Bank kuu uingereza kuchunguza mali au pesa yoyote inayohusiana na Gaddafi na serikali yake.Imedaiwa kuwepo kwa mabillion ya dola nchini humo kutoka serikali ya Libya pamoja na Gaddafi mwenyewe.Kwa ufupi imebainika kuwepo mali zenye thamani ya pauni Billion 20 ikiwemo pauni Million 10 ya jumba la kifahari lililopo jijini London.Huo kwasasa ni mpango wa serikali ya Uingereza kumlazimisha aachie ngazi kama wananchi wake huko Libya watakavyo.
Tamko hilo la serikali limesisitiza kwa kuwatoa raia wake kwanza toka Libya na baada ya kumaliza ndio uchunguzi wa kina kutaifisha mali za Gaddafi na serikali yake kuendelea.Wakati huo huo Gaddafi amekaririwa akisema wasishangae yeye kuongoza nchi muda mrefu mbona hawashangai Queen?.Alimalizia kwa kusema ataongoza nchi hio mpaka ifikie miaka 57.Pia wataalamu wa umoja wa mataifa wamedai inawezekana zaidi ya watu 3000 wamepoteza maisha nchini Libya kutokana na vurugu za kisiasa zinazo zidi shamiri ichini humo.(Telegraph)