05 September, 2011

ETI 'VAT' MAANA YAKE VATICAN?????

Kipande hiki cha video kimeeleza mambo kadha wa kadha yenye wasiwasi kama sio upotoshaji eti VAT ambayo ni 'Value Added Tax (Kodi ya Ongezeko la thamani) kama 'Vatican' na watu wanaitikia? Mwl.Nyerere apondwa eti alikua kiungo muhimu wa makanisa na alifanya maisha kuwa magumu na mzee Ali H Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa afagiliwa.Sambamba na hayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimedaiwa kuwa ni chama cha makafiri na kama yeyote aliye serikalini au CCM ngazi yeyote ana swali basi huyu jamaa yupo tayari kujibu.Aidha kanisa katoliki limetajwa kubomoa uislam(udini wa nini Tanzania?)

Kwa mengine mengi sikiliza hii clip ni ajabu na nimeshindwa kushangaa labda sijaelewa sikiliza na wewe mpenzi msomaji wa kibaraza hiki
No comments: