08 September, 2011

HII BADO NI CHANGAMOTO KUBWA KWA SERIKALI

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay akikabidhi ambulansi ya "kisasa" aina ya bajaj kwa mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dk Rajab Rutengwe (kushoto). Ambulansi za miguu mitatu zimesambazwa na serikali kusaidia kutoa huduma za afya vijijini ambapo mkoa wa Rukwa utapokea miguu hii mitatu 20. Picha na Hamza Temba!!! 

Maswali:
>>Je huyo mgonjwa atapataje huduma ya kwanza?
>>Je dereva atakua daktari/muuguzi ama?
>>Je kwa barabara tulizo nazo hii miguu mitatu  inakidhi kiwango?

Maoni:

>>Serikali tunashukuru kwa kutoa huduma ambayo ni tatizo sehemu nyingi Tanzania lakini hii haikidhi mahitaji kwa karne hii ya 21 bila kusahau miundombinu yetu ambayo bado sio mizuri sehemu nyingi.

>>Ni bora zinunuliwe gari hata za kawaida (kama lengo ni kubana matumizi of which sina hakika kama hizo bajaji ni bei ndogo!) japo kufikisha mgonjwa hospitali ila sio pikipiki kwani ni rahisi mgonjwa kudhurika na jua,mvua (utelezi wa barabara kipindi cha masika), vumbi,au hata ajali kwani ni rahisi kupata ajali kwa pikipiki kuliko gari.

>>Kununua pikipiki kama nyenzo ya kusafirishia wagonjwa wakati wewe unatembelea  Landcruiser V8 (4.7Litre posh and expensive) hakuleti picha nzuri kwa wapiga kura na walipa kodi kwa ujumla au kwa maneno mengine serikali haijali wananchi ambao wameipa ridhaa ya kuwatumikia kwani hata 
matunda ya kodi zao hayaridhishi!


Free Thinking aka Mpayukaji  naye katoa  maoni yake kuhusiana na changamoto hii yasome  HAPA

No comments: