17 May, 2010

Sheria na Alama za barabarani..

Hivi bongo ni lini tutakua na vizuizi katika makutano ya train na barabara za magari? pamoja na kwamba kuna madereva naita wapumbavu kwakutoa zingatia alama za barabarani. Hawa ndio wana sababisha ajali na kufanya ziendelee kuwepo kila siku na kugharimu roho za watu wengine.Angalia huyu kwenye video sijui anawaza nini get limefungwa lakini kapita hivo hivo.Ni muhimu yakawepo kwa wale wasio zingatia alama za makutano ya njia za train na barabara za magari. Hata hivyo wanao kiuka ama kutofata alama za barabarani ni wengi ona huyu angekufa hapo sijui angemlaumu nani. Na pia adhabu iwe kali ili sheria ifuatwe.

Ona huyu yani so stupid! nasikia kuna police traffc hua wanapiga makofi sijui kifungu gani cha sheria kina waruhusu kupiga lakini kwa dereva kama huyu mtu yeyote angeshawishika kupiga japo yeye mwenyewe alikua hatarini kufa au hata kusababisha mauti kwa wengine.Iangalie hii Video uone..




Nimependa sheria ya hapa UK kwani usipo fata sheria una punguziwa points kwenye leseni yako na mwisho kama unaendelea kufanya makosa barabarani basi unakua banned kuendesha.Hii nchi kuna discipline nzuri kwa upande wa ufataji wa sheria dereva mataa anasimama, bongo mataa unakuta jitu limetoka huko taa nyekundu anapita tu kisa kaona hakuna gari upande wa pili. Si wote wanafanya hivyo ila wanao fanya hayo wapo nimewahi ona kwa macho yangu! eti hapo mtu akamatwe umwambie fine 20,000/=
haisaidii kwasababu makosa kama hayo yataendelea kutokea.kwanini utaratibu huu usiwekwe wa vunja sheria za barabarani wakabaki kuendeshwa tu?.Na pia sheria kama ipo basi ifuatwe na kila mtumiaji wa barabara ile bila kujali wadhifa au aina ya gari anayoendesha.

Sasa kichekesho kwa mfano unakuta mida ya foleni asubuhi na jioni mtu mwenye tuseme suzuki vitara kapita service Road basi ata kamatwa na hata kucheleweshwa anakoenda. Wakati huo huo utaona mwingine kakatiza na VX lake anapungiwa mikono tu kana kwamba yule ni mtu zaidi kuliko walipo kwenye foleni. Na hapo usikute hana lolote anawahi zake bar ama nyumba ndogo (mtanisamehe wenye nazo)> Sielewi ile wanaita Equality before law kama inafanya kazi sawa kwa watu wote ama ni kwa baadhi tu hasa WALALA HOI!! Kwasababu kama watu wote wako sawa mbele ya sheria kwanini mwingine tena ukute ni kiongozi kabisa na akili zake anafanya hivyo sasa sijui niseme viongozi wako juu ya sheria ama sheria inatumika tu kwa wasio maofisa?

David Cameron, waziri mkuu mpya wa sasa wa Uingereza aliunga msafara wa foleni kali zinazo zidi kukua siku hadi siku hapa UK bila kujali.Nadhani pamoja na kuhatarisha maisha yake kama walivyodai maofisa wake wa usalama aliweza kuzingatia umuhimu wa watu wake na japo kuonja adha ya foleni hata kwa siku moja tu.Kwani wangetumia ule mtindo wa escort basi foleni ingekua mara mbili zaidi kwani magari yote yangetakiwa kupisha kitu ambacho yeye hakupenda kitokee Soma zaidi hapa http://http//www.dailymail.co.uk/news/article-1278618/Security-fears-Cameron-ditches-police-outriders.html.Si vibaya viongozi wetu wakajifunza kutokana na mfano huo kwasababu kama wewe ni mtu wa watu kweli kwanini ukimbie kimbie na kuwaongezea walipa kodi wako foleni. Inamaana baada ya kuchaguliwa wale walio kuchagua wanageuka kua maadui? Na kwanini uwasumbue kwa kuwaongezea foleni? mimi hii hua naona ni sawa na baba kumpa mwanae pesa akalewe huko akirudi amsumbue tena baba yake kwa kumsemea mbovu, kumtukana ikibidi kumzaba makofi.

Viongozi ni muhimu na raia pia kwani ndio wapiga kura na ndio walipa kodi. Kimsingi katika utawala wa kidemokrasia raia ndio ma-boss na wenye nguvu japo katika nchi zetu nguvu walizo nazo ni kuchagua mtu kukaa madarakani na sio kuchagua anaye takiwa atoke hata muda wake ukiwa haujaisha. sitaki kuongea sana ila tu sheria ifuatwe sio wengine wawe juu ya sheria na kua watu zaidi linapo kuja swala zima la uvunjaji wa sheria. Mwisho kabisa sheria za barabarani ziwekewe utekelezaji mzuri na adhabu iongezwe ili kupunguza ajali za barabarani.Ni hayo tu kwa leo

No comments: