawe makini na kazi yao) na sehemu nyingine zote uozo mtupu na ameaibisha wasanii wenzie (mtazamo wangu)...sikiliza halafu nipe mtazamo wako pia (ni mtazamo tu)
Vituko vingine vya wasanii angalia hapa: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/hasheem-thabeet-afanya

Msikilize Hemed akifunguka hapa chini (Aibu)
(kwa hisani ya Zamaradi Mketema)
Vituko vingine vya wasanii angalia hapa: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/hasheem-thabeet-afanya
By
Rik Kilasi
On
Tuesday, May 24, 2011
0
comments
Labels:
BONGO CELEBS,
HEMED,
TAKE ONE,
ZAMARADI MKETEMA
SIMBA SC KUVAANA NA BIRMINGHAM CITY FC JULY 7 MWAKA HUU
Timu ya mpira Simba Sports Club ya Dar es salaam kuvaana na Birmingham City Football Club ya Uingereza Julai 7,2011.Hayo yatategemea kuthibitishwa baada ya timu ya wataalamu toka Uingereza kuona kiwango cha uwanja na mazingira kiujumla kimichezo baada ya kukagua tarehe 16/05/2011.Kama mechi hio itaridhiwa Birmingham City ita ambatana na mashabiki wasio pungua 1000 watakao jilipia gharama za safari na malazi wenyewe wakati timu itajipatia vijisenti visivyo pungua Dola Million 1.2 na kulala hotel nzuri.
kikosi cha timu ya simba
Mpaka sasa safari ya BCFC kwenda Tanzania haijathibitishwa baada ya ukaguzi ulio pangwa ufanywe tarehe tajwa hapo juu na pia kutokana na ratiba za mechi za hapa ulaya.Baada ya hayo yote kukamilika ndipo safari itathibitishwa.Pia nimetembelea mtandao wa Simba SC (http://simbasportsclub.co.tz/v3/) hakuna taarifa yoyote kuhusu mechi hio sasa sijajua mashabaki tutajua nini kinaendelea maana menu zenyewe hazina maelezo yoyote yaani hata menu iko empty: Mfano events,matches,News hakuna kitu-sijui labda nimeingia sio site yenyewe kuna anayejua anipe site halisi please! maana kama ndio yenyewe bado hatupo siriazi kiukweli maana haina cha maana zaidi ya orodha ya viongozi,wachezaji na historia ya timu!!!!!.Angalieni Yanga http://www.yangasc.com/
Anyways, hongereni Simba kama hio mechi itachezwa na nawatakieni ushindi dhidi ya wazungu!.
soma zaidi hapa:http://www.goal.com/en/news/89/africa/2011/05/03/2469421/birmingham-city-officials-to-inspect-facilities-in-tanzania
: http://www.birminghampost.net/midlands-birmingham-sport/west-midlands-sports/birmingham-city-fc/2011/04/18/birmingham-city-tanzania-confirmed-as-potential-destination-for-pre-season-tour-97319-28542251/

LIMO YA OBAMA MAARUFU KAMA ''BEAST'' YABUMA ZIARANI IRELAND
Gari moja wapo katika msafara wa Obama huko Ireland yabuma baada ya kugonga tuta nje ya ubalozi wa Marekani jijini Dublin-Ireland.Gari hilo aina ya Cadillac la Mr Obama lenye jina maarufu kama ''The Beast'' Yaani 'Mnyama' kwa kimakonde lilisekana kubeba wataalamu wa ulinzi katika msafara huo wakati Rais wa Marekani Barack Obama akiwa ziarani nchini humo jana tarehe 23/05/2011.
Umati mkubwa wa watu umeshuhudia tukio hilo 'live' ambapo mlio mkubwa ulitokea baada ya chesis lake kugusa tuta na kushindwa kwenda mbele na muda si mrefu waliletewa gari lingine kuendelea na msafara.

Kama uonavyo kwenye video hapo juu hicho ndicho kilichotokea.Limo/The Beast hilo lina urefu wa futi 18 na uzito wa tani 8 na upana wa chuma cha bodi wa inch 8 halipitishi bomu wala risasi na lina lina oxygen yake ndani.Rais Obama akiwa ndani ya hilo gari nick name yake inakua Cadillac one na sio The Beast. The beast inasemekana kua na camera kila kona,shotguns na vingine vingi kwa ulinzi zaidi
Mafundi wakinasua The Beast iliponasa
The Beast katika mchoro
(chanzo:dailymail)
23 May, 2011
UNAIKUMBUKA HII??
Hiki kiatu kilikua maarufu sana zamani siku hizi sikioni tena sijui bado kinavaliwa? Na kama kinavaliwa sijui utaanguka mara ngapi kwenye hizi barabara zetu? Hiki huvaliwa na suruali yake (hasa draft) ambayo ni pana kwa chini nyembamba karibia kubana fulani kwenye magoti.Si kila mtu alikua na kiatu kama hiki jina kama sikosei ni Laison (kama kuna jina lingine usisite nitafurahi kulijua). Pia sikumbuki ni miaka gani ila zamani niliweza ona watu wachache wanavaa na ilikua fashion by then.Wewe je umewahi kuona hiki kiatu? je kina kukumbusha nini??
21 May, 2011
ATI UMASIKINI WA TANZANIA NI LAANA???
Hebu sikiliza mjadala huo hapo chini na useme mtazamo wako kama ni laana au tunajitakia kua masikini? je kila mmoja wetu katika jamii tunayo ishi anawajibika kwa nafasi yake au ndio tunanyoosheana vidole kuonyesha kijibanzi kwenye jicho la jirani wakati sisi tuna boriti machoni mwetu? Penye wengi hapa haribiki neno, maswali ni mengi ila kwa sasa tuangalie haya kwanza kama ni laana,tunajitakia,hatuwajibiki,hatuja wezeshwa,uzembe,bora liende,aliye shiba hamjui mwenye njaa au ndio niseme kama wanavyosema kwetu kule ''TUNGAYA SIDA'' YAANI HATUNA SHIDA KABISAA YAANI YOTE SAWA TU?? SEMA USIKIKE!!!
SEHEMU YA KWANZA
SEHEMU YA PILI
CHANZO:MWANAKIJIJI
20 May, 2011
DOLLAR MILLION 6 ZAMUOKOA
Hatimaye aliyekua Mkurugenzi wa IMF Dominique Strauss-khan akubaliwa kutoka rumande kwa dhamana ya Dollar Million 6 ( $6m) na masharti makali ikiwemo kua chini ya ulinzi kutoka kampuni binafsi kwa gharama ya Dollar laki mbili kwa mwezi ambazo ni juu yake,kuwekwa chombo cha kisasa mguuni kitakacho onyesha alipo kwa saa 24 kila siku,kufungwa kwa video camera katika nyumba atakayo kaa na alarms kumzuia asitoke.
Mheshimiwa huyo ambaye mpaka sasa amejihudhuru wadhifa wake kama Mkurugenzi wa IMF kwa takribani miaka minne kutokana na kashfa ya kutaka kubaka mhudumu wa hotel huko Marekani,ataachiwa na kwenda kuishi kwa muda katika nyumba ya muda ambako mkewe Heiress, Anne Sinclair, mwanahabari na Millionea wa kifaransa amempangishia wakati akisubiri kesi yake kusikilizwa hivi karibuni.
Zaidi soma hapa kwa kiingereza: http://www.dailymail.co.uk/news/article-1388834/Wife-daughter-disgraced-IMF-boss-arrive-court-appeal-bail-hearing.html#ixzz1MrCCmdJV

19 May, 2011
VIJISENTI VINAPOSHINDWA KUKUSAIDIA..
Mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF) bwana Dominique Strauss-Kahn ambaye pia ni mwanasheria,mwanasiasa na mwanauchumi wa kifaransa amewekwa jela Marekani kufuatia madai ya kutaka kumbaka mhudumu wa Hotel (Hotel Maid).Baada ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kufuatia kitendo hicho bwana Strauss-Kahn kupitia mwanasheria wake aliomba aachiwe kwa dhamana ya (vijisenti) Dollar Million moja ($1m) mahakama ilikataa dhamana hio na kumrudisha rumande.
Aliyekua mkurugenzi wa IMF-Dominique Strauss-kahn
Kufuatia skendo hio mkuu huyo wa IMF amelazimika kujiuzulu wadhifa wake ambapo Umoja wa nchi za Ulaya (EU) wamesha tangaza kinyang'anyiro na wagombea wa awali ni kama ifuatavyo:-
Mohamed El-Erian, Egypt
Stanley Fischer, Israel
Gordon Brown, UK
Kemal Dervis, Turkey
Peer Steinbrueck, Germany
Montek Singh Ahluwalia, India
Christine Lagarde, France
Agustin Carstens, Mexico
Trevor Manuel, South Africa
Axel Weber, Germany
Aliyekua mkurugenzi wa IMF-Dominique Strauss-kahn
Kufuatia skendo hio mkuu huyo wa IMF amelazimika kujiuzulu wadhifa wake ambapo Umoja wa nchi za Ulaya (EU) wamesha tangaza kinyang'anyiro na wagombea wa awali ni kama ifuatavyo:-
ETI JUMAMOSI TAREHE 21/05/2011 MWISHO WA DUNIA???!!
Imeripotiwa kutokea wahubiri wa kidini jijini New York-Marekani kufuatia wanacho dai mwisho wa dunia ni tarehe 21/05/2011 ambayo ni siku ya Jumamosi.Wahubiri hao ambao wamekua wakifanya kazi hio bila kuchoka wametoa vielelezo mbali mbali kuthibitisha tukio hilo.Zaidi wamedai tukio hilo si lazima litokee wakati mmoja duniani kote kufuatia kutofautiana masaa lakini lazima iwe tarehe iliyo tajwa!!
Ni matumaini yangu hayata tokea yale ya Kibwetere wa Uganda kuchoma moto waumini wake wanao sadikika kufika 1000 ndani ya kanisa la '' Amri kumi za Mungu'' eti mwisho wa dunia umefika na kubaki yeye na bosi msaidizi wake Bi Credonia Mwerinde nje mnamo Machi 17 mwaka 2000.Hata hivyo mpaka sasa haijulikani kama Kibwetere na mwenzie wapo hai na polisi wa Uganda kwa kushirikiana na wale wa kimataifa (Interpol) bado wana mtafuta Kibwetere popote alipo Duniani. Pamoja na kua na maswali mia nane kidogo mie yangu macho!!
Kwa habari zaidi soma hapa:http://uk.news.yahoo.com/preachers-prophesying-end-world-york-000338169.html
Zaidi kuhusu Kibwetere soma hapa:http://www.culteducation.com/kibwetere.html

18 May, 2011
50 CENT IS BACK, ANAKWAMBIA ''DIAL 911''
NB:****SONG CONTAIN STRONG LANGUAGE,PLEASE BE WARNED****
17 May, 2011
15 May, 2011
BAFANA BAFANA 1 TAIFA STARS 0
Timu ya Taifa ya Africa kusini maarufu kama Bafana Bafana au Boys Boys or Go Boys Go Boys jana Jumamosi ya tarehe 14/05/2011 imeibanjua Taifa Stars ya Tanzania 1-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.Bafana Bafana ilijipatia goli lake hilo kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake Siyabonga Sangweni (29) jezi namba 44.Hilo ndo lilikua gori pekee lililo ipa Bafana Bafana ushindi mpaka mwisho wa mchezo
Habari zaidi za mechi hio bonyeza link:
http://supersport.com/football/bafana/news/110514/Bafana_defeat_Taifa_Stars
Man of the match Siyabonga Sangweni
http://supersport.com/football/bafana/news/110514/Bafana_defeat_Taifa_Stars
10 May, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)