14 July, 2010

Burudani yasogea Coventry na Mb Dogg..

Bongouk this time naona wamechachamaa na kuleta wasanii wa kibongo hapa UK.Kwa kua stress ni nyingi inchi hii bila shaka ni jambo jema kupata burudani za hapa na pale kupunguza stress ambazo zina changia kwa kiasi kikubwa watu kuzeeka kabla ya umri wao.Ni imani yangu kua hilo limezingatiwa kitu ambacho kita leta utofauti na wenzetu wazungu ambao kila siku wengine hujirusha kwenye mito na kufa ama kupigana risasi kutokana na stress za hapa na pale hata kwa kisa kidogo kabisa.

Kwa waliopo UK nadhani hili sio jambo geni japo natambua hata waliopo bongo wanaona kupitia vyombo mbalimbali mbalimbali vya habari namna watu wanavyo chukua sheria mkononi kutokana na stress. Pamoja na kupunguza stress matamasha ya muziki kama haya yanawezesha kukutanisha ama kufahamiana kwa watanzania wengi waliojaa na kuendelea kuja nchi hii.Pamoja na mambo mengine Coventry ni mji wenye watanzania wengi ambao kwa bahati mbaya wengi wao hawafahamu ama hawataki kuwafahamu watanzania wenzao kwahio ni imani tu kupitia matamasha kama haya wanaotaka kufahamiana watafahamiana vizuri.

Kwa mujibu wa habari zilizo nifikia ni kwamba MB Dogg atakua LIVE in Coventry jumamosi ya tarehe:17.07.2010 mahali ni 116 Forgosford street:Palms Bar iliyopo CV1 5EA katika jiji la Coventry-United Kingdom.wapenda burudani wote mnakaribishwa kiingilio ni 10£ tu. Muda kuanzia 9Pm- 4Am.

Difficult Interview questions ...1

Watch this video clip thoroughly well, I hope it will be of great help to job seekers when prepares for an interview.Keep in touch with 'The Network' blog for more interview tips




(Jobstreet.com)

Ushawahi sikia Radio Mbao???!!!

Kuna kipindi nilisoma mahali kua kuna Radio inatarajiwa kuanzishwa na inaitwa Radio mbao nikadhani ndio zile kama wanavyoita magazeti ya udaku.Lakini nimejaribu isikiliza kwa wale wanao sikiliza Bongo Radio basi Radio mbao haitakua na tofauti kubwa kwani zote ni Internet based Radio. Pamoja na jina la Radio hio kua la ajabu nina imani watu wengi wamevutika kuisikiliza na kwa wale tunaopenda muziki basi ukifungua 'Radio Mbao' utaburudika vya kutosha.

Na kwa wale waliokua hawajui kama iko LIVE HEWANI basi mnaweza isikia wenyewe hapa
http://cp.radiostreamhost.com/radio/player.php?station=kpentertainment&nc=5976812