10 November, 2011

TANGAZO: WANACHAMA ZANZIBARWEBSITE MNAOMBWA KUZINGATIA.


Nachukua fursa hii kukusalimuni nyote wanaukumbi.
Hapa,Zanzibarwebsite ni pahala panapowaunganisha wazungumzaji Kiswahili popote walipo duniani.
Hilo ndio lengo mama.
Mengine kwa kupitia lugha yetu hii unapata haya yafuatayo:
  1. Kujifunza taaluma mbali mbali kupitia kwa wenzako waliokuzidi.
  2. Kujipatia taarifa mpya na zilizopita
  3. Kujipatia Rafiki /Shoga
  4. Kukutanisha na wenzako ambao mlipoteana kwa masiku.
  5. Kujiliwaza kwa picha/habari/mazungumzo/muziki n.k
  6. Kutumia uhuru wako wa kusema ( freedom speech) na kusikilizwa.
Hili la 6 - Ndio la kuwa makini - UHURU WAKO isiwe ukajisahau kutoheshimu UHURU WA WENGINE.
Ili kulinda mipaka ya uhuru wa wengine na wako mwenyewe ilipaswa haya yafuatayo uzingatie:
  1. Heshima na Nidhamu- usiropoke matusi makavu makavu.
  2. Usilete mas-hara ya kuchupa mipaka ya kumuingia mtu maungoni - kiasi cha mtu kujiona amedhalilishwa ama kudharauliwa.
  3. Epukana na Ubaguzi wa aina yeyote iwe rangi/jinsia/kabila au wakimajimbo.
  4. Uwe tayari kutoa mchango ili na wewe uchangiwe  mawazo.
  5. Uwe tayari kukosolewa pale unapokosea.
HAYA YAKIZINGATIWA NA KUFANYIWA KAZI - Zanzibarwebsite will be the place of leisure,educative,harmony and more communicative one rather than others.
Shime wadau- HESHIMA NI KITU CHA BURE
Babengwa wa Upendo.
Zaidi watembelee  Zanzibarwebsite

No comments: