21 July, 2011

ATI UTANI KWA WAHEHE....JE NI SAWA?

Ukiangalia kwa haraka unaonekana kama ni utani lakini ukitafakari huu ni uchokozi wa maksudi katika kubeza makabila.Leo katika blog ya rafiki yangu Mwanasosholojia nimekuta utani kuhusu kabila la Wahehe ambao si vibaya wasomaji wake tukafaidi na nikaona si vibaya na sisi hapa kuona mawili matatu.Kiukweli nimecheka sana japo sijaufurahia utani kama huu kwani unanigusa kiasi fulani na kinacho kera zaidi mtu ukimwambia unatoka Iringa cha kwanza kusema ni ''eeh nisikuuzi usije jinyonga bure'' au ''eheee kwahio unakula mbwa??''

Kiukweli sijui kama Wahehe wanakula mbwa maana sina ushahidi ila nasikia tu watu wakisema.Hua pia najiuliza kama wahehe ndio wanakula mbwa kwanini iwe wote watokao Iringa wahusishwe kubezwa kiasi hiki? Iringa kuna makabila mengi yakiwemo Wakinga,Wabena,Wahehe,Wapangwa n.k. No offense intended kama kuna mhehe unasoma hii habari labda niulize hivi kweli Wahehe mnakula mbwa??   Yaani hii chini ya mshale
                                  Nataka kujua tu msini elewe vibaya!

Swala la kujinyonga (suicide) lipo kila mahali kwa makabila yote mpaka wazungu wanajinyonga sasa sijui nao ni Wahehe?.Mtazamo wangu hili linaweza kua la kihistoria zaidi ukizingatia aliyekua Chief wao Mkwawa alijinyonga ili asitiwe mikononi mwa Wajerumani akiwa hai.Lilikua jambo la kishujaa zaidi ambalo pengine ndio chimbuko la mwendelezo wa kujinyonga baina ya Wahehe kwani pengine ni ushujaa kufanya hivyo.Lakini mpaka sasa si Wahehe peke yao ndio wanajinyonga ni mtu yeyote bila kujali kabila anaweza jinyonga kwa sababu zake binafsi au kutokana na jamii inayomzunguka,matatizo n.k.Well ni mtazamo tu tujiunge na tangazo hapa chini kwa imani kua ni UCHESHI TU NA SI VINGINEVYO!!


TANGAZO KWA WAHEHE WOTE:
Chuo kipya kabisa cha Kihehe kimefunguliwa Kihesa, Iringa.(HEHE SKILLS AND TECHINICAL COLLEGE OF LIFE)

Kinatangaza kozi za mwaka 2011/2012 kama ifuatavyo,1.Kugema ulanzi miezi 6
2.Kusokota kamba za kujinyonga miezi 9;  3.Kuchagua mbwa anaefaa kuliwa na mapishi yake miezi 8;  4.Kuongeza hasira miezi 10-12Atakae jiunga mapema atapewa kozi ya upishi wa Mkunungu pamoja na uoshaji wa Mbeta.

ASANTE KAKA MWANASOSHOLOJIA,KWA HABARI ZAIDI MTEMBELEE HAPA

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA ATOA UFAFANUZI SWALA LA UMEME

KUSIKILIZA UFAFANUNUZI WA TATIZO LA UMEME TANZANIA KUTOKA KWA MHESHIMIWA RAIS MH JAKAYA MRISHO KIKWETE FATA LINK HAPO CHINI ALIVYO HOJIWA NA MWANDISHI WA BBC BWANA OMAR MUTASA.RAIS ANASISITIZA WATANZANIA MUWE NA SUBIRA SERIKALI INAFANYA JITAHADA KUBWA LAZIMA WATU WATAMBUE NA KAMA KUNA MTU ANA MAARIFA YA HARAKA KATIKA KUTOA UFUMBUZI WA UMEME BASI AYATOE SERIKALI ITAYAFANYIA KAZI.


ZAIDI SIKILIZA RAIS AKIFAFANUNUA KUHUSU UMEME KWA KUBONYEZA HAPA





KISONONO SASA HAINA TIBA!!!!!!!!

Kuna habari kuwa wana sayansi  huko Japan wamegundua kuwepo kwa jamii ya gonorrhea (kisonono) ambayo haitibiki kwa dawa zote ambazo awali zilikua  zikitibu gonjwa hilo.Jamii hio iliyopewa jina la H041 imewaacha madaktari midomo wazi kwani dawa zilizopendekezwa hazitibu tena na kuwafanya wajaribu kutumia dawa zingine ambazo hazikujaribiwa kutibu ugonjwa huo ili kutafuta suluhu ya ugonjwa huo ambao umedaiwa kua tishio jipya idara ya afya siku za usoni kama tiba haitapatikana.


Gonorrhea hapa Uingereza ni ugonjwa uliozagaa sana pamoja na Chlamydia (klamidia) ambayo yote ni magonjwa ya zinaa maarufu na umaarufu wake unakua siku hadi siku ukiumwa daktari hata hashangai!!.Magonjwa haya unaweza yapata kwa kufanya mapenzi bila kinga na muathirika.Kwa maana hio mambo ya kusema huniamini na blah blah kama hizo LAZIMA TUZIACHE VINGINEVYO HALI ITAKUA MBAYA NA HUO UTAKUA MKATABA WA MIONDOKO YA BATA WAKATI WA KUTEMBEA (usicheke ila ndivyo ilivyo ukiupata)


Kibaya zaidi ukishapata haya magonjwa uwezekano wa kupata HIV/AIDS na magonjwa mengi ya zinaa ni mkubwa.Na kujua kama umeupata inachukua siku 5 hadi 30  dalili ni pamoja na kusikia maumivu unapokojoa (kwa wanawake/wanaume), kutokwa usaha wa njano kwa wanawake na kuvimba korodani kwa wanaume.Aidha kwa wanawake wakati mwingine hakuna dalili yoyote ukiupata zaidi ya kua na uwezekano mkuwa  wa kuharibika mimba mara kwa mara, kuzaa kabla ya siku au ugumba wakati kwa wanaume inaweza pelekea kansa  ya kibofu (prostate cancer).


Kwahio tucheze salama ndugu zangu!


Zaidi kwa lugha ya kiingereza soma HAPA na HAPA