07 September, 2011

RAFIKI ZANGU WAKUMBANA NA FRAUD!!!!

Wanasema kuuliza sio ujinga na ni kweli rafiki zangu wawili wakumbana na michezo ya wizi mitandaoni lakini wakaamua kuuliza baada ya kupata wasiwasi na kushinda pound kibao na wakati huo huo kutakiwa kutoa kiasi kidogo cha pesa ili wapewe pesa wanazo dai wameshinda.Sasa mie najuuliza kama nimeshinda kweli si wapunguze zile ambazo nimeshinda na zilizo baki wanipe kwanini wanataka niongeze pesa? well tujiunge na kisa hapa chini


Mdau  wa kwanza:
 To: rijaki@ymail.com
Sent: Sunday, 4 September 2011, 14:51

Leo nimepata email toka huko uingereza kwa mtu aliyejitambulisha kama Angelina Keith mwenye umri wa miaka 87 ambaye mumewe alikufa kwenye ajali ya ndege. Kwa kuwa walikuwa na uwezo sana basi sasa anadai ameamua kuishi katika ranch yao na karibu asilimia 30 ya mali zake amegawia charity mbalimbali na kiasi kingine ameandikia check kwangu na kuiacha DHL london kwa lengo la kutuma huku. katoa jina, namba ya simu na namba ya siri ya bahasha (brown envelope) yenye hiyo check nikatuma email kwa hao DHL wakasema ni kweli kuna hiyo bahasha ninachotakiwa ni kupeleka taarifa zangu kama jina, anuani namba siri na kisha nitatakiwa kulipia security fee pound 160 kisha wataleta.


 Nimeona kama vile hata wazungu wanaweza kuwa matapeli hebu niambie aina hii ya wizi ipoje hapo Uingereza. maana nimepiga simu yamepokea na kufuatilia kisha yakajibu lakini nimeona haiji akilini.....................Nikamshauri aachane mara moja na hao wezi mitandaoni kama haitoshi mdau huyu akataka kujua zaidi kwa kufuatilia DHL ndipo akabaini mchezo huo wa wizi na akanijibu......


Tuesday, 6 September 2011, 10:01


>>>kweli bwana majamaa haya ni majizi inavyonesha maana yanajifanya yanafanya kazi DHL Express lakini nimefungua mtandao wa DHL sijaona namba za simu yenyewe yanapiga simu karibu kila siku kuulizia nimelipa na kama nimelipa ni scan risiti ya malipo nitume kwa mtandao haraka.


Mdau wa pili:
Huyu alianza na kuulizasorry,eti unafahamu mashindano ya iphone mobile promo,mama yangu katumiwa meseji ya kushinda unaweza kunichunguzia maana isije ikawa matapeli,naomba 
uniulizie,kama ni kweli


*Nikaomba kupata maelezo aliyopata kwenye ujumbe nayo ni:-


message imetoka iphone mobile promo UK, iliandikwa kuwa your cell phone number has won 715000 pounds from I- PHONE-UK,for claims of prize wakatutumia email iphoneclaims @gmail.com.ss tulivyo watumia meseji ya kupata huo ushindi waka tutumia verification form ambayo tulijaza jina la mama,namba ya cm ya ushindi anuani,network name ,maana wanasema ni mashindano ya kwanza yaliyo tumia automated ramdom computer kwa kutumia namba za simu,sasa walipotoa option ya kupata pesa kuna ya kufuata huko london hadi adress wametoa,au njia ya ndege ambayo ni cheki au kutumia bank ya western union .sisi tuliomba watumie njia ya barclays ,wametutumia form ya barclays lkn ukitumia njia hiyo wanatuma kama dollars.na mtu ambaye amepewa jukumu hilo ni stephen elop na namba za simu wametoa ambazo ni+4915118186861
naomba unitafitie maana wametoa hadi Adress zao za hapo london na iko under BRITISH LAW.



**Ndugu wasomaji hizi ni fraud (kudanganya ili kupata pesa) na nime post nyingi sana katika blog hii.Wanaweza kukupata kwa njia ya simu,email au hata barua kwa njia ya posta kwa hio ukipata ujumbe kama huo si vibaya kuuliza au kuupotezea ukifanya kimya kimya basi jiandae kulia kilio cha samaki!!.Dar es salaam na sehemu nyingine watu wameibiwa eti mtu anakuambia ananunua paka mweusi kwa MILLION 2 hivi mtu huwezi shituka kama ni wizi unataka kufanyika?.Kiufupi nimefurahishwa na hawa ambao wameuliza na nimesha wajibu huu ni wizi tu wa mitandaoni waachane nao**


Kwa habari zaidi kuhusu fraud bonyeza HAPAHAPAHAPA HAPA NA HAPA