28 May, 2010

Scholarship Scams!!!:

Following the fast ever growing number of scholarship seekers worldwide and based on the means through which adverts are being made on scholarships. Scholars MUST bear in mind that, not all scholarships information/correspondences/emails are genuine. This should be understood from the very beginning of any process in this context that, since a scholarships is a NEEDY thing, an illegal plan for making money (SCAM) is so prevalent and linked to both true and fake scholarships. So today I’m giving you some things that you should be skeptical in pursuit of scholarships.

Firstly, be skeptic on any request for Personal Information: Some scams ask for your personal details. For example: bank statements, date of birth, passwords, account numbers etc. NEVER share any of your personal information with anyone online!.

Secondly, Watch out application fee: Scholarship scammers might act as organizations that charge fees for availing procedures or application submissions that could be undertaken for free!. Again NEVER pay for scholarship application fees!!!!!!!!!!!!!!!! Chunga vijisent vyako!!!!.

Thirdly, questioning every now and then is sometimes not good, BUT for this one you’ve to question every single thing, You MUST question "Winnning" a Scholarship that You Never Applied!!!!: Scholarships scams may contact college/University students informing them that they have won full scholarship. You cannot win a scholarship if you have never applied for it before! Never on Earth!!. A bit of linking this with DAILY scams in our inboxes….at least every day I receive an email like this ‘’you’ve a won a sum of 75,000£’’ give us your details so that we can process it for you (example only).The question here is, how can you win without doing the LOTTERY thing??????

Fourthly, be skeptic on any guaranteed scholarship award: Scams that guarantee an award focus mainly on trapping tempted students. Nobody can guarantee a scholarship. . Don't get into the trap commonly known as 'Scholarship guarantee'. Nothing of the sort exists on Earth except SCAMS!

Fifth and last, there is NO Free Scholarships: How? Nothing comes so easily and for free. No such thing like free Scholarships. This means Scholarships are generally given to students with genuine and asked academic records. UNLESS YOU WANT TO BUY A DEGREE, which I’ve no comment at this point in time!.

NB: As a scholarship aspirant you MUST research around meticulously on the funding procedures IF ANY!! Or else at least every scholarship seeker is at risk of being a prey to any scholarship scam.

26 May, 2010

School of History MA by Research Fees-only Scholarship,The University of Leeds,UK

The School of History Masters Scholarship is for full fees at the UK/EU rate.

Eligibility:

All of the following are available to UK, EU and International postgraduates applying to study in the School of History.

In order to be eligible to be considered for these scholarships, you must:

•have applied, and received an offer, for a place in the School of History
•have supplied us with copies of transcripts from previous degrees and one academic reference by the deadline of 4pm on 30 June 2010
•have fulfilled our entry requirements before official acceptance of any scholarship
•be starting your course in the next academic year (2010/11)
not already have an MA in History.


Read more:http://www.leeds.ac.uk/history/prospective/pg/school.htm

Namna ya kutafuta Scholarships

Ukiingia kwenye website ya chuo chochote kile kuna mahali kuna ‘search box’ andika pale ‘scholarships’ then search itakuletea scholarships nyingi tu (kama zipo). Kuna watu wanadhani mie chizi kulundika websites nyingi za vyuo mbalimbali vya hapa UK na Tanzania.Lengo langu kubwa hapo ni hilo,si mara zote nitakua na habari za scholarship tena ‘ IN TIME’ na nije kuzi post hapa bloguni.Pia ieleweke kwamba hizi scholarships nazi post nikipata ‘MUDA’ Kwahio nina uhakika kuna scholarships nyingi zinanipita!!

Kwahiyo basi, kama upo kwenye website ya chuo kilichopo USA ama sehemu nyingine yeyote duniani fata procedures hizo hizo kama kuna scholarships utaziona. Ukiziona angalia ‘eligibility’ (nchi zipi zimetajwa kama ndio wawe waombaji?) Mfano unaweza ona scholarship ipo specific ‘For UK/EU only. (hii haikuhusu unless una makaratasi ya UK/EU).

Ukiona ‘International Scholarship for any Developing Countries’ basi omba fasta kwani Tanzania ni moja wapo ya nchi zinazo endelea aka Developing Countries.Kuna scholarships nyingine ni very specific mfano: Ni Edinburgh University hua wanatoa scholarships kwa Heshima ya Mwl.Nyerere tena ‘For Tanzanians only’ Ukiona hio omba pia na uzingatie maagizo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata kwani waombaji ni wengi sana.

NB1: Scholarships ni kinyang’anyiro cha hali ya juu sana waombaji ni LAZIMA wazingatie vigezo /maagizo/maelezo yaliyo tolewa tena kwa umakini wa hali ya juu. Vile vile zingatia muda (Deadlines) kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata. Imagine unakuta ‘scholarship for any African student’ maana yake the whole of Africa wanafunzi wote wenye sifa wataigombea hiyo nafasi hata kama ikawa iko moja tu.

NB2: mwenye taarifa za uhakika kuhusu scholarships popote pale anitumie kwenye e-mail (rijaki@ymail.com) nita zipost.Ni hayo tu kwa leo.

21 May, 2010

Scholarships za leo

Edinburgh Global Development Academy Master’s Scholarships, UK
Description : The University of Edinburgh will offer 2 full Master’s scholarships for students from less developed countries and 2 partial Master’s scholarships for UK/EU students for eligible Master’s programmes offered by the University.
Scholarships will be available for students pursuing one of the following Global Development Academy programmes:

• MSc Africa and International Development
• MSc Environment and Development
• MSc Science, Technology and International Development
• MSc Multilevel and Regional Politics

Each full scholarship will cover the overseas rate of tuition fee, a maintenance allowance of £10,000 and return flights. Each partial scholarship will cover the UK/EU rate of tuition fee only.

Eligibility The full scholarships will be awarded to students who are accepted for admission onto an eligible Global Development Academy programme at the University of Edinburgh. Applicants must be both nationals of and resident in the following countries mentioned on the site.
Criteria

The scholarship will be awarded on the basis of academic merit. Candidates must have, or expect to obtain, a UK first class or 2:1 Honours degree at undergraduate level or the international equivalent.

Application Procedure
Candidates should have applied for postgraduate admission and received an offer of admission on one of the Global Development Academy programmes before making an application for an Edinburgh Global Development Academy Master’s Scholarship.
Eligible applicants should complete an online scholarship application at http://www.scholarships.ed.ac.uk/postgraduate/apply/online.cfm
Completed application forms must be received by the Scholarships and Student Finance Office no later than 31 May 2010.
Selection Procedure

A Selection Committee will meet in late June 2010 to select the scholarship holders. The winners of the scholarships will be announced by the end of June 2010.

MSc in Investment Analysis Scholarships – Karen Napier Scholarships, University of Stirling-UK)
Job Description :The Karen Napier Scholarships are generously funded by the Karen Napier Charity in memory of Karen, a graduate of the MSc in Investment Analysis. Each Scholarship will meet the course fees at the Home/EC rate and will offer £3,500 toward maintenance. In addition, the Accounting and Finance Division will waive the remainder of the course fees in the event that a Scholarship is awarded to an overseas fee paying applicant.

Who can apply?
Applicants may be of any nationality and must hold or expect to obtain an offer of a place on the full time MSc in Investment Analysis for entry in September 2010. Applications may be submitted for the Scholarships along with the course application, but only those obtaining a place on the course will be entered into the Scholarship competition.

How to apply
• Complete the Karen Napier Scholarship application form, (pdf document 24kb) at http://www.accountingandfinance.stir.ac.uk/apps-postgrad/scholarships/documents/MScIAKarenNapierScholarshipForm.pdf ensuring that all sections are answered legibly.

• Pay particular attention to the section which requires a handwritten statement of approximately 500 words on why a Scholarship would help you, and what your career or educational aims are for the five year period after you graduate from the Investment Analysis course.

• The closing date for receipt of applications is 30 June 2010.
• Please note that the Scholarships will be allocated in July and therefore if you are applying both for the Scholarships and the Investment Analysis course close to the 30 June deadline, you should ensure that your course application is completed legibly
(http://www.accountingandfinance.stir.ac.uk/apps-postgrad/scholarships/InvestmentAnalysisScholarships-KarenNapier.php)


MSc in Finance Scholarships - Divisional Scholarships
(University of Stirling-UK)

These Scholarships are funded by the Accounting and Finance Division and meet course fees up to the home/EU rate. This means that the successful candidates will pay no course fees in September 2010 if they are home/EU fee category students. Overseas fee paying students are also encouraged to apply and would pay the difference between home and overseas fees.

Who can apply?
Applicants may be of any nationality and must hold or expect to obtain an offer of a place on the full time MSc in Finance for entry in September 2010. Applications may be submitted for the Scholarship along with the course application, but only those obtaining a place on the course will be entered into the Scholarship competition.

How to apply
Complete the MSc Finance application form (pdf document 17kb) At http://www.accountingandfinance.stir.ac.uk/apps-postgrad/scholarships/documents/MScFinanceScholarshipForm.pdf ........
ensuring that all sections are answered legibly.

• Pay particular attention to the section which requires a handwritten statement of approximately 500 words on why a Scholarship would help you, and what your career or educational aims are for the five year period after you graduate from the Finance course.

• The closing date for receipt of applications is 30 June 2010.
• Please note that the Scholarships will be allocated in July and therefore if you are applying both for the Scholarships and the Finance course close to the 30 June deadline, you should ensure that your course application is complete.

Scholarships for International students
(Westminster University-UK)

Full International Scholarships
Amount: Full tuition fee waivers, accommodation, living expenses and flights to and from London. The scholarship will be renewed each year, subject to satisfactory academic progress.

Eligibility: You must be an international student from a developing country and hold an offer for a full-time undergraduate degree at the University.
Criteria: Academic excellence, development potential and financial need.
Deadline: 31 May 2010.

Diplomatic Scholarships
Amount: 65% fee waivers.
Eligibility: These scholarships are available to you if you are a child of diplomats from developing countries, whose countries are unable to contribute to the fees. Your parent in the diplomatic post must be based in the UK, and you must hold an offer for a full-time undergraduate degree at the University. The scholarship is for the length of the course (3 or 4 years) and is subject to satisfactory academic progress. These scholarships are limited in number and are competitive.

Criteria: Academic excellence.
Deadline: 31 May 2010.

Part Fee Waiver Scholarships
The University offers a number of part scholarships (£2,000 fee waiver) to you if you are an exceptionally well qualified student from outside the UK/EU.
These will be for each year of the undergraduate degree, subject to satisfactory academic progress. In the case of courses with a placement year, no scholarship is payable in that year as the University does not charge fees.

Amount: £2,000 fee waivers.
Eligibility: You must be an international student and hold an offer for a full-time undergraduate degree at the University.
Criteria: Academic excellence.
Deadline: 31 May 2010.

EHWLC International Business Programme Progression Scholarship
This scholarship will be for each year of your undergraduate degree, subject to satisfactory academic progress. In the case of courses with a placement year no scholarship is payable in that year as the University does not charge fees.
Amount: £2,000 fee reduction

Eligibility: You must be an International student (non-EU) on the International business programme at Ealing Hammersmith and West London College and hold an offer (conditional or unconditional) of a full time undergraduate degree at the University of Westminster.

Criteria: Academic excellence
Deadline: 31 May 2010
Read more at:- http://www.westminster.ac.uk/study/fees-and-funding/scholarships/undergraduate-scholarships#international

Contact Us
General enquiries
309 Regent Street
London
W1B 2UW
Tel: +44 (0) 20 7911 5000
Course enquiries
Tel: +44 (0) 20 7915 5511
Email: course-enquiries@westminster.ac.uk
International office
Tel: +44 (0) 20 7911 5769
Email: international-office@westminster.ac.uk

20 May, 2010

Walofukuzwa kazi baada ya kuandika udaku facebook!!

Kama nilivyo ahidi kutoa mwendelezo wa 'Namna ya kufukuzwa kazi kwa kutumia facebook'' leo nawaletea baadhi tu ya walio fukuzwa baada ya kupatikana wameandika 'udaku' facebook tena bila kufikiri kama siku hizi ma-boss hawako nyuma kupitia mitandaoni kujua yanayo jiri.Siku hizi unaweza itwa interview wakati wameshakusoma mambo yako yote ya facebook sasa wale tunaopenda kujiachia huko unaweza jikuta unakosa kazi. Haya tujiunge kupata habari za waliofukuzwa chanzo kikiwa facebook!!

Msichana mmoja aitwaye Ashley Johnson ,22 huko North Calorina kafukuzwa kazi baada ya kuandika udaku facebook.Msichana huyo alisema wateja ambao yeye anaita ‘WA BEI RAHISI’ kwa kimatumbi ‘CHEAP CUSTOMERS’ wamemkalisha kwa saa moja zaidi ya muda aliotakiwa kumaliza kazi na baadae kumpa shukrani maarufu kama ‘tip’ ya $5.

Mwanadada huyo mhudumu wa Brixx Pizza alikasirika kwa kupewa 'tip' ndogo hata akadiriki kuwaita CHEAP wateja na kutaja na jina la mgahawa huo kama status message yake facebook.Bahati mbaya mdada huyu hakujua kama waajiri siku hizi wanapitia Facebook kusoma soma yaliyojiri.Hivyo dada huyo yakamkuta siku chache baadae baada ya meneja wake kuona alichoandika facebook ikiwa ni moja ya vitu ambavyo mfanyakazi huyo kakiuka kwani kawasema vibaya wateja, na kukiuka sera ya biashara ya mgahawa huo ikiwa ni pamoja na kuchafua jina kibiashara kwa jamii ya watumiaji wa mahali hapo . Hata hivyo mdada huyo baada ya kufukuzwa aliomba msamaha na hivi sasa yuko mbioni kutafuta kazi mpya.

Hii imefanya idadi ya wanaofukuzwa kutokana matumizi ya facebook kua kubwa siku hadi siku.Mfano mfanyakazi wakike (31) wa shirika la bima inchini Uswisi mwaka jana (2009) alifukuzwa kwa kubainika kutumia facebook akiwa kaomba ruhusa kua ni mgonjwa hawezi tumia computer siku hio kwani mwanga una msumbua. Zaidi soma hapa http://www.reuters.com/article/idUSTRE53N4JF20090424.

Sambamba na hio Kimberely Swan (16) mwanzoni mwa mwaka (2009) alifukuzwa kazi kwa kuandika facebook kama kazi inaboa na kuguna kwa sana tu. Zaidi soma hapa http://www.dailymail.co.uk/news/article-1155971/Teenage-office-worker-sacked-moaning-Facebook-totally-boring-job.html .

Si hao tu bali, Dan Leone mnamo April 2009 aliandika facebook kumkashifu mwajiri wake na baada ya kujua kama lilikua kosa alifuta mara moja ila kwa bahati mbaya haikusaidia. Hatimaye siku chache baadae alipigiwa simu kama kafukuzwa kazi. Zaidi soma hapa http://sports.espn.go.com/nfl/news/story?id=3965039.

Mnamo mwezi wa nane mwanamke mmoja mwenye asili ya kiingereza adaiwa kufukuzwa kazi baada ya kuandika facebook ‘’kazi inaboa’’ asikumbuke kwenye friends list yuko boss wake zaidi soma hapa http://stupididiotjerk.com/2009/08/12/another-person-gets-fired-due-to-facebook/ mwaka 2008 kijana kyle doyle wa Australia alifukuzwa kazi kwa kuomba likizo ya kuumwa. Baada ya kejeli za facebook aliombwa cheti cha matibabu aliposhindwa kutoa na kazi ikaishia hapo hapo.Zaidi soma hapa http://bb.nsmb.com/showthread.php?t=116471

Hawa ni baadhi tu ya waliofukuzwa kazi kutokana na kujiachia na facebook. Hata hivyo mijadala mbalimbali mitandaoni imethibitisha kua idadi kubwa ya watumiaji wa facebook ni wafanyakazi kwani ofisi nyingi zina Internet.Hivyo hiyo imepelekea wale wenye facebook accounts kua bize sana wakiwa kazini kwani pamoja na mambo mengine ni lazima wapitie facebook kuchat ama kuangalia yaliyo jiri pamoja na marafiki zao ama kuandikiana meseji.

Utafiti uliofanywa na Nucleus mwaka 2009 upo kama hivi:-

Facebook Usage At Work

Information-----------------------------------% of Respondents

Workers with a Facebook account--------------------77%
Facebook users that access Facebook at work-------61%
Workforce accessing Facebook at work---------------47%
Average minutes accessed per day---------------------15

Total lost productivity to Facebook across the entire employee population 1.47%

(Source: Nucleus Research, July 2009)

Na mwisho kabisa utafiti uliofanywa na Family attitudes hapa Uingereza umebaini kwamba facebook kama ni mtandao uliopendwa zaidi na wasichana kwa asilimia 40 ukilinganisha na wavulana kwa 6%. Katika utafiti huo wasichana walipo ulizwa wataje vitu vitatu muhimu sana kwao katika maisha, waliweza taja ,MARAFIKI,FAMILIA, FACEBOOK NA MSN.Wakati huo huo wavulana walitaja cha kwanza FAMILIA,MARAFIKI NA PESA. Je kwako wewe msomaji ungetaja nini kiwe cha kwanza? Na je iitwe Fail book kama ambavyo watu wameanza kuiita au ibaki kua Facebook??

Gari za kukodi..

Hivi wale jamaa wanao kodisha magari hua wanakagua magari yao kabla na baada ya kukodisha? Duh kama mambo yenyewe ndio haya kazi ipo.Au ndo cha mtu ma**!!!





19 May, 2010

Utani wa kijinga!!!

Radio Dj mmoja wa shirika la utangazaji BBC kituo cha jijini Birmingham jumatatu ya tarehe 17 mchana aliropoka na kusema Malikia kafariki dunia.Kama haitoshi inadaiwa kua Dj huyo alipiga wimbo wa taifa kusindikiza tangazo lake.Mtangazaji huyo kwa jina Danny Kelly, 39 amekiri kukosea tangazo na kuomba radhi kwani alikua na tangazo tofauti na maalumu kwa wasikilizaji wake ambalo lilimfanya amtaje Malikia bila kukusudia.

Habari zaidi zinasema Dj huyo amekiri kukosea tangazo muda mfupi baada ya kutangaza na hatimaye kuomba radhi kwa wasikilizaji na kwa mhusika mwenyewe.Baadae shirika kubwa kabisa la utangazaji hapa Uingereza liliomba radhi pia kwa kosa hilo ambalo limechukuliwa kama ni utani alio ufanya mtangazaji huyo dhidi ya Malikia.

Hata hivyo inadaiwa mtangazaji huyo ni mahiri kwa kuchekesha wasikilizaji wake kwa kufanya utani mwingi katika vipindi vyake au status message ambazo amekua akiandika kwenye mtandao wa kijamii maarufu kama facebook.Vyombo vya habari vimesema BBC imemsimamisha kazi kwa muda wa wiki moja na pengine hatua zaidi zikachukuliwa dhidi yake kwa kosa alilofanya.

Money is not a problem, the problem is how to use it!

Muziki unapotumika kutoa ujumbe ambao kila mtu aweza kua na mtazamo tofauti.Huyu anasema money is not a problem, problem how to use it..je ni kweli? unaweza jiuliza unavyotumia pesa zako kama ni sahihi ndo zinavyotakiwa kutumika? Hapa najua kila mtu atakua na jibu lake kutokana na kuwepo mitazamo tofauti.Hata hivyo usawa wa matumizi ya pesa kwa kila mtu ni vigumu kuutaja kwani kila mmoja anaona halali kulingana na matakwa yake yanavyo weza kutimia vile atakavyo.

Tuwekee mfano yule mwanamme/mwanamke anayetumia pesa zake kuhonga mwanamke/mwanaume na kufanya nae mapenzi tena BILA KINGA kwa kiburi cha pesa zake na kwa makusudi kabisa kumwambukiza ugonjwa (UKIMWI) mtu mwingine, je ametumia pesa zake sawa? hapa jibi litakua HAPANA! JE anaye honga wanafunzi na kuwapa MIMBA? (hapa ni vijana na mijibaba) Vipi kuhusu Mijimama (samahani) inabidi tu niseme! inayo honga vijana wadogo aka serengeti boys na kufanya nayo hayo wanayo yafanya? .tena wengine wakishapata hio mishahara walio sotea kwa sana kinachofuata ni kulala BAR.Nadhani wale wanaoijua Bia moja Tz aina ya Bingwa wakati inaingia watu wengi walilazwa hadi mahospitali maana ile ukinywa kama safari utajua maana ya pombe nini.Sijui bado ipo! na kama ipo ni wazi watu wanaiogopa maana wengi iliwafanya mbaya hasa walimu.

Ntombi (ni jina la mwanamziki sio tusi kama unavyotaka kufikiri lol!) anasema Money is not a problem , the problem is how you use it..je wewe unasemaje kama ukiulizwa?
sambamba na hio angalia video hii watu walivyo changamka na usiite walevi utapigwa bure ita walipa kodi wazuri aka wanywaji!!



Sina mengi sana kwa leo ila tu jiulize kama matumizi yako ya pesa ni sahihi ama sio sahihi.Tena wengine bila aibu unakuta anatumia hata kuzidi bajeti aliyo nayo.Kama ni mfanya kazi ataacha kua mla rushwa kweli mtu wa namna?? Na kama ni mfanya biashara je ataacha kufanya biashara Haramu?.Kama matumizi yanazidi kipato wapi atafidia kama sio njia za panya/zisizo halali?.

Pamoja na yote haya bado nchi kama Tanzania imeendelea kua na tatizo la mishahara midogo kwa wafanyakazi kitu ambacho kina karibisha rushwa kwa kishindo kabisa.Kwani hawa wafanyakazi kama kima cha chini kwa mujibu wa TUCTA kua 315,000/= basi ni wazi rushwa haitaisha. Kwani mnfanya kazi huyu huyu ana majukumu yanayozidi mshahara je pesa atatoa wapi?.Kwa kweli nimecheka kuona hii katuni lakini ina ukweli ndani yake, na si kwamba nimecheka nafurahia ila kuna baadhi ya vitu vina chekesha kama NYUMBA NDOGO ( sio lazima kua na nyumba ndogo kwanini uwe nayo? inachekesha sana kwa kweli mie naita mtu mzima ovyo hata kama ni private life ya mtu!)

Hongera kwa mchora katuni, ebu angalia mwenyewe hio katuni halafu sema kama 80,000/= inatosha chochote. Hata ada tu haitoshi,bill ya umeme? maji? kodi ya nyumba?.yani huyu ndio apewe ofisi aache kufungua bucha?.Sina maana walipwe vizuri ili kumudu nyumba ndogo bali mahitaji ya msingi kama baadhi ya ambayo yameonyeshwa kwenye katuni.ok hata tuseme huyu mtu hana mke still hii pesa haitoshi sasa ana mudu vipi maisha? Hii ni sawa na useme mlinzi analinda bank kwenye mamilioni ya pesa halafu mshahara duni je wezi wakija wakala dili naye nani atalaumiwa? kuna vitu vingine zinatia vishawishi mtu analinda mamilioni halafu analipwa kiduchu yani hio ni sawa na simba kumpa alinde nyumbu!!




Kwahio hapa nimedokeza mambo mawili kwa pamoja ambayo yatafanya ujiulize ni yapi ndio matumizi halali ya pesa tulizo nazo hio mosi, pili,je mishahara tunayo lipa wafanya kazi wetu inakidhi mahitaji ya msingi tukiondoa yale yasio ya lazima?

Namna ya kufukuzwa kazi kutumia facebook!!

Kwa wale waheshimiwa wafanya kazi hii imedaiwa kua ni njia moja wapo ya kufanya uachishwe kazi mara moja na kwa njia rahisi kabisa ya mtandao wa kijamii maarufu kama facebook. Kwa raha zako andika kama inavyoonyesha hapo tena bila kujali kwenye orodha ya marafiki yuko boss wako.kwani boss kitu gani hahahhahahaha lol! kweli dunia inaenda kubaya sasa kuna baadhi ya watu wanaita FAIL BOOK!!!!wewe je utaiitaje??



Baadae nitawaletea wafanyakazi walio fukuzwa kwa sababu mbalimbali zilizo patikana na waajiri kupitia facebook.Kaa mkao wa kula, kibarua kitaota majani ushindwe wa kumlaumu.

18 May, 2010

Matumizi ya simu kwa madereva barabarani

Imekua ni kawaida sana kuona mtu anaendesha gari, pikipiki,ama hata baiskeli huku akiandika meseji kwneye simu yake. Tukichukulia ule usafiri wa umma kama bus na usfairi miwingine kama taxi au Coach, school bus na zingine.Ivi nini wajibu wetu kama abiria unapokua kwenye bus au taxi na kuoana dereva yuko busy na simu huku anaendesha? Busy nina maana kutuma meseji au kuhangaika kupokea simu wakati gari liko kwenye mwendo mkali. Ukiacha yeye mwenyewe kua hatarini kuacha njia anaweza pia sababisha ajali kwa madereva wengine.

Wataalamu wa mambo ya usalama barabarani Virginia Marekani, wamesema kuna asilimia kubwa kwa dereva anaye endesha gari huku akitumia simu ya mkono kupata ajali, au kusababisha ajali kwa madereva wengine wanaotumia barabara wakati huo.Wataalamu hao kutoka chuo cha usafiri cha Virginia, wanasema kugonga au kugongana na gari jingine kuanaweza kutokea wakati wowote wakati dereva anaandika meseji ama kupiga na kupokea simu ya mkono huku akiwa anaendesha gari.



(video za ajali zinazo sababishwa na na matumizi ya simu gari likiwa ktk mwendo).




(dada anayetumia simu wakati anaendesha)

Hizi ziko sana bongo hapo akikugonga anasema samahani bro au sis…mie simuelewi mtu kwa hili !!

Wataalamu hao wanazidi kudai hakuna sheria kamili inayotaja kosa la kutumia simu wakati unaendesha bali ipo tu ya makosa ya jumla mfano: kuendesha gari kwa uzembe barabarani (reckless driving). Ambayo inamtaja mkosaji kua nakosa ya kutojalia usalama wa wengine, mali, hata kuhatarisha maisha.Hivi sasa majimbo kama California, Connecticut, DC, new Jersey, new York, Oregon na Washington wamezuia matumizi ya simu kwa madereva wote sio tu waendesha mabasi na madereva walio chini ya miaka 20 kama ilivyo kua hapo mwanzo.

Hata hivyo kukua kwa teknolojia ya simu kumechangia kwa kiasi kuongezeka kwa ajali za barabarani kutokana na kwamba watu wamekua wakitumia simu wakati wanaendesha. Kwa maana hio kuna haja ya kuanzisha sheria inayo husu matumizi ya simu kwa madereva ili kupunguza ajali za barabarani. Chini hapa ni baadhi ya video zinazo onyesha ajali mbalimbali kutokana matumizi ya simu wakati unaendesha barabarani.

17 May, 2010

Sheria na Alama za barabarani..

Hivi bongo ni lini tutakua na vizuizi katika makutano ya train na barabara za magari? pamoja na kwamba kuna madereva naita wapumbavu kwakutoa zingatia alama za barabarani. Hawa ndio wana sababisha ajali na kufanya ziendelee kuwepo kila siku na kugharimu roho za watu wengine.Angalia huyu kwenye video sijui anawaza nini get limefungwa lakini kapita hivo hivo.Ni muhimu yakawepo kwa wale wasio zingatia alama za makutano ya njia za train na barabara za magari. Hata hivyo wanao kiuka ama kutofata alama za barabarani ni wengi ona huyu angekufa hapo sijui angemlaumu nani. Na pia adhabu iwe kali ili sheria ifuatwe.

Ona huyu yani so stupid! nasikia kuna police traffc hua wanapiga makofi sijui kifungu gani cha sheria kina waruhusu kupiga lakini kwa dereva kama huyu mtu yeyote angeshawishika kupiga japo yeye mwenyewe alikua hatarini kufa au hata kusababisha mauti kwa wengine.Iangalie hii Video uone..




Nimependa sheria ya hapa UK kwani usipo fata sheria una punguziwa points kwenye leseni yako na mwisho kama unaendelea kufanya makosa barabarani basi unakua banned kuendesha.Hii nchi kuna discipline nzuri kwa upande wa ufataji wa sheria dereva mataa anasimama, bongo mataa unakuta jitu limetoka huko taa nyekundu anapita tu kisa kaona hakuna gari upande wa pili. Si wote wanafanya hivyo ila wanao fanya hayo wapo nimewahi ona kwa macho yangu! eti hapo mtu akamatwe umwambie fine 20,000/=
haisaidii kwasababu makosa kama hayo yataendelea kutokea.kwanini utaratibu huu usiwekwe wa vunja sheria za barabarani wakabaki kuendeshwa tu?.Na pia sheria kama ipo basi ifuatwe na kila mtumiaji wa barabara ile bila kujali wadhifa au aina ya gari anayoendesha.

Sasa kichekesho kwa mfano unakuta mida ya foleni asubuhi na jioni mtu mwenye tuseme suzuki vitara kapita service Road basi ata kamatwa na hata kucheleweshwa anakoenda. Wakati huo huo utaona mwingine kakatiza na VX lake anapungiwa mikono tu kana kwamba yule ni mtu zaidi kuliko walipo kwenye foleni. Na hapo usikute hana lolote anawahi zake bar ama nyumba ndogo (mtanisamehe wenye nazo)> Sielewi ile wanaita Equality before law kama inafanya kazi sawa kwa watu wote ama ni kwa baadhi tu hasa WALALA HOI!! Kwasababu kama watu wote wako sawa mbele ya sheria kwanini mwingine tena ukute ni kiongozi kabisa na akili zake anafanya hivyo sasa sijui niseme viongozi wako juu ya sheria ama sheria inatumika tu kwa wasio maofisa?

David Cameron, waziri mkuu mpya wa sasa wa Uingereza aliunga msafara wa foleni kali zinazo zidi kukua siku hadi siku hapa UK bila kujali.Nadhani pamoja na kuhatarisha maisha yake kama walivyodai maofisa wake wa usalama aliweza kuzingatia umuhimu wa watu wake na japo kuonja adha ya foleni hata kwa siku moja tu.Kwani wangetumia ule mtindo wa escort basi foleni ingekua mara mbili zaidi kwani magari yote yangetakiwa kupisha kitu ambacho yeye hakupenda kitokee Soma zaidi hapa http://http//www.dailymail.co.uk/news/article-1278618/Security-fears-Cameron-ditches-police-outriders.html.Si vibaya viongozi wetu wakajifunza kutokana na mfano huo kwasababu kama wewe ni mtu wa watu kweli kwanini ukimbie kimbie na kuwaongezea walipa kodi wako foleni. Inamaana baada ya kuchaguliwa wale walio kuchagua wanageuka kua maadui? Na kwanini uwasumbue kwa kuwaongezea foleni? mimi hii hua naona ni sawa na baba kumpa mwanae pesa akalewe huko akirudi amsumbue tena baba yake kwa kumsemea mbovu, kumtukana ikibidi kumzaba makofi.

Viongozi ni muhimu na raia pia kwani ndio wapiga kura na ndio walipa kodi. Kimsingi katika utawala wa kidemokrasia raia ndio ma-boss na wenye nguvu japo katika nchi zetu nguvu walizo nazo ni kuchagua mtu kukaa madarakani na sio kuchagua anaye takiwa atoke hata muda wake ukiwa haujaisha. sitaki kuongea sana ila tu sheria ifuatwe sio wengine wawe juu ya sheria na kua watu zaidi linapo kuja swala zima la uvunjaji wa sheria. Mwisho kabisa sheria za barabarani ziwekewe utekelezaji mzuri na adhabu iongezwe ili kupunguza ajali za barabarani.Ni hayo tu kwa leo

LATEST NOKIA!!!!

Hapo lazima picha itoke very clear kama ya studio siunajua mega pixel hapo zimezingatiwa NOT LESS THAN 12 meg.pixel.....dah imenikumbusha mbali sana... zamani kulikua na siemen portable kabisa kama hio ukiwa nayo full RESPECT !!! sijui bado kuna watu wanatumia mmmh ..ivi wakumbuka simu wewe? watu waliita kila jina mshindi, sijui mbunju, ikiwa ndogo kiberiti-I miss my T600 Sony erricson enzi za meta mbeya duuh tumetoka mbali sana.Kuna mtu akiona hii post lazima aangue kicheko hehehehe!! (lol!) ...Nahisi hii itakua N 12000!!! halafu simu za hivi nimewahi ona simu moja salio laki 5 lakini simu ndo kama unavyoiona hapo akikupigia inabidi ukae na charger karibu maana itakuishia na mwingine ana Blackberry kali kweli kweli hata ku beep hai beep!!! so sad ! sijui hata hua wananunua za nini?!!

Lugha gongana...

Yani unaweza mdhibiti mtu kwa makofi kumbe yuko sahihi.Tuangalie matumizi ya lugha na watu unao ongea nao ni MUHIMU SANA!!!!.. ''YOU'' kidhungu na ''ME'' Kwani kichina china ''YU'' ni jina na ''Mi'' laweza kua jina pia.tujiunge

16 May, 2010

Hesabu za ajabu!!!!!!!!!!

Kama Hesabu zenyewe ndio hizi kuna haja ya kufuta zisiwepo kabisa hahahahaha japo tumaneno tunaonekana tuna ukweli ndani yake lol! sasa sijui ukweli uko wapi.Hebu tazama jamaa alivyo kokotoa DADA ZETU hapo halafu nipe comment ukweli wa maneno ukoje.Nimeona si vibaya kusikia maoni ya wengine kuhusiana na ujumbe uliomo kwenye hesabu ya ajabu kabisa kama inavyo onekana hapo. Hii naifananisha na ile mtu anaye kunywa (mnywaji wa pombe aka mlevi) ukimwambia bei ya kitu fulani anaanza kutoa comparison na bei ya pombe. Mfano ukisema mkanda wa suruali unauzwa Tshs 4000/= yeye atasema, haaaaa 4000/= yote hiyo unajua hapo nisawa na beer ngapi? hahahahaha. sasa nimeshindwa kuelewa hii mwana mahesabu ana maanisha nini...toa maoni yako tafadhali yani mie huku sina mbavu lol!



When a girl..........

How true is this? Girls can you justify? Kuna wengine ukute anakuangalia kwa makini ukadhani yuko pale kumbe hata hayuko, aliko anapajua mwenyewe na roho yake. Funny stuff and confusing of course!!...Girls have you are say hua mko wapi? je hayo maneno ni ya kweli? au mmependelewa tu lol!

13 May, 2010

Burudani anga za bongo flava..

Watu walisema sana kama huu muziki wa kizazi kipya hatutafika popote/mbali kutokana na watu kuingia kwa fujo/kasi lakini siku hadi siku wazidi kufanya vizuri na hatimaye kupiga hatua japo sio kwa wote. Ni vizuri kuona vijana walio wengi wanapata kujiajiri kupitia nyanja hii japo sio wote wameweza kutoka kimuziki.Si vibaya kuwapa moyo ili waweze fanya vizuri zaidi.Ukiachia mbali burudani muziki unaweza kuelmisha kwa kufikisha ujumbe mbalimbali kwa jamii.Kwa maana hio basi tunategemea kuona wahusika wakiwa wamejipanga kutoa burudani, elimu n.k

Nimependa collabo hii ya Albino fulani, Sugu, mwana FA, na Belle9 katika wimbo NAFASI.Mistari yote iko poa kwa mtazamo wangu ila nimeguswa na mistari ya FA eti ''wafungwa wangetembelewa na mademu na wake zao'' hili nalo ni neno hivi wale jamaa kule jela SEGEREA na kwingineko wanaishi vipi ukizingatia kama binadamu wanapata hamu ya kufanya mapenzi! Mbaya zaidi wengine wameacha wake zao wapendwa na wa ndoa kabisa huko majumbani.Kuna habari zisizo rasmi kugeuzana huko jela je wimbi la mashoga litaisha kweli kwa mtindo huu?? sasa hivi ukiingia chatrooms za kiswahili hukosi shoga ni wengi hadi kero lol..japo hata chatrooms za kiingereza wapo inashangaza kwa Tanzania nchi changa kabisa kua na kiasi kikubwa cha mashoga....hali kadhalika wale wa kusagana nao wazidi ongezeka sijui tunaelekea wapi?!..well turudi kwenye track/muziki huu wa kizazi kipya.

Wanasema penye nia pana njia pamoja na kwamba vijana wengi wanapenda kuingia katika muziki bahati mbaya wachache ndio wana ng'ara siku hadi siku wakati wengine ndio wanapotea.Lakini ni mambo ya kujipanga tu wazuri katika fani hii wata ng'ara na wale wasiojipanga watapotea KIMYA KIMYA...Hivi yule Mr Nice na takeu style yuwapi? Alitamba na vibao ''FAGILIA,KIDALI POA,YEBO YEBO na nyingine nyingi. Wapi Hard blasters? Uswahilini matola waliwahi tamba na kibao 'KOSA LA MAREHEMU', wapi Mwana wa komba (Caz-T)- aliwahi tamba na kibao ''NAKUHITAJI'' n.k aaah nimesahau wengine wengi nikikumbuka nitawataja au kama vipi nitajie lol.




Ujumbe huhusu simu za mkononi hahahah hawa jamaa nyimbo zao hua sina mbavu, wasikie mwenyewe mimi sina la kuongeza zaidi ya kusema tu kua makini na simu yako maana wewe ndo waijua namna unavyoitumia na namna inavyokusaidia kwa ishu zako za kila siku.

Yanayo jiri kwenye inbox zetu..

Dearest,

I am writing this mail to you with tears and sorrow from my heart.I will really like to have a good relationship with you, and i have a special reason why i decided to contact you.

I decided to contact you because of the urgency of my situation here ,I am Miss jenet Harry Johnson 25years old girl from Liberia,the only daughter of Late prince Harry Johnson the deputy minister of national security under the leadership of president Charles Taylor who is now in exile after many innocent soul were killed ,My father was killed by government of Charles Taylor ,he accuse my father of coup attempt.

I am constrained to contact you because of the maltreatment I, am receiving from my step mother. She planned to take away all my late father's treasury and properties from me since the unexpected death of my beloved Father.Meanwhile I wanted to escape to the Europe but she hide away my international passport and other valuable travelling documents.

Luckily she did not discover where I kept my father?s File which contains important documents. So I decided to run to the refegee camp where I am presently seeking asylum under the United Nations High Commission for the Refegee here in Ouagadougou, Republic of Burkina Faso. I wish to contact you personally for a long term business relationship and investment assistance in your Country.My father of blessed memory deposited the sum of US$5, 7,Million Dollars in Bank with my name as the next of kin.However,

I shall forward you with the necessay documents on confirmation of your acceptance to assist me for the transfer and investment of the fund.As you will help me in an invsetment, and i will like to complete my studies, as i was in my ist year in the university, when the crisis started.It is my intention to compensate you with 10% of the total money for your services and the balance shall be my investment capital.

This is the reason why I decided to contact you.Please all communications should be through this email address only for confidential purposes.As soon as I receive your positive response showing your interest I will put things into action immediately In the light of the above, I shall appreciate an urgent message indicating your ability and willingness to handle this transaction sincerely. iam staying at the female hostel. Awaiting your urgent and positive response.Please do keep this to yourself and every cummicationshall be made throuh this email address alone for comfidetial purpose and you should notdisclose it till i come over , once the fund has been transfered.

Thanks,I will send you my pictures as soon as i Read from you again please tell me more about yourself.
Yours Love Sincerely,
Miss Jenet Harry Johnson.


NB: Huu ni wizi tu hakuna kitu hapa, ukipata hii as usual delete tu halafu kaa kimya

10 May, 2010

Hongera sana Ernest Makulilo


(Picha toka Facebook)

Napenda kutumia fursa hii kukupa hongera Mdau Ernest Makulilo kwa hatua uliofikia ya kufunga pingu za maisha na kuachana ukapera. Japo sijajua watu ( wabongo) wanataka nini hasa waonapo mtu anafanikiwa ama kufanya jambo fulani zuri huishia kuponda na kutoa comments zinazo katisha tamaa! Yaani sasa imekua kama ndo msemo mtu akioa mzungu anataka PAPERS aka MAKARATASI!!! Hua nashindwa kupata jibu kama kwa sasa watu wameanza kupanga maisha ya mtu mwingine ama Mungu pekee ndio anaweza panga?? Na kwanini mtu aponde wakati maisha ni ya kwako si yake na wala haya mhusu?! kwanini kila asiangalie maisha yake?

Nilipoona hii '' MZEE WA NONDOZZZZZZZ ERNEST MAKULILO NA MARIE WAMEREMETA'' nilifurahi lakini nikawa na shauku kuona comments ambazo zilikua nyingi kabisa... kwa muda huo zilikua 52...nilitegemea kuona HONGERA nyingiiiii lakini cha ajabu na kilicho sikitisha zaidi karibia kila comment inasema MAKARATASI,MARA SIJUI AGE IS JUST A NUMBER!!! what is this for? kwa mtindo huu ninathubutu kusema kuna watu wataishia kusema ya watu na kushindwa kufanya yao....kwani MAKARATASI NDIO NINI? MTU BILA MAKARATASI HUWEZI ISHI? wewe maisha yake yanakuhusu nini? kwanini kama huna cha kuongea usikae kimya??!!

LAZIMA TUFIKE MAHALI TUKUBALI MATOKEO...Mtu sijui niite HATER anatoa comment kama hii '' nasikia harufu ya MAKATARATASI AU hapo hakuna kitu ila MAKARATASI halafu mwisho anamalizia HONGERA SANA!!! Kama sio unafiki ni nini??!! kwahio mtu anaponda huku anakubali kimoyo moyo..kiukweli sio nzuri wenye tabia kama hizi ni vema wakabadirika kwani ni wazi kwamba mtu ukiwa na roho ya korosho hutakaa uendelee utabaki kusema ya watu tu, fanya yako..kila mtu ana yake FANYA YAKO!! na ukiwa huna cha kuongea ni vema KUKAA KIMYAA HAIKUPUNGUZII CHOCHOTE kuliko kumaliza muda wako kuongea ya watu!! ( yani comments zimenichefua utadhani nasemwa mimi hahahhaha!!)


(Picha toka Facebook)

picha zaidi toka facebook>>>
http://www.facebook.com/photo.php?pid=12573404&id=623205200

Binafsi natumaini Mungu atakubariki zaidi na maisha yatakua mazuri kwa sasa na huko mbeleni maneno ya watu ni kama mbu nje ya net au kelele za vyura ambazo hazizuii ng'ombe kunywa maji mtoni hehehe!. Pamoja na mambo mengine umekua mtu wa kujitolea kutoa habari mbalimbali za vyuo na scholarship ambazo zimesaidia watu mbalimbali katika kujipatia habari za namna hio kupitia blog yako
ni imani yangu wapenda maendeleo watakubaliana na mimi katika kutambua mchango wako katika swala zima la elimu. Kwa kupata habari zaidi za scholarships tembelea
-------------------------------------------------------------------------------------
http://www.makulilo.blogspot.com/ na
http://scholarshipnetwork.ning.com/

06 May, 2010

Nilihisi masikio yanakosea kusikia...

Ngoja nicheke kwanza (hahahhahahhahaha uwiiiii) leo nimekutana na hii na mdhungu:-

Me: hello!
Mdhungu: hi, you alright?
Me: yeah I’m good thanks!
Mdhungu: how is your day…..busy?
Me: I’m always busy sir
Mdhungu: ok… you must be a hard working man
Me: Exactly (I laughed a bit lol)
Mdhungu: are you from Africa?
Me: yes
Mdhungu: who is the president of Africa?
Me: I was like…F**** hell, say it again (I pretended not to have heard the question very well)
Mdhungu: I said who is the president of Africa?
Me: Africa is not a country …Is a continent man (lol)
Mdhungu: really? Well ermm is there houses?
Me: (I wanted to say NO basi tu) yes better than those we’ve here
Mdhungu: No it cannot be possible, a friend of mine told me is just like a forest
Me: google it you will see….
Mdhungu: ok
Me: have you ever been outside UK?
Mdhungu: No, I can’t afford going anywhere may be Spain
Me: hahahaha ok

Yani mie sijawahi fikiria kuna wazungu wajinga kiasi hiki,mtu anajua Africa ni nchi??? Cha ajabu zaid hata haamini kama kuna Mungu duh. Ivi hawa wazungu/watu weupe si ndio walileta dini ya kanisani na misikitini kulikoni wao wanaikacha sasa hivi? Kweli duniani kuna mambo yani sikua na mbavu na huyo mzungu. Ila katika kuongea na wazungu mbalimbali inaonyesha wazungu ambao hawaja wahi toka nje ya UK ni wabaguzi kidogo

05 May, 2010

Lack of sleep 'linked to early death' wana sayansi wamesema!

Inasemekana kulala chini ya masaa sita si nzuri kwa afya yako na inapelekea mtu afe mapema. Wana sayansi hao wametoa ripoti hio baada ya kufanya tafiti 16 zilizo husisha watu/washiriki 1.5 million. Ripoti inasema 12% ya watu wanao lala chini ya masaa 6 wapo kwenye hatari ya kufa mapema zaidi kuliko wale wanaolala muda ulio shauriwa kulala.

Hata hivyo kulala zaid ya masaa 9 imehusianishwa na kudhoofika kwa afya. Hii ina maana kulala sana pia kuna pelekea kufa mapema (Professor Francesco Cappucio head of the Sleep, Health and Society Programme at the University of Warwick) amesema.

Wana sayansi hao walimaliza kwa kusema kadri siku zinavyo kwenda watu wengi wamekua wanachelewa kulala kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kujishughulisha zaidi na kazi kwa masaa mengi kutokana na msukumo wa kijamii katika swala zima la kutafuta na kumudu maisha ambayo yamekua magumu siku hadi siku. Ripoti imetolewa baada ya kujumuisha tafiti 16 zilizo fanyika UK, US, EUROPE na ASIA na kutumia zaidi ya watu 1.3 Million.

Aidha watu laki moja wame ripotiwa kufa kutokana na sababu za kutolala kwa muda unaotakiwa ama kulala sana kupitiliza muda ulio shauriwa.

Hapa lile kundi la walevi aka wanywaji au walipa kodi wakubwa kupitia pombe wako hatarini kwa sababu unakuta mtu anakunywa hadi usiku wa manane wakati huo huo asubuhi anaingia kazini.

wale wakusoma mashuleni(wale wakusoma & walimu), dukani kuuza( wafanya biashara)Internet cafe (wale wanaomiliki ama kufanya kazi aina hizo za ofisi) bila kusahau wanao penda kuchat kwa muda mrefu (msiniseme LOL..), wahudumu sehemu mbalimbali za huduma za kijamii kama Guest house, Hotels,Bar, Night/late Clubs,casino na nyingine nyingi sana waweza zitaja

Niliwahi andika article ya the Value of time nadhani inaweza kua suluhisho kwa wanao kesha bila sababu za msingi na hatimaye kuto lala vizuri kwani hakuna bank ya kuweka muda eti nitautumia baadae, hio haipo cha msingi ni kupanga mambo yako vizuri ili ikifika saa ya kulala ulale!.


unaweza soma zaidi yahoo uk news on Lack of sleep 'linked to early death'

Ash Clouds returns to the UK.

Some airspace in the UK have been closed again due to the cloud of volcanic ash from the Iceland which has once again returned leading to disrupted passengers travel plans. Flights affected of the same include those over parts of Scotland, Northern Ireland and the Republic of Ireland. Similarly, Glasgow, Edinburgh, Dublin and Belfast International are amongst the airports affected. Glasgow flights resumes on Thursday 0100 whereas Edinburgh resumes 1900 tonight. However the Civil Aviation Authority (CAA) will give updates after 1800.

Last month, the ash cloud forced the closure of much of Europe's airspace for almost a week. Thus this time, the CAA says passengers should contact their airlines to check whether their flight is operating. At the same time passengers are warned of the EMAIL SCAMS targeting passengers whom their travel plans been disrupted by the ash. Hence, they are advised to delete any message asking for personal details including passport information for refund. Instead all inquiry/claims have to be directed to the airline first for further details.

(Source: uk news/yahoo.com)

Read more at http://uk.news.yahoo.com/5/20100505/tuk-new-no-fly-zone-as-ash-cloud-returns-45dbed5.html

02 May, 2010

Juma pili njema wote

Ni matumaini yangu wote muwazima kabisa na mnaendelea vizuri na mapumziko ya mwisho wa wiki .Hali kadhalika wenye shida mbalimbali na wagonjwa nawapa pole (kama wapo). Ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa kila jambo maana yeye anajua hata kile ambacho hujafanya ama unakusudia kufanya. Ametoa hewa ya bure ambayo tunaivuta kila siku na maisha yana kwenda kwa namna ya pekee kwa kila mmoja wetu. Kwanini tusimshukuru? Leo sina jipya nawatakia tu jumapili njema na mmalize week end kwa aman na familia zenu au mtu yeyote aliye karibu yako katika kuimaliza hii wiki (Ndugu, jamaa na marafiki n.k). Ujumbe wa leo:-

Delight yourself in the Lord and He will give the desires of your heart.
Psalm 37:4


Ujumbe huo usindikizwe na ''Trading my sorrows'', ''Butu na moyi'' na ''around the corner''. Enjoy!