Sudan ilikua ni nchi ambayo imekua na mvutano na mapigano ya hapa na pale kati ya Sudan kusini na kaskazin kwa muda mpaka Sudan ya kusini ilipoamua kujitenga na kujiita Taifa linalojitegemea japo halikutambulika na Umoja wa Mataifa (UN) ama Umoja wa Africa (AU).Hatimaye mnamo July 9,2011 Sudan ya kusini imetambulika na Umoja huo kama taifa huru na kufanya bara la Africa kua na jumla ya nchi 54.
Kushoto ni Rais wa Sudan kusini Jenerali Salva akiwa na Rais wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete katika hafla ya uhuru wa Sudan Kusini
Kutambulika kwa uhuru wa Sudan ya kusini ni njia moja wapo kuzuia umwagaji damu uliodumu kwa muda mrefu ambapo UN na AU zimeridhia na kutambua hatua hio kama njia ya kuzuia machafuko zaidi..Ripoti ya BBC inaonyesha takribani watu Million moja na nusu wamepoteza maisha.Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alikua moja ya viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za uhuru mjini Juba ambapo Jenerali Salva Kiir Mayardit ndio Rais wa kwanza wa Sudan ya Kusini.Ujumbe wa umoja wa mataifa ulikua ni kulitambua Taifa hilo jipya na kushirikiana nalo japo changamoto ni nyingi hasa kuwepo kwa vikundi kadhaa vya waasi, elimu duni na mengineyo (BBC).Kwa habari zaidi SOMA HAPA