05 May, 2010

Lack of sleep 'linked to early death' wana sayansi wamesema!

Inasemekana kulala chini ya masaa sita si nzuri kwa afya yako na inapelekea mtu afe mapema. Wana sayansi hao wametoa ripoti hio baada ya kufanya tafiti 16 zilizo husisha watu/washiriki 1.5 million. Ripoti inasema 12% ya watu wanao lala chini ya masaa 6 wapo kwenye hatari ya kufa mapema zaidi kuliko wale wanaolala muda ulio shauriwa kulala.

Hata hivyo kulala zaid ya masaa 9 imehusianishwa na kudhoofika kwa afya. Hii ina maana kulala sana pia kuna pelekea kufa mapema (Professor Francesco Cappucio head of the Sleep, Health and Society Programme at the University of Warwick) amesema.

Wana sayansi hao walimaliza kwa kusema kadri siku zinavyo kwenda watu wengi wamekua wanachelewa kulala kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kujishughulisha zaidi na kazi kwa masaa mengi kutokana na msukumo wa kijamii katika swala zima la kutafuta na kumudu maisha ambayo yamekua magumu siku hadi siku. Ripoti imetolewa baada ya kujumuisha tafiti 16 zilizo fanyika UK, US, EUROPE na ASIA na kutumia zaidi ya watu 1.3 Million.

Aidha watu laki moja wame ripotiwa kufa kutokana na sababu za kutolala kwa muda unaotakiwa ama kulala sana kupitiliza muda ulio shauriwa.

Hapa lile kundi la walevi aka wanywaji au walipa kodi wakubwa kupitia pombe wako hatarini kwa sababu unakuta mtu anakunywa hadi usiku wa manane wakati huo huo asubuhi anaingia kazini.

wale wakusoma mashuleni(wale wakusoma & walimu), dukani kuuza( wafanya biashara)Internet cafe (wale wanaomiliki ama kufanya kazi aina hizo za ofisi) bila kusahau wanao penda kuchat kwa muda mrefu (msiniseme LOL..), wahudumu sehemu mbalimbali za huduma za kijamii kama Guest house, Hotels,Bar, Night/late Clubs,casino na nyingine nyingi sana waweza zitaja

Niliwahi andika article ya the Value of time nadhani inaweza kua suluhisho kwa wanao kesha bila sababu za msingi na hatimaye kuto lala vizuri kwani hakuna bank ya kuweka muda eti nitautumia baadae, hio haipo cha msingi ni kupanga mambo yako vizuri ili ikifika saa ya kulala ulale!.


unaweza soma zaidi yahoo uk news on Lack of sleep 'linked to early death'

No comments: